TRANSLATE THIS BLOG

Sunday, October 7, 2012

MBOYA CUP 2012

Ligi ya mboya cup bado inaendelea kutimua vumbi  katika uwanja wa Chera uliopo Tanga mjini br.19,ikiwa ni hatua ya mtoano kutafuta timu 11 zitakazoungana na timu moja ya best loser  na kutimia timu kumi na mbili ili kutengeneza makundi mawili(A-B)...Kila kundi litakuwa na Timu sita sita zitazochuana vikali na hatimaye kupata bingwa wa msimu huu ambae ataibuka na jezi na mbuzi kwaajili ya supu huku tukishuhudia mshindi wa pili akipewa nae zawadi ya  mbuzi kwaajili ya nyama choma.......

 Katika ligi ya safari hii ya MBOYA CUP ambayo hufanyika kila mwaka mara moja,Ligi imekuwa ngumu hasa katika hatua hii ya mtoano ambayo ukifungwa safari kwani timu shiriki  zimefanya usajili wa maana ukilinganisha na mwaka jana.

Kwamujibu wa waandaaji wa ligi ya Mboya,zipo pia zawadi mbali mbali kwa wachezaji watakao onyesha kiwango cha juu katika mechi ikiwa ni mchezaji bora,mfungaji bora,golikipa bora na timu yenye nidhamu....nk!

AWARDS


1.       Club of the Year
2.       Most Promising Talent of the Year
3.       Coach of the Year
4.       Referee of the Year
5.       Fair Play Award

Katika mchezo wa jana ambao ulishuhudiwa na mamia ya wapenda soka  tanga mjini kati ya  SQUEEZ  watoto wa barabar ya 16 vs SINAGOGI ya Msambweni C  zote zikipatikana katika manispaa  ya jiji la TANGA,waliopata fursa ya kutembelea viwanjan hapo walipata burudani ya aina yake licha ya timu hizo kufungana magoli ya Rede kwa Sinagogi kuchapa Squeez bagoli 9-4

                                                                                   (kikosi cha Sinagogi fc)
Mechi hiyo iliopigwa majira ya saa 16;30 za jioni na kushudiwa na mdhamini wa ligi hiyo Aphonce D.Mboya na kuweza kuwapatia kifuta jasho kwa timu zote mbili licha ya kuwa na karamu nyingi ya magoli timu husika zilionyesha mpira safi.

                                                                               (Timu ya Squeez kutoka br.16)

HEKA HEKA UWANJANI....PICHA NA MATUKIO
                                              Heka heka uwanjani,wengine shingo zataka kuwatoka

                Mwamuzi wakati maaruf katika mpira wa makaratasi Omar Maute akiita mpira kati 

BAADA YA MECHI MDHAMINI WA LIGI AKATOA NASAHA ZAKE

                                                    Bw.Mboya akiwapa darasa wachezaji baada ya kuisha kwa mpambano na kufurahishwa na mchezo wao

KIFUTA JASHO!!!!!!BAADA YA MCHEZO SAFI.........
                                                                       Capt.wa Squeez Rasheed akipokea sh.elf 10

Capt.wa timu ya Sinagogi Nzara Ndaro akipokea sh.elf 13 kama hongera ya kuonyesha kandanda safi kutoka kwa mdhamini wa ligi

Mpaka sasa timu zilizofuzu Katika hatua ya makundi ni Wenyeji timu ya ROAD CAMP,HARLEM CONER,MAKAMUZI,ALQAIDA na SINAGOGI....

Mboya cup inaendelea tena leo kwa mechi kati ya YEBO YEBO vs TALIBAN kutoka chumbageni...saa kumi na nusu.....

UNAKUMBUKA HIZI....KAMA ULAYA!!!!!!!!!
                                                                                    G.Kepeer wa Ngome Star
                                                     G.kepeer wa Makamuzi akifuta mkwaju wa pen......


No comments:

Post a Comment