TRANSLATE THIS BLOG

Tuesday, April 7, 2015


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI - RELEASE NO. 51

TAREHE 07 APRILI 2015

U-15 YAINGIA KAMBINI


Timu ya Taifa ya Tanzania ya Vijana wenye umri chini ya miaka 15 (U-15) imeingia kambini leo katika hoteli ya Itumbi iliyopo magomeni chini ya kocha mkuu Adolf Rishard kujiandaa na progamu ya vijana kuwania kufuzu kwa fainali za U-17 mwaka 2017 nchini Madagascar.
Akiongea na waadishi wa habari leo kwenye ukumbi wa habari wa TFF Karume, mwenyekiti wa kamati ya soka la vijana Bw. Ayoub Nyenzi amesema kamati yake imeandaa programu maalumu ya kuwaanda vijana kwa ajili ya kuichezea timu ya Taifa U-17 mwaka 2017.

TFF imeandaa program hiyo ya vijana U-15 ambao watakua kambini kwa muda siku 10, wakifanya mazoezi uwanja wa Karume na kucheza michezo kadhaa ya kirafiki na timu za Azam U17 na shule ya Sekondari Makongo.

Kocha mkuu na timu yake ya U-15 atazunguka mikoa saba nchini kwa ajili ya kucheza michezo kadhaa ya kirafiki na kungamua vipaji vingine kwa ajili ya kuboresha timu yake. Mikoa itayotembelewa ni Mbeya, Mwanza, Morogoro, Arusha, Tanga, na Dar es alaam (Ilala, Kinondoni, Temeke).

Aidha katika kuhakikisha timu hiyo inakua tayari kwa michuano ya kuwania kufuzu kwa fainali za U-17 mwaka 2017 nchini Madagascar, timu hiyo ya vijana itafanya ziara ya mafunzo mwezi Disemba mwaka huu katika nchi za Malawi, Zambia, Zimbambwe, Botswana na Afrika Kusini kwa kucheza michezo ya kirafiki.

Mwezi Februari 2016 timu hiyo itacheza michezo miwili ya kirafiki na timu za mikoa ya Dodoma na Mwanza, kabla ya kuelekea tena katika ziara kwenye nchi za Burundi, Rwanda, Uganda na Kenya mwezi Aprili 2016.

Ratiba ya CAF kuwania kufuzu kwa fainalizaAfrika 2017 inatarajiwa kuanza mwezi Juni 2016, ambapo kikosi cha Tanzania kitakua kimeshapata muda mzuri wa maandalizi kwa lengo la kuhakikisha timu inashiriki fainali hizo nchini Madagascar 2017.

Fainali za U-17 mwaka 2017 zinatarajiwa kufanyika nchini Madagascar, huku Tanzania ikitarajia kwa kuwa mwenyeji wa fainali hizo za vijana U-17 kwa mwaka 2019.

Jumla ya wachezaji 30 wameitwa kuingia kambini, wachezaji hao ni Kelvin Deogratius, Magazi Dotto, Anthon Shilole (Geita), Sadik Sud Ramadhani , Mwinchumu Yahya(Tanga),Faraji John, David Mbakazi , Juma Juma, Pius Raphael, Davison Meddy, Maulid Lembe (Dodoma), Ibrahim Koba (Morogoro).

Wengine ni Abubakar Badru Nassoro, Yusuf B.A. Khalfani, All Hafidh Mohamed (Kusini Pemba), Joachim Mwenda, Charles Cassiano, Luqman Shauri (Tanga), Juma Zuberi (Kigoma), Ismail Abdallah (Kusini Pemba), Robert Philipo (Arusha), Alex Peter, Mohamed Ally, Rashid Kilongola (Kinondoni), Saad Juma (Mkoa Magharibi), Ibrahim Shamba (Kusini Unguja), Ally Msengi, Klevin S.Kijili (Mwanza), Frank Abel (Simiyu) na Bryan Jamal.

VPL KUENDELEA KESHO


Ligi kuu ya Vodacom Tanzania inatarajiwa kuendelea kesho jumatano katika viwanja viwili jijini Dar es salaam, kwa vinara wa ligi hiyo Young Africans kuwakaribisha Coastal Union kwenye dimba la Uwanja wa Taifa.

Uwanja wa Chamazi Complex, wenyeji timu ya Azam FC wanaokamata nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu, watawakaribsiha wagonga nyundo kutoka jijini Mbeya timu ya Mbeya City FC.

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
Natasha Jonas retires: British Olympic boxer quits aged 30

 Natasha Jonas, the first woman to box for Great Britain at the Olympic Games, has retired 16 months before Rio 2016.

The Liverpudlian won bronze at the 2012 World Championships before reaching the quarter-finals at the London Olympics.

The 30-year-old, who hopes to move into coaching, told BBC Sport: "I don't think I've got the hunger and dedication to achieve any more.

"My mind is wandering to other things, and there's younger people coming through that want it a bit more."

Jonas took up boxing in 2005 to lose weight and rose through the amateur ranks before competing for Britain alongside gold medallist Nicola Adams and Savannah Marshall at London 2012.

Who is Natasha Jonas?

Date of birth: 18 June 1984
Height: 1.72m (5ft 7in)

Birthplace: Liverpool
Olympic division: Lightweight

Did you know? Jonas had to drop down two weight divisions (8kg) for the Olympics as there is no welterweight category.

Sunday, October 26, 2014

Robert Pires: kukosa mechi mbili za ligi

kiungo wa zamani wa  Arsenal Robert Pires amefungiwa kutocheza michezo miwili ya Indian Super League after an alleged altercation with an opposing coach.
Pires miaka 40, kwa sasa anachezea  FC Goa,awali alisema alipigwa na kocha wa Atletico de Kolkata  Antonio Lopez Habas wakati timu zinakwenda mapumziko katika mechi ya Alhamis ya wiki iliyopita.
                                                          pires enzi akiwa Arsenal na mzee wenga
Habas amefungiwa mechi nne na shirikisho la soka huko india( All India Football Federation (AIFF), na wawili hao kupigwa faini kila mmoja ya 500,000 (£5,085).
Pires na Habas wamepewa siku nne kuwasilisha pingamizi zao(kukata rufaa).

Nigeria washinda taji la akina dada


Nigeria iliicharaza Cameroon na kushinda kombe taifa bingwa barani Afrika miongoni mwa akina dada mjini Windhoek namibia.

Baada ya kufanya mashambulizi kadhaa mwanzoni mwa mechi hiyo,Desire Oparanozie aliipatia Super Falcon bao lao la kwanza katika dakika ya 12 baada ya kupiga mkwaju wa nidhamu. Asisat Oshoala baadaye aliifungia Nigeria bao lao la Pili dakika mbili kabla ya kukamili kwa kipindi cha pili na kufanya mambo kuwa mbili kwa sufuri.
Nigeria imeshindwa kushinda taji hilo mara mbili Pekee tangu mashindano hayo yalipoanzishwa mwaka 1991.

Equitorial Gunea ndio washindi wengine wa Kombe hilo mnamo mwaka 2008 na 2012,lakini walishindwa kufuzu katika michuano ya mwaka huu.
Mkufunzi wa cameroon Enoh Ngatchu amesema kuwa kufuzu kushiriki katika dimbala dunia kwa upande wa akina dada kwa mara ya kwanza huenda ukaimarisha mchezo huo miongoni mwa akina dada nchini mwake.
Nigeria na Cameroon tayari walikuwa wamefuzu kushiriki katika kombe la dunia mwaka ujao nchini canada baada ya kufuzu katika fainaliza kombe hilo la Afrika
MAMBO YA JANA..LIGI KUU UINGEREZA..
Song na mambo ya chizungu

                   MOYES MBIONI KUTUA INTER MILAN

KOCHA David Moyes yumo kwenye orodha fupi ya mwisho ya makocha wanaotakiwa na Inter Milan ya Italia inayotaka kumtimua kocha wake wa sasa, Walter Mazzarri.
Kocha huyo wa zamani wa Manchester United na Everton anapewa nafasi kubwa ya kurithi mikoba ya Mazzarri, ambaye timu yake inacheza na Cesena leo akiwa katika shinikizo baada ya mwanzo mbaya unaoifanya Inter iwe katika nafasi ya tisa kwenye msiamo wa ligi hivi sasa.

                                     David Moyes yuko kwenye dada za Inter Milan
Moyes mwenyewe amekua akiamini akipata nafasi ya kufundisha klabu nje ya Uingereza itakuwa ni fursa nzuri kwake kurejesha heshima yake- hivyo akifanikiwa mpango huo atakuwa ametimiza ndoto zake kwa sasa.

Sunday, January 26, 2014

NIMESHAIVA VYA KUTOSHA KWA NAFASI YA KOCHA MKUU.


NGULI wa soka wa zamani wa Ufaransa, Zinedine Zidane amesema yuko tayari kuwa kocha mkuu baada ya kufanya kazi kama kocha msaidizi wa Carlo Ancelotti katika klabu ya Real Madrid.

 Zidane ambaye aliteuliwa kuwa mkurugenzi wa michezo wa Madrid mwaka 2011, amechagua kuwa msaidizi wa Ancelotti baada ya Muitaliano huyo kutua klabu hapo kuziba pengo la Jose Mourinho aliyetimuliwa katika kipindi cha kiangazi. Kufuatia kupita miezi sita ya kwanza akiwa chiini ya Ancelotti, Zidane amesisitiza kuwa sasa anadhani yuko tayari kujaribu nafasi yake kama kocha mkuu na kuahidi kukitengeneza kikosi chake kuwa chenye kufanya mashambulizi.

 Zidane amesema ana hamu kubwa ya kupewa nafasi kamili ya ukocha kwasababu anajiona ana mambo mengi yanayoweza kunufaisha timu yoyote itakayomuhitaji.

 Zidane ambaye ameshinda mataji manane akiwa mchezaji wa Madrid, pia aliwashukuru Ancelotti na rais wa klabu hiyo Florentino Perez kwa kumsaidia katika kipindi chote ambacho amekuwa hapo.