TRANSLATE THIS BLOG

Monday, January 7, 2013

Saunders;Kocha mpya Wolves

Klabu ya Wolves imethibitisha kwamba  Dean Saunders ndie meneja mpya wa timu hiyo hii nikufuatia kutimuliwa kwa aliekuwa kocha wa Wolves Stale Solbakken kutimuliwa siku ya jumamosi.

Dean Saunders Doncaster Rovers

Saunders, 48, ameiwezesha  Doncaster Rovers kusalia nafasi ya pili katika  League One msimu huu na alianza kazi ya kuwa meneja akiwa na timu ya Wrexham.

 Taarifa kutoka ndani ya klabu kupitia tovuti yao imesema: "Wolves  wanapenda kuwafahamisha kwamba Dean Saunders ndie atakuwa meneja mpya . Doncaster Rovers wamekubali kumuachia kocha huyo mwenye umri wa miaka 48 kuelekea  Molineux kufuatiwa kutimuliwa kwa aliyekuwa mwalimu wa timu hiyo Stale Solbakken siku ya jumamosi."

 Saunders ni boss wa nne wa  Wolves katika kipindi kisichopungua mwaka mmoja hii ni baada ya mwezi wa pili kutimuliwa kwa Mick McCarthy na kufuatiwa na and the Terry Connor.

YADAIWA FERGIE ANASAKA KIPA MPYA!!

WALENGWA NI BEGOVIC & REINA!

GAZETI la Uingereza, The Mirror, limeripoti kuwa Meneja wa Manchester United Sir Alex Ferguson anafikiria kumpiga shoka David De Gea na kusaka Kipa mpya katika kipindi hiki cha Dirisha la Uhamisho la Mwezi Januari.

Gazeti hilo limedai Sir Alex Ferguson amezidi kuvunjwa moyo na uchezaji wa Kipa De Gea ambae anashindwa kudhibiti eneo la Penati Boksi na mara nyingi huonekana mwenye mchecheto katika eneo hilo, hasa kwa mipira ya juu ya frikiki na kona, ambayo wapinzani wamechukulia hilo kama ni udhaifu wa Manchester United.

 The Mirror limedai kuwa Ferguson amemwomba Mkurugenzi Mtendaji, David Gill, pamoja na Wamiliki wa Klabu, Familia ya Glazers, kutoa Fedha ili kumnunua Kipa ambae ataruhusiwa kuichezea Man United kwenye Mashindano ya UEFA CHAMPIONZ LIGI Msimu huu.

Tangu atue Man United kutokea Atletico Madrid Mwaka 2011, De Gea amekuwa hana namba ya kudumu na mara nyingi amekuwa akibadilishana na Kipa mwingine, Anders Lindegaard, kutoka Denmark.

Ripoti za Gazeti hilo zimedai walengwa wa Sir Alex Ferguson ni Makipa wa Stoke City, Asmir Begovic, na yule wa Liverpool, Pepe Reina, kwani wote wataruhusiwa kuichezea Man United kwenye Mashindano ya UEFA CHAMPIONZ LIGI.

Hata hivyo, kumng’oa Begovic kutoka Stoke City itakuwa kazi kubwa kwani yeye ndie moja ya nguzo kubwa Klabuni hapo lakini duru hizo za habari zimekiri kumpata Reina ni rahisi kidogo maana inaonekana sasa Liverpool inatafuta mwelekeo mwingine kuhusu Kipa.

Andre Ayew out of Ghana squad

Meneja wa Ghana  Kwesi Appiah amethibitisha ya kwamba winga wa club toka ufaransa  Marseille  Andre Ayew hatoshiriki michuano ya African Nations Cup kwa mwaka huu 2013 huko Africa ya Kusini inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi lake tarehe 19 mwezi huu..

Ayew, 23,ameshindwa  kureport katika kambi ya timu ya taifa ya Ghana huko Abu Dhabi kutokana na kuwa majeruhi( hamstring injury), kwa maana hiyo hatokuwa katika kikosi cha wachezaji 23 kitakacho minyana huko kusini mwa Africa

Appiah said in a statement on Monday: "Unfortunately, Andre failed to report to camp and indicated that owing to the treatment he was receiving from his doctor he would report to camp on Wednesday.

kulingana na mwenendo mzima ulivyo sasa Appiah amesema kwa sasa ataendelea na wachezaji waliopo katika kambi yake,hata hivyo meneja huyo amesema Ayew atakuja kutumika siku za usoni akiwa Fit!!........

.Ayew ni mmoja ya wachezaji muhimu katika kikosi cha timu ya Taifa na mwaka 2011  alitajwa kama ndie mchezaji bora wa mwaka huo.



Wakala: Lampard lazima aondoke Chelsea.
 
Imethibitika kuwa Frank Lampard ataihama Chelsea mwishoni mwa msimu huu, kwa mujibu wa wakala wake Steve Kutner.
 
Akikaririwa na magazeti ya nchini Uingereza akisema,
"watendaji wa Chelsea walimwambia Frank kule Japan wakati wa michuano ya kombe la dunia la vilabu na hata mara baada ya ushindi dhidi ya Everton mwezi uliopita kuwa hakuna chochote kitakacho pelekea klabu kumpa ofa nyingine Lampard baada ya msimu huu"
 
"hakuna kitakacho badilika kwa vyovyote vile. Frank anapashwa kukubaliana na hayo inabidi ajikusanye kumalizia msimu kwa mafanikio katika klabu ambayo aliipenda sana."
 
Lampard alipata nguvu mpya kutokana na kushangiliwa na mashabiki wa Chelsea katika mchezo wa mzunguko wa tatu wa michuano ya FA dhidi ya Southampton jumamosi pale alipofunga goli ambalo kimsingi lilimfanya kuwa sawa na mchezaji wa zamani klabu hiyo Kerry Dixon mwenye rekodi ya juu ya ufungaji magoli, lakini inaonekana sherehe ya ushangiliaji baada ya kufunga goli akiwa katika jezi yake maarufu namba 8 mgongoni inaelekea ukingoni.
 
Mashabiki wa Chelsea wamekuwa wakitaka Lampard apewe mkataba mwingine lakini hali inavyo onekana ni kuwa hakuna nafasi nyingine ya kuendelea kusalia Stamford Bridge.
Mwenyewe Lampard amekaririwa akisema
"pengine sikuwa na mvuto wa kutosha lakini mashabiki wamekuwa na mimi katika kipindi chote ambacho tumekuwa pamoja hapa"