TRANSLATE THIS BLOG

Saturday, August 3, 2013

NASSIBU RAMADHANI AMTAMBIA JUMA FUNDI

BONDIA Nassibu Ramadhani amejigamba kuwa atamchakaza mpinzani wake Juma Fundi wakati wa mpambano wao utakaopigwa siku ya Idi pili katika ukumbi wa friends corner Manzese

Aliongeza kwa kusema unajua mimi anaeniumiza kichwa kwa sasa ni Fransic Miyeyusho pekee kwa Tanzania hii kwa kuwa nilicheza nae na nikashindwa kummudu ata hivyo ipo siku nitaomba mpambano mwingine wa marudiano nae hivyo nimemuweka kiporo

Bondia huyo aliendelea kujinasibu kwa kusema kwa sasa mimi ni nambari One hivyo fundi ategemee kipigo cha mbwa mwizi kwa ni ato furukuta
Naomba mashabiki wangu wa ngumi mjitokeze kuja kunishangilia ata kama wewe sio shabiki wango njoo uone ngumi nitakazokuwa nikicheza na utamini kuwa mimi ni kiboko yao

Ramadhani ambaye ucheza kwa kasi kubwa sana awapo ulingoni amekuwa kivutio kikubwa kwa mashabiki na kumpachika jina la Mann Paquaio wa Philipins kwa kuwa wote wanatanguliza mguu wa kulia mbele 

Siku hiyo kutakuwa na uhuzwaji wa DVD mpya kwa ajili ya mafunzo ya mchezo wa masumbwi zatakazokuwa zikisabazwa na kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D'

pia siku hiyo kutakuwa na mapambano mengine ya utangulizi wakisindikiza mpambano huo
HABARI HII NI MALI YA http://burudan.blogspot.com/

Wednesday, July 24, 2013

Sevilla wamsajili Gameiro wa PSG

Timu ya Sevilla imefanikiwa kumsajili striker Kevin Gameiro kutoka mabingwa wa ufaransa msimu uliopita Paris Saint-Germain,klabu hiyo toka hispania imethibitisha hayo leo jumatano.
kwa mujibu wa vyombo vya habari ,Sevilla watalipa kiasi cha yuro euro 10mil ambazo nisawa na  (13.2 million dollars) kwaajili ya saini ya mchezaji huyo mwenye miaka 26.

Sevilla,ambao msimu uliokwisha walimaliza ligi spain LA LIGA wakiwa nafasi ya tisa,wanatizamia sasa kukiimarisha kikosi chao hasa safu ya mbele tangu kufuatiwa kuuzwa kwa strikers wao Alvaro Negredo na Jesus Navas kwa vijana wa ligi kuu uingereza  Manchester City.

Klabu ya Sevilla imetangaza kuwa wamemtoa kwa mkopo beki wao Alberto Botia kwa timu ya  Elche ili       kupata nafasi ya kucheza zaidi.

HAYATOU AMTEUA JORDAAN KUWA MSHAURI WAKE.

OFISA mkuu wa zamani wa kamati ya maandalizi ya michuano ya Kombe la Dunia 2010, Dr Daniel Alexander "Danny" Jordaan (born 3 September 1951) ambae ni mwafrika  kusini   ameteuliwa kuwa mshauri wa rais wa Shirikisho la Soka barani Afrika-CAF Issa Hayatou.

 Katika taarifa iliyotumwa katika mtandao wa CAF imeeleza kuwa uteuzi wa Jordaan umekuja kufuatia mchango wake anaoendelea kutoka katika kunyanyua soka la Afrika. huku Hayatou akiongeza kuwa anategemea mafanikio makubwa kwa kushirikiana vyema na Jordaan.

MARADONA AFANYIWA UPASUAJI WA MACHO.

NGULI wa soka nchini Argentina, Diego Maradona amefanyiwa upasuaji wa macho ambao umemalizika kwa mafanikio.

 Maradona mwenye umri wa miaka 52 alifanyiwa upasuaji huo ili kukwangua utandu uliokuwa katika macho yake ambao ulikuwa ukisumbua kutokuona sawasawa katika mji wa Mendoza uliopomagharibi mwa Argentina.

Daktari aliyemfanyia upasuaji Roberto Zaldivar aliwaambia waandishi wa habari kuwa Maradona alikuwa akiendelea vyema na upasuaji huo ni wa kawaida kwa watu wenye umri kama wake.

Maradona anatarajiwa kufanyiwa uchunguzi kabla ya kurejea Buenos Aires na baadae kwenda Dubai ambako anafanya kazi kama balozi wa soka.

HIGUAIN KWENDA NAPOLI...arsenal hoi!!!


MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Argentina na klabu ya Real Madrid, Gonzalo Higuain inasemekana amekamilisha usajili wake kwenda Napoli ya Italia kwa mujibu ya magazeti ya nchini Hispania.

 Gazeti la AS na Marca ya nchi hiyo lilidai kuwa Napoli wamelipa kiasi cha euro 37(Ambazo ni sawa na dollar za kimarekani 48.8mil) kwa ajili saini ya nyota huyo mwenye umri wa miaka 25.

 Kama mpango huo ukikamilika Higuain atakuwa mchezaji wa tatu wa Madrid kuuzwa Napoli katika kipindi hiki cha uasajili majira ya kiangazi baada ya Raul Albiol na Jose Callejon kuwa tayari wameuzwa.

Kumbuka Napoli kwa sasa inaongozwa na Mhispania Rafa Benitez.

 Kwa mujibu wa taarifa za gazeti hilo pesa zitakazopatikana kwa mauzo ya Higuain zitatumika katika kutafuta saini za Gareth Bale wa tottenham na Luis Suarez wa Liverpool...

Kwa msisitizo!!!!!!!!...
According to media reports, Real will use the money for Higuain to bid for Gareth Bale of Tottenham and Luis Suarez of Liverpool.

SIJUTII KUINUNUA QPR - FERNANDES.

MMILIKI wa klabu ya Queens Park Rangers, QPR, Tony Fernandes amesema hajutii kuinunua klabu hiyo pamoja na kushuka daraja na kudai kuwa ana mategemeo ya kuigeuza na kuwa klabu yenye mafanikio.

 Fernandes ambaye alitenga mamilioni ya paundi kwa ajili ya kuibakisha klabu hiyo ligi kuu amesema hana mpango wa kumiliki klabu kubwa kama Liverpool au Arsenal kwani kwa kufanya hivyo ni sawa na kununua mafanikio ya wengine.

 Bilionea huyo wa Malaysia ameamua kuchagua QPR ili aweze kuipa mafanikio kama zilivyo klabu nyingine kubwa nchini Uingereza na ana mategemeo ya kurejea tena ligi kuu katika kipindi cha muda mfupi ujao.
 Fernandes ambaye pia anamiliki timu ya Caterham ya langalanga amesema alikuwa akijua kuwa kulikuwa na uwezekano mkubwa wa kushuka daraja wakati alipoinunua klabu hiyo mwaka 2011.

Monday, July 22, 2013

Scotland teyari kuivaa Uingereza

 
 Meneja wa timu ya taifa ya Scotland GORDON STRACHAN ametangaza kikosi kazi tayari kuivaa three lion(Timu ya taifa ya Uingereza) katika mechi ya kimataifa ya kirafiki itakayopigwa Wembley tarehe14 August ikiwa ni maandalizi  ya mechi yao ya  kuwania kufuzu  World Cup nyumbani dhidi ya  Belgium mwezi September. 

katika ushindi waliopata Scotland dhidi ya Croatia katika kuwania kufuzu fainali hizo mwezi june wameshuka katika viwango vya ubora wa soka kutoka nafasi ya 24 mpka nafasi ya50

Scotland squad:
Goalkeepers: Matt Gilks (Blackpool) David Marshall (Cardiff City) Allan McGregor (Hull City)
Defenders: Gordon Greer (Brighton and Hove Albion) Steven Hammell (Motherwell) Grant Hanley (Blackburn Rovers) Alan Hutton (Aston Villa) Russell Martin (Norwich City) Charlie Mulgrew (Celtic) Andy Webster (Unattached) Steven Whittaker (Norwich City) 

Evan Kangwa aitwa Zambia

Mshambuliaji wa Nkana Evans Kangwa ameitwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Zambia Chipolopolo katika maandalizi ya kufuzu 2014 African Nations Championship (CHAN) raundi ya kwanza dhidi (The Zebras)’of Botswana.

The Nkana striker ni mmoja kati ya wachezaji wawili wapya walioitwa na kocha mkuu wa Zambia Herve Renard has named to his 2013 Cosafa Cup winning team ahead of Saturday’s CHAN first round away leg game against Botswana to be played in Molepolole.

Kangwa returns to the fold for the first time since December 21, 2012 when he came on as a substitute in Zambia’s 1-0 away friendly loss to Tanzania. He also makes the team despite not playing any competitive action this year after he was hold-up in Spain on trials for the last six months.

Kangwa’s call-up swells Nkana’s contingent in the Zambia team to four joining striker Festus Mbewe plus defenders Masauso Zimba and Christopher Munthali. Also getting a recall is Zanaco defender Salulani Phiri who joins club mates Fackson Kapumbu and striker Moses Phiri.

Meanwhile, Zambia enters camp on July 22 in Lusaka to begin preparations for their CHAN qualifier this Saturday prior to departure for Gaborone on July 25.

The two sides will face each other in the return leg on August 3 with the winner advancing to the final second round qualifier to play either Zimbabwe or Mauritius for a place in next January’s CHAN finals in South Africa.

FROOME BINGWA WA MICHUANO YA TOURE DE FRANCE.

MSHINDANO ya baiskeli yajulikanayo kama Tour de France yamefikia tamati jana kwa Chris Froome wa Uingereza kutawadhwa bingwa mpya wa mashindano ambayo ni ya 100 toka kuanzishwa kwake.

 Akishinda taji hilo kwa zaidi ya dakika nne, Froome alishikana mikono na na wenzake wa timu ya Sky wakati akikatisha katika msitari wa ushindi jijini Paris, Ufaransa.

 Huo unakuwa ushindi wa pili kwa Uingereza kwenye michuano hiyo baada ya mwendesha baiskeli Sir Bradley Wiggins ambaye naye anatoka katika timu ya Sky kushinda michuano hiyo mwaka jana. Mashindano yalishirikisha waendesha baiskeli kutoka nchi mbalimbali ambapo waliendesha baiskeli kwa kilometa 3,200 katika miji mbalimbali ya ya Ufaransa katika kipindi cha wiki mbili cha mashindano hayo.

Taifa Stars kwenda Kampala Jumatano


Timu ya Taifa ya Tanzania itaondoka Mwanza Jumatano kwenda Kampala, Uganda kwa ajili ya mechi ya marudiano ya Kombe la CHAN itakayochezwa Jumamosi katika Uwanja wa Mandela kuanzia saa kumi kamili jioni. 

Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager iko kambini jijini Mwanza chini ya Kocha Kim Poulsen tangu Julai 14 mwaka huu kujiandaa kwa mechi hiyo itakayoamua ni timu ipi kati ya hizo mbili itacheza Fainali za CHAN zitakazofanyika mwakani nchini Afrika Kusini.
Timu hiyo itaondoka Uwanja wa Ndege wa Mwanza saa 7.25 mchana kwa ndege ya PrecisionAir, na inatarajiwa kutua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Entebbe saa 10.15 jioni.
Wakati huo huo, Kocha Kim Poulsen atakuwa na mkutano na waandishi wa habari kuzungumzia maandalizi ya kikosi chake Jumanne.

United ofa nyingine kwa Cesc


Manchester United manager David Moyes jumatatu ya leo amefunguka na kusema kwamba,mabingwa hao wa ligi kuu ya soka uingereza  had made a second offer kwa kiungo wa Barcelona Cesc Fabregas.
Awali United iliripotiwa kuwa  walimtengea mhispania huyo dau la £25 million,ambalo lilikataliwa kwaajili wa nahodha huyo wa zamani wa  Arsenal .
Moyes said United made a second bid and were working hard to bring the Spanish international back to England.

Moyes akizungumza mbele ya  press conference katika ziara ya United huko Japan amesema kwamba  Ed Woodward, mwenyekiti wa klabu, had received a response from Barcelona
Hata hivyo moyes amesema kwamba Woodward amejaribu  kufanya usajiliwa kwa baadhi ya wachezaji wapya kabla ya kuanza kwa msimu...

Ligi kuu ya Vodacom 2013/2014 kuanza Agosti 24



Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara msimu wa 2013/2014 itaanza kutimua vumbi Agosti 24 mwaka huu huku timu zote 14 zitakuwa viwanjani katika miji saba tofauti.
Hata hivyo, kabla ya ligi hiyo kuanza kutakuwa na mechi ya kufungua msimu (Ngao ya Jamii- Community Shield) kati ya bingwa mtetezi Yanga na Makamu bingwa Azam itakayochezwa Agosti 17 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. 

Mechi za VPL za Agosti 14 mwaka huu zitakuwa kati ya Yanga na Ashanti United (Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam), Mtibwa Sugar na Azam (Uwanja wa Manungu, Morogoro), na JKT Oljoro na Coastal Union (Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Kaluta Amri Abeid, Arusha).
Nyingine ni Mgambo Shooting na JKT Ruvu (Uwanja wa Mkwakwani, Tanga), Rhino Rangers na Simba (Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora), Mbeya City na Kagera Sugar (Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine, Mbeya), na Ruvu Shooting na Tanzania Prisons (Uwanja wa Mabatini, Mlandizi, Pwani).
Mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo utamalizika Novemba 3 mwaka huu wakati wa pili utamalizika Aprili 27 mwakani.

Thursday, March 14, 2013

BRAZIL YAPUMULIA MASHINE VIWANGO VYA UBORA WA SOKA,MALI YAIPUMULIA
MBAVUNI(Fifa rankings)
 
Mabingwa wa kihistoria wa dunia mara tano(5) wameendelea kuburuzwa na
kuporomoka katika ubora wa soka duniani na hii ni kwa mujibu wa
viwango vya ubora wa kutandaza soka duniani vilivyotolewa leo
alhamisi na shirikisho la soka duniani FIFA,ikiwa chini ya Ecuador,
Switzerland na Greece and kupishana na Mali toka Africa kwa nafasi
sita bingwa huyo kufikiwa.
 
Brazili ndio wenyeji wa fainali zijazo za kombe la dunia zitakazo
fanyika 2014,kwa sasa katika msimamo wa ubora wa soka inakamata
nafasi ya 18 wakati Mali ambao hawajawahi kucheza  World
Cup,wanakamata nafasi ya 24 baada ya kupanda nafasi moja zaidi.
 
Timu zote kumi(10)kutoka Aamerika ya kusini bado zimesalia katika 50
bora,na timu ya mwisho kutoka barani humo ni Venezuela iliyoshika
nafasi ya 43.
 
Brazil are not involved in the World Cup qualifiers and have
plummeted down the rankings as friendlies earn fewer points than
competitive games in the completed rankings calculations.
Afghanistan, languishing near the foot of the table until last month,
leapt 48 places thanks to wins over Laos and Sri Lanka, leaving them
141st out of 209 teams.
 
Japan ndio timu iliyokuwa juu kuliko zote toka barani Asia katika
viwango hivi vilivyotolewa leo vya ubora wasoka duniani na fifa baada
ya kukamata nafasi ya  26,kutoka Afrika Ivory Coast wameendelea 
kufanya vizuri kwa kukamata nafasi ya 13na ndio vinara kutoka
Afrika,Mexico yenyewe inakamata nafasi ya 15 na kuwa juu kwa ukanda
wa CONCACAF.
 
Hakuna mabadiliko kwa viongozi,mabingwa Dunia na ulaya Spain
wameendelea kushika usukani ikifuatiwa na Germany, Argentina, England
na Italy.
KUMI BORA
1.Spain
2.Germany
3.Argentina
4.England
5.Italy
6.Colombia
7.Portugal
8.Netherlands
9.Croatia
10.Russia
11.Ecuador
12.Greece
13.Côte d'Ivoire
14.Switzerland
15.Mexico
16.Uruguay
17.France
18.Brazil
19.Belgium
20.Ghan
Mabingwa wa Afrika kwa mwaka huu Nigeria wamekamata nafasi ya 30
Nigeria,kutoka Afrika Mashariki Uganda imeendele kufanya vyema katika
ukanda huu kwa kushika nafasi ya 85 ikifuatiwa na Tanzania na Kenya
wakikamata 126.

Monday, February 25, 2013

  YANGA WAINGIA KAMBINI KATIKATI YA JIJI

 
Baada ya kuichapa timua ya Azam FC kwa bao 1-0 mwishoni mwa wiki, timu ya Young Africans Sports Club leo imeingia kambini katika Hoteli ya Tansoma katikati ya jiji kujiaandaa na mechi inayofuata dhidi ya timu ya Kagera Sugar, mchezo utakaofanyika siku ya jumatano katika dimba la Uwanja wa Taifa kuanzia majira ya saa 10 jioni.
Young Africans ambayo iliwapa furaha washabiki, wapenzi wa soka na wanachama wake kwa soka safi la ufundi wa hali ya juu, itashuka dimbani kuwakabili wakata miwa hao ambao katika mchezo wa awal waliibuka na ushindi wa bao 1-0 mchezo uliofanyika katika dimba la Kaitaba mjini Bukoba.
                                                       kikosi cha Dar Youn African
Young Africans yenye jumla ya point 39 na mabao 34 ya kufunga na mabao 12 ya kufungwa itashuka dimba la uwanja wa Taifa kuhakikisha inaibuka na ushindi katika mchezo huo ili kuendelea kuongoza  msimamo wa Ligi Kuu ya VPL na hatimaye iweze kutwaa Ubingwa huo.
Mara baada ya mazoezi ya leo asubuhi, kocha mkuu Brandts amesema anashukuru vijana wake kwa kufanya kile alichowaagiza, nidhamu ya hali ya juu na kushika maelekezo yake ndio vitu vilivyopelekea kuendelea kuibuka na ushindi katika michezo mbali mbali waliyocheza.
Nawapongeza washabiki, wanachama na wapenzi wa Yanga waliojitokeza kwa wingi siku ya jumamosi, kuja kuwashangilia vijana, kikubwa nawaomba waendelee na moyo huo huou kwani waliwapa nguvu vijana na kuwafanya wacheze kwa kujiamini mda wote wa mchezo 'alisema Brandts'.
Aidha Brandts alisema matokeo ya juzi yameendelea kuiweka Yanga katika nafasi nzuri ya kuelekea kutwaa Ubingwa na atahakikisha wanajitahidi kushinda kila mchezo ili kujiweka katika mazingia mazuri ya kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom.
Kikosi cha  wachezaji 26 na benchi la ufundi wote wameingia kambini katika Hoteli ya Tansoma mara baada ya mazoezi ya leo asubuhi na wachezaji wote ni wazima kiafya na kiakili hivyo hakuna mcheaji hata mmoja ambaye ni majeruhi.
CHANZO:www.youngafricans.co.tz/&Dinna  ismail

WAZIRI WA HABARI UTAMADUNI NA MICHEZO FENELLA MUKANGARA.

 
 Waziri wa habari vijana utamaduni na michezo Fenella Mukangara amefuta matumizi ya katiba mpya ya TFF ya mwaka 2012 kwa vile imekiuka kanuni na sheria za BMT hivyo TFF wanatakiwa kutukia katiba ya mwaka 2006 ambayo imetumika katika mikoa kufanyia uchaguzi.

 Mukangara amesema TFF inatakiwa kufuata kanuni nasheria za BMT ambazo ambazo ndizo zenye maelekezo ya kufanya marekebisho ya katiba .

 Hakuna chama chochote hapa nchini kilicho juu ya BMT yaani baraza la michezo nchini ,hivyo TFF wanatakiwa kufanya mkutano mkuu kwa kutumia katiba ya mwaka 2006 na FIFA wanatakiwa kuelezwa mambo yalivyo pindi watakapokuwa hapa.

 Pia waziri amesema anamuondoa kazi msajili aliyepitisha katiba ya TFF kwani hajafuata kanunu na sheria na kumuweka mwingi pamoja na kuhamisha ofisi ya msajili

   KUELEKEA DABY YA  LONDON KASKAZIN

Beki wa washika bunduki wa london Arsenal Per Mertesacker amesema kiungo wa timu hiyo says Santi Cazorla ni mtandaza soka hasa na hii ni baada ya muhispania huyo kutupia nyavuni mara mbili katika ushindi walioupata jumamosi iliyopita wa magoli 2-1 dhidi ya Aston Villa.

 

Cazorla alikuwa katika kiwango chake kwa mara nyingine tena na jumamosi hii Gunners watakuwa ugenini katika dimba la White Hart Lane kuwakabili wenyeji wao spurs katika ile derby ya london ya kaskazin na Mertesacker anamatumaini na kiungo wake huyo kuendelea kufanya vizuri..
------------------------

WILSHARE;BADO TUNAWEZA

Tukiendelea kusalia London kunako vijana wa ARSHBATON,Kiungo  Jack Wilshere amewataka wechezaji wenzake kuendelea kufanya vyema na kuhakikisha hawashuki kiwango kwani msimu bado haujafika mwisho wanayo nafasi ya kufanya vyema na kuwapiku wapinzani wao katika ligi na hata kukamata nafasi mbili za juu....

Katika upande wa klabu bingwa barani ulaya,Arsenal inaonekana kuwa na nafasi finyu ya kusonga mbele  baada ya kukubali kichapo cha goli 3-1 toka kwa Bayern Munich katika uwanja wa nyumbani na mwezi ujao Arsenal itasafiri mpaka Munich katika dimba la Arena kuikabili Bayern.
-------------------------------------------------
BALE;SPURS ZAIDI

Wakati huo huo kutoka london ya kaskazini,Gareth Bale anaamini kwa sasa Tottenham iko vizuri (ni bora) zaidi ya  Arsenal katika kuwania nafasi nne za juu ambazo zinakuwezesha kucheza Champions League.

HABARI FUPI FUPI NA HARAKATI ZA USAJILI

Klabu ya Newcastle inamtaka winga mfaransa Hatem Ben Arfa kusaini mkataba mpya na kuendelea kusalia St James' Park,na hii ni baada ya Liverpool kuanza kumtolea macho kijana huyo mwenye miaka 25.

---------------------------------
Meneja wa majogoo wa jiji Liverpool Brendan Rodgers alifunga safari mpaka Holland kumshuhudia nahodha wa Feyenoord anaecheza beki ya kati Stefan De Vrij(21 yrs),katika mchezo wa ligi ya uholanzi iliyopigwa jumapili ambapo Feyenoord iliibuka na ushindi wa 2-1 mbele ya PSV Eindhoven. Rodgers amekuwa akisaka beki kwaajili kuziba nafasi ya Jamie Carragher ambae amestaafu soka.
----------------------------------
Kiungo wa Southampton Gaston Ramirez, 22yrs,anawindwa na vilabu vinavyoshiriki ligi kuu ya Italia seria A,vinara Juventus,Inter Milan na Fiorentina.
----------------------------------
Boss wa West Ham Sam Allardyce huwenda akamuongeza katika kikosi chake beki wa zamani wa Bolton Ricardo Gardner.mchezaji huyo wa kimataifa toka Jamaica ,34yrs,kwa sasa ni mchezaji huru baada ya kuondoka Reebok Stadium akiwa mchezaji huru msimu uliopita.
-----------------------------------
Mshambuliaji wa mashetani wekundu Manchester United Robin van Persie atakuwa fit kuikabili Real Madrid wiki ijayo katika klabu bingwa barani ulaya baada ya kuumia katika mchezo dhidi ya Queens Park Rangers.

 

lakini taarifa iliyopo nikwamba Van Persie ataukosa mchezo wa jumamosi katika dimba la nyumbani Old Trafford watakapo wakaribisha nyumbani Norwich City.
-----------------------------------
Meneja wa Celtic Neil Lennon ameitaka klabu yake kumpatia kandarasi mpya kiungo wa timu hiyo mwenye umri wa miaka 26 Joe Ledley.
------------------------------------
AND FINALLY

Klabu toka Italia Palermo imemfukuza kazi manager wao Alberto Malesani baada ya wiki tatu tu katika kazi yake,nafasi yake amepewa Gian Piero Gasperini - the man Malesani replaced.

 Full story: La Gazzetta dello Sport 

Mario Balotelli: AENDELEA KUBAGULIWA ITALIA

Italian media reports suggest AC Milan's Mario Balotelli was the target of racial abuse from fans of ex-club Inter Milan in Sunday's derby.

Balotelli, 22,alishachezea Inter kabla ya kusaini Manchester City na mwezi wa kwanza mwaka huu 2013 katika dirisha la usajili alihamia AC Milan.

Gazeti linaloandika habari za michezo Italia,Gazzetta dello Sport  ni moja ya chombo cha habari kilichoripoti ubaguzi huo kwa kutupiwa ndizi na mashabiki wa Inter katika mchezo uliopigwa jumapili na kulazimishana sare ya1-1 katika dimba la San Siro.

 

Balotelli also put his finger to his lips in an apparently defiant gesture.

Chama cha soka inchini Italia kimesema kamati ya nidhamu ya Serie A(Serie A disciplinary council) itakuwa na mkutano huko Milan kesho jumanne.....

Mapema mwezi huu,Inter walipigwa faini ya 15,000 yuro(sawa na paund 12,900) baada ya kuwa na vitendo vya kibaguzi kwa baadhi ya mashabiki juu ya Balotelli katika mchezo dhidi Chievo.

Makamo wa raisi wa AC Milan Paolo Berlusconi,kaka wa raisi wa klabu ya San Siro Silvio,nae alitumia lugha ya kibaguzi wakati akimuelezea  Balotelli.

ARSENE WENGER ;ARSENAL INAWEZA KUMALIZA NAFASI YA PILI KATIKA LEAGUE

Meneja wa washika bunduki wa london Arsenal,mzee Arsene Wenger amesema vijana wake wanaweza kukamata nafasi ya pili katika ligi kuu ya soka inchini uingereza na nijambo linalowezekana kwa Gunners...

Siku chache zilizopita Wenger ameishuhudia Arsenal ikibwagwa nje ya michuano ya FA baada ya kupata kichapo cha bao 1-0 toka kwa vijana wanaoshiriki ligi daraja la kwanza Blackburn na kufuatia kipigo katika dimba la nyumbani Emarete toka kwa  Bayern Munich katika hatua ya 16 bora ya klabu bingwa barani ulaya.

MBIO ZA KUWANIA NAFASI YA PILI!!!!!


Licha ya kuwa nyuma kwa poiti 9 mbele ya timu ya Manchester City ambao mpaka sasa wanaendelea kukamata nafasi ya pili katika ligi na ikiwa imesalia michezo 11 kumalizika kwa msimu bado mzee wa kifaransa anamatumaini ya kuleta ushindani katika nafasi hiyo.

"Man City is not out of reach. It could be a tight fight until the end," said the Arsenal boss.

wiki iliyopita Arsenal walipata ushindi wao wa tatu mfululizo katika ligi baada ya ushindi wa jumamosi 2-1 dhidi ya Aston Villa ikiwa ni muendelezo toka kwa Sunderland na Stoke.

Bado Arsenal inaendelea kukamata nafasi ya tano katika msimamo wa ligi kuu soka inchini uingereza wakiwa nyuma ya City, Chelsea na Tottenham ambao siku ya jumapili ya tareh 3 kutakuwa na north London derby katika dimba la White Hart Lane watakapokutana nao.

Manchester United, who Arsenal still have to play at Emirates Stadium on 28 April, are 21 points clear of the Gunners at the top of the table.

Wenger insists his team can not only overtake Tottenham and Chelsea, but also overhaul City and qualify automatically for a place in next season's Champions League group stage.


Arsenal haijawahi kumaliza nje ya top four katika Premier League tangu Wenger alipochukua majukumu mwezi September 1996.

Mara ya mwisho kwa Gunners kumaliza ligi ikiwa nafasi mbili za juu ni katika msimu wa mwaka 2004-05 when they were runners-up to Chelsea.

Race for second - key games

Man City Chelsea Spurs Arsenal
Everton (A) 16 March
Spurs (H) 14 April
Arsenal (H) 3 March
Spurs (A) 3 March
Man Utd (A) 8 April
Liverpool (A) 21 April
Chelsea (A) 14 April
Everton (H) 9 March
Spurs (A) 21 April
Man Utd (A) 4 May
Man City (H) 21 April
Man Utd (H) 28 April

 
 
 
 
 
 

Monday, January 7, 2013

Saunders;Kocha mpya Wolves

Klabu ya Wolves imethibitisha kwamba  Dean Saunders ndie meneja mpya wa timu hiyo hii nikufuatia kutimuliwa kwa aliekuwa kocha wa Wolves Stale Solbakken kutimuliwa siku ya jumamosi.

Dean Saunders Doncaster Rovers

Saunders, 48, ameiwezesha  Doncaster Rovers kusalia nafasi ya pili katika  League One msimu huu na alianza kazi ya kuwa meneja akiwa na timu ya Wrexham.

 Taarifa kutoka ndani ya klabu kupitia tovuti yao imesema: "Wolves  wanapenda kuwafahamisha kwamba Dean Saunders ndie atakuwa meneja mpya . Doncaster Rovers wamekubali kumuachia kocha huyo mwenye umri wa miaka 48 kuelekea  Molineux kufuatiwa kutimuliwa kwa aliyekuwa mwalimu wa timu hiyo Stale Solbakken siku ya jumamosi."

 Saunders ni boss wa nne wa  Wolves katika kipindi kisichopungua mwaka mmoja hii ni baada ya mwezi wa pili kutimuliwa kwa Mick McCarthy na kufuatiwa na and the Terry Connor.

YADAIWA FERGIE ANASAKA KIPA MPYA!!

WALENGWA NI BEGOVIC & REINA!

GAZETI la Uingereza, The Mirror, limeripoti kuwa Meneja wa Manchester United Sir Alex Ferguson anafikiria kumpiga shoka David De Gea na kusaka Kipa mpya katika kipindi hiki cha Dirisha la Uhamisho la Mwezi Januari.

Gazeti hilo limedai Sir Alex Ferguson amezidi kuvunjwa moyo na uchezaji wa Kipa De Gea ambae anashindwa kudhibiti eneo la Penati Boksi na mara nyingi huonekana mwenye mchecheto katika eneo hilo, hasa kwa mipira ya juu ya frikiki na kona, ambayo wapinzani wamechukulia hilo kama ni udhaifu wa Manchester United.

 The Mirror limedai kuwa Ferguson amemwomba Mkurugenzi Mtendaji, David Gill, pamoja na Wamiliki wa Klabu, Familia ya Glazers, kutoa Fedha ili kumnunua Kipa ambae ataruhusiwa kuichezea Man United kwenye Mashindano ya UEFA CHAMPIONZ LIGI Msimu huu.

Tangu atue Man United kutokea Atletico Madrid Mwaka 2011, De Gea amekuwa hana namba ya kudumu na mara nyingi amekuwa akibadilishana na Kipa mwingine, Anders Lindegaard, kutoka Denmark.

Ripoti za Gazeti hilo zimedai walengwa wa Sir Alex Ferguson ni Makipa wa Stoke City, Asmir Begovic, na yule wa Liverpool, Pepe Reina, kwani wote wataruhusiwa kuichezea Man United kwenye Mashindano ya UEFA CHAMPIONZ LIGI.

Hata hivyo, kumng’oa Begovic kutoka Stoke City itakuwa kazi kubwa kwani yeye ndie moja ya nguzo kubwa Klabuni hapo lakini duru hizo za habari zimekiri kumpata Reina ni rahisi kidogo maana inaonekana sasa Liverpool inatafuta mwelekeo mwingine kuhusu Kipa.

Andre Ayew out of Ghana squad

Meneja wa Ghana  Kwesi Appiah amethibitisha ya kwamba winga wa club toka ufaransa  Marseille  Andre Ayew hatoshiriki michuano ya African Nations Cup kwa mwaka huu 2013 huko Africa ya Kusini inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi lake tarehe 19 mwezi huu..

Ayew, 23,ameshindwa  kureport katika kambi ya timu ya taifa ya Ghana huko Abu Dhabi kutokana na kuwa majeruhi( hamstring injury), kwa maana hiyo hatokuwa katika kikosi cha wachezaji 23 kitakacho minyana huko kusini mwa Africa

Appiah said in a statement on Monday: "Unfortunately, Andre failed to report to camp and indicated that owing to the treatment he was receiving from his doctor he would report to camp on Wednesday.

kulingana na mwenendo mzima ulivyo sasa Appiah amesema kwa sasa ataendelea na wachezaji waliopo katika kambi yake,hata hivyo meneja huyo amesema Ayew atakuja kutumika siku za usoni akiwa Fit!!........

.Ayew ni mmoja ya wachezaji muhimu katika kikosi cha timu ya Taifa na mwaka 2011  alitajwa kama ndie mchezaji bora wa mwaka huo.



Wakala: Lampard lazima aondoke Chelsea.
 
Imethibitika kuwa Frank Lampard ataihama Chelsea mwishoni mwa msimu huu, kwa mujibu wa wakala wake Steve Kutner.
 
Akikaririwa na magazeti ya nchini Uingereza akisema,
"watendaji wa Chelsea walimwambia Frank kule Japan wakati wa michuano ya kombe la dunia la vilabu na hata mara baada ya ushindi dhidi ya Everton mwezi uliopita kuwa hakuna chochote kitakacho pelekea klabu kumpa ofa nyingine Lampard baada ya msimu huu"
 
"hakuna kitakacho badilika kwa vyovyote vile. Frank anapashwa kukubaliana na hayo inabidi ajikusanye kumalizia msimu kwa mafanikio katika klabu ambayo aliipenda sana."
 
Lampard alipata nguvu mpya kutokana na kushangiliwa na mashabiki wa Chelsea katika mchezo wa mzunguko wa tatu wa michuano ya FA dhidi ya Southampton jumamosi pale alipofunga goli ambalo kimsingi lilimfanya kuwa sawa na mchezaji wa zamani klabu hiyo Kerry Dixon mwenye rekodi ya juu ya ufungaji magoli, lakini inaonekana sherehe ya ushangiliaji baada ya kufunga goli akiwa katika jezi yake maarufu namba 8 mgongoni inaelekea ukingoni.
 
Mashabiki wa Chelsea wamekuwa wakitaka Lampard apewe mkataba mwingine lakini hali inavyo onekana ni kuwa hakuna nafasi nyingine ya kuendelea kusalia Stamford Bridge.
Mwenyewe Lampard amekaririwa akisema
"pengine sikuwa na mvuto wa kutosha lakini mashabiki wamekuwa na mimi katika kipindi chote ambacho tumekuwa pamoja hapa"