TRANSLATE THIS BLOG

Sunday, October 26, 2014

Robert Pires: kukosa mechi mbili za ligi

kiungo wa zamani wa  Arsenal Robert Pires amefungiwa kutocheza michezo miwili ya Indian Super League after an alleged altercation with an opposing coach.
Pires miaka 40, kwa sasa anachezea  FC Goa,awali alisema alipigwa na kocha wa Atletico de Kolkata  Antonio Lopez Habas wakati timu zinakwenda mapumziko katika mechi ya Alhamis ya wiki iliyopita.
                                                          pires enzi akiwa Arsenal na mzee wenga
Habas amefungiwa mechi nne na shirikisho la soka huko india( All India Football Federation (AIFF), na wawili hao kupigwa faini kila mmoja ya 500,000 (£5,085).
Pires na Habas wamepewa siku nne kuwasilisha pingamizi zao(kukata rufaa).

Nigeria washinda taji la akina dada


Nigeria iliicharaza Cameroon na kushinda kombe taifa bingwa barani Afrika miongoni mwa akina dada mjini Windhoek namibia.

Baada ya kufanya mashambulizi kadhaa mwanzoni mwa mechi hiyo,Desire Oparanozie aliipatia Super Falcon bao lao la kwanza katika dakika ya 12 baada ya kupiga mkwaju wa nidhamu. Asisat Oshoala baadaye aliifungia Nigeria bao lao la Pili dakika mbili kabla ya kukamili kwa kipindi cha pili na kufanya mambo kuwa mbili kwa sufuri.
Nigeria imeshindwa kushinda taji hilo mara mbili Pekee tangu mashindano hayo yalipoanzishwa mwaka 1991.

Equitorial Gunea ndio washindi wengine wa Kombe hilo mnamo mwaka 2008 na 2012,lakini walishindwa kufuzu katika michuano ya mwaka huu.
Mkufunzi wa cameroon Enoh Ngatchu amesema kuwa kufuzu kushiriki katika dimbala dunia kwa upande wa akina dada kwa mara ya kwanza huenda ukaimarisha mchezo huo miongoni mwa akina dada nchini mwake.
Nigeria na Cameroon tayari walikuwa wamefuzu kushiriki katika kombe la dunia mwaka ujao nchini canada baada ya kufuzu katika fainaliza kombe hilo la Afrika
MAMBO YA JANA..LIGI KUU UINGEREZA..
Song na mambo ya chizungu

                   MOYES MBIONI KUTUA INTER MILAN

KOCHA David Moyes yumo kwenye orodha fupi ya mwisho ya makocha wanaotakiwa na Inter Milan ya Italia inayotaka kumtimua kocha wake wa sasa, Walter Mazzarri.
Kocha huyo wa zamani wa Manchester United na Everton anapewa nafasi kubwa ya kurithi mikoba ya Mazzarri, ambaye timu yake inacheza na Cesena leo akiwa katika shinikizo baada ya mwanzo mbaya unaoifanya Inter iwe katika nafasi ya tisa kwenye msiamo wa ligi hivi sasa.

                                     David Moyes yuko kwenye dada za Inter Milan
Moyes mwenyewe amekua akiamini akipata nafasi ya kufundisha klabu nje ya Uingereza itakuwa ni fursa nzuri kwake kurejesha heshima yake- hivyo akifanikiwa mpango huo atakuwa ametimiza ndoto zake kwa sasa.