TRANSLATE THIS BLOG

Wednesday, July 24, 2013

Sevilla wamsajili Gameiro wa PSG

Timu ya Sevilla imefanikiwa kumsajili striker Kevin Gameiro kutoka mabingwa wa ufaransa msimu uliopita Paris Saint-Germain,klabu hiyo toka hispania imethibitisha hayo leo jumatano.
kwa mujibu wa vyombo vya habari ,Sevilla watalipa kiasi cha yuro euro 10mil ambazo nisawa na  (13.2 million dollars) kwaajili ya saini ya mchezaji huyo mwenye miaka 26.

Sevilla,ambao msimu uliokwisha walimaliza ligi spain LA LIGA wakiwa nafasi ya tisa,wanatizamia sasa kukiimarisha kikosi chao hasa safu ya mbele tangu kufuatiwa kuuzwa kwa strikers wao Alvaro Negredo na Jesus Navas kwa vijana wa ligi kuu uingereza  Manchester City.

Klabu ya Sevilla imetangaza kuwa wamemtoa kwa mkopo beki wao Alberto Botia kwa timu ya  Elche ili       kupata nafasi ya kucheza zaidi.

HAYATOU AMTEUA JORDAAN KUWA MSHAURI WAKE.

OFISA mkuu wa zamani wa kamati ya maandalizi ya michuano ya Kombe la Dunia 2010, Dr Daniel Alexander "Danny" Jordaan (born 3 September 1951) ambae ni mwafrika  kusini   ameteuliwa kuwa mshauri wa rais wa Shirikisho la Soka barani Afrika-CAF Issa Hayatou.

 Katika taarifa iliyotumwa katika mtandao wa CAF imeeleza kuwa uteuzi wa Jordaan umekuja kufuatia mchango wake anaoendelea kutoka katika kunyanyua soka la Afrika. huku Hayatou akiongeza kuwa anategemea mafanikio makubwa kwa kushirikiana vyema na Jordaan.

MARADONA AFANYIWA UPASUAJI WA MACHO.

NGULI wa soka nchini Argentina, Diego Maradona amefanyiwa upasuaji wa macho ambao umemalizika kwa mafanikio.

 Maradona mwenye umri wa miaka 52 alifanyiwa upasuaji huo ili kukwangua utandu uliokuwa katika macho yake ambao ulikuwa ukisumbua kutokuona sawasawa katika mji wa Mendoza uliopomagharibi mwa Argentina.

Daktari aliyemfanyia upasuaji Roberto Zaldivar aliwaambia waandishi wa habari kuwa Maradona alikuwa akiendelea vyema na upasuaji huo ni wa kawaida kwa watu wenye umri kama wake.

Maradona anatarajiwa kufanyiwa uchunguzi kabla ya kurejea Buenos Aires na baadae kwenda Dubai ambako anafanya kazi kama balozi wa soka.

HIGUAIN KWENDA NAPOLI...arsenal hoi!!!


MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Argentina na klabu ya Real Madrid, Gonzalo Higuain inasemekana amekamilisha usajili wake kwenda Napoli ya Italia kwa mujibu ya magazeti ya nchini Hispania.

 Gazeti la AS na Marca ya nchi hiyo lilidai kuwa Napoli wamelipa kiasi cha euro 37(Ambazo ni sawa na dollar za kimarekani 48.8mil) kwa ajili saini ya nyota huyo mwenye umri wa miaka 25.

 Kama mpango huo ukikamilika Higuain atakuwa mchezaji wa tatu wa Madrid kuuzwa Napoli katika kipindi hiki cha uasajili majira ya kiangazi baada ya Raul Albiol na Jose Callejon kuwa tayari wameuzwa.

Kumbuka Napoli kwa sasa inaongozwa na Mhispania Rafa Benitez.

 Kwa mujibu wa taarifa za gazeti hilo pesa zitakazopatikana kwa mauzo ya Higuain zitatumika katika kutafuta saini za Gareth Bale wa tottenham na Luis Suarez wa Liverpool...

Kwa msisitizo!!!!!!!!...
According to media reports, Real will use the money for Higuain to bid for Gareth Bale of Tottenham and Luis Suarez of Liverpool.

SIJUTII KUINUNUA QPR - FERNANDES.

MMILIKI wa klabu ya Queens Park Rangers, QPR, Tony Fernandes amesema hajutii kuinunua klabu hiyo pamoja na kushuka daraja na kudai kuwa ana mategemeo ya kuigeuza na kuwa klabu yenye mafanikio.

 Fernandes ambaye alitenga mamilioni ya paundi kwa ajili ya kuibakisha klabu hiyo ligi kuu amesema hana mpango wa kumiliki klabu kubwa kama Liverpool au Arsenal kwani kwa kufanya hivyo ni sawa na kununua mafanikio ya wengine.

 Bilionea huyo wa Malaysia ameamua kuchagua QPR ili aweze kuipa mafanikio kama zilivyo klabu nyingine kubwa nchini Uingereza na ana mategemeo ya kurejea tena ligi kuu katika kipindi cha muda mfupi ujao.
 Fernandes ambaye pia anamiliki timu ya Caterham ya langalanga amesema alikuwa akijua kuwa kulikuwa na uwezekano mkubwa wa kushuka daraja wakati alipoinunua klabu hiyo mwaka 2011.

Monday, July 22, 2013

Scotland teyari kuivaa Uingereza

 
 Meneja wa timu ya taifa ya Scotland GORDON STRACHAN ametangaza kikosi kazi tayari kuivaa three lion(Timu ya taifa ya Uingereza) katika mechi ya kimataifa ya kirafiki itakayopigwa Wembley tarehe14 August ikiwa ni maandalizi  ya mechi yao ya  kuwania kufuzu  World Cup nyumbani dhidi ya  Belgium mwezi September. 

katika ushindi waliopata Scotland dhidi ya Croatia katika kuwania kufuzu fainali hizo mwezi june wameshuka katika viwango vya ubora wa soka kutoka nafasi ya 24 mpka nafasi ya50

Scotland squad:
Goalkeepers: Matt Gilks (Blackpool) David Marshall (Cardiff City) Allan McGregor (Hull City)
Defenders: Gordon Greer (Brighton and Hove Albion) Steven Hammell (Motherwell) Grant Hanley (Blackburn Rovers) Alan Hutton (Aston Villa) Russell Martin (Norwich City) Charlie Mulgrew (Celtic) Andy Webster (Unattached) Steven Whittaker (Norwich City) 

Evan Kangwa aitwa Zambia

Mshambuliaji wa Nkana Evans Kangwa ameitwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Zambia Chipolopolo katika maandalizi ya kufuzu 2014 African Nations Championship (CHAN) raundi ya kwanza dhidi (The Zebras)’of Botswana.

The Nkana striker ni mmoja kati ya wachezaji wawili wapya walioitwa na kocha mkuu wa Zambia Herve Renard has named to his 2013 Cosafa Cup winning team ahead of Saturday’s CHAN first round away leg game against Botswana to be played in Molepolole.

Kangwa returns to the fold for the first time since December 21, 2012 when he came on as a substitute in Zambia’s 1-0 away friendly loss to Tanzania. He also makes the team despite not playing any competitive action this year after he was hold-up in Spain on trials for the last six months.

Kangwa’s call-up swells Nkana’s contingent in the Zambia team to four joining striker Festus Mbewe plus defenders Masauso Zimba and Christopher Munthali. Also getting a recall is Zanaco defender Salulani Phiri who joins club mates Fackson Kapumbu and striker Moses Phiri.

Meanwhile, Zambia enters camp on July 22 in Lusaka to begin preparations for their CHAN qualifier this Saturday prior to departure for Gaborone on July 25.

The two sides will face each other in the return leg on August 3 with the winner advancing to the final second round qualifier to play either Zimbabwe or Mauritius for a place in next January’s CHAN finals in South Africa.

FROOME BINGWA WA MICHUANO YA TOURE DE FRANCE.

MSHINDANO ya baiskeli yajulikanayo kama Tour de France yamefikia tamati jana kwa Chris Froome wa Uingereza kutawadhwa bingwa mpya wa mashindano ambayo ni ya 100 toka kuanzishwa kwake.

 Akishinda taji hilo kwa zaidi ya dakika nne, Froome alishikana mikono na na wenzake wa timu ya Sky wakati akikatisha katika msitari wa ushindi jijini Paris, Ufaransa.

 Huo unakuwa ushindi wa pili kwa Uingereza kwenye michuano hiyo baada ya mwendesha baiskeli Sir Bradley Wiggins ambaye naye anatoka katika timu ya Sky kushinda michuano hiyo mwaka jana. Mashindano yalishirikisha waendesha baiskeli kutoka nchi mbalimbali ambapo waliendesha baiskeli kwa kilometa 3,200 katika miji mbalimbali ya ya Ufaransa katika kipindi cha wiki mbili cha mashindano hayo.

Taifa Stars kwenda Kampala Jumatano


Timu ya Taifa ya Tanzania itaondoka Mwanza Jumatano kwenda Kampala, Uganda kwa ajili ya mechi ya marudiano ya Kombe la CHAN itakayochezwa Jumamosi katika Uwanja wa Mandela kuanzia saa kumi kamili jioni. 

Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager iko kambini jijini Mwanza chini ya Kocha Kim Poulsen tangu Julai 14 mwaka huu kujiandaa kwa mechi hiyo itakayoamua ni timu ipi kati ya hizo mbili itacheza Fainali za CHAN zitakazofanyika mwakani nchini Afrika Kusini.
Timu hiyo itaondoka Uwanja wa Ndege wa Mwanza saa 7.25 mchana kwa ndege ya PrecisionAir, na inatarajiwa kutua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Entebbe saa 10.15 jioni.
Wakati huo huo, Kocha Kim Poulsen atakuwa na mkutano na waandishi wa habari kuzungumzia maandalizi ya kikosi chake Jumanne.

United ofa nyingine kwa Cesc


Manchester United manager David Moyes jumatatu ya leo amefunguka na kusema kwamba,mabingwa hao wa ligi kuu ya soka uingereza  had made a second offer kwa kiungo wa Barcelona Cesc Fabregas.
Awali United iliripotiwa kuwa  walimtengea mhispania huyo dau la £25 million,ambalo lilikataliwa kwaajili wa nahodha huyo wa zamani wa  Arsenal .
Moyes said United made a second bid and were working hard to bring the Spanish international back to England.

Moyes akizungumza mbele ya  press conference katika ziara ya United huko Japan amesema kwamba  Ed Woodward, mwenyekiti wa klabu, had received a response from Barcelona
Hata hivyo moyes amesema kwamba Woodward amejaribu  kufanya usajiliwa kwa baadhi ya wachezaji wapya kabla ya kuanza kwa msimu...

Ligi kuu ya Vodacom 2013/2014 kuanza Agosti 24



Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara msimu wa 2013/2014 itaanza kutimua vumbi Agosti 24 mwaka huu huku timu zote 14 zitakuwa viwanjani katika miji saba tofauti.
Hata hivyo, kabla ya ligi hiyo kuanza kutakuwa na mechi ya kufungua msimu (Ngao ya Jamii- Community Shield) kati ya bingwa mtetezi Yanga na Makamu bingwa Azam itakayochezwa Agosti 17 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. 

Mechi za VPL za Agosti 14 mwaka huu zitakuwa kati ya Yanga na Ashanti United (Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam), Mtibwa Sugar na Azam (Uwanja wa Manungu, Morogoro), na JKT Oljoro na Coastal Union (Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Kaluta Amri Abeid, Arusha).
Nyingine ni Mgambo Shooting na JKT Ruvu (Uwanja wa Mkwakwani, Tanga), Rhino Rangers na Simba (Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora), Mbeya City na Kagera Sugar (Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine, Mbeya), na Ruvu Shooting na Tanzania Prisons (Uwanja wa Mabatini, Mlandizi, Pwani).
Mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo utamalizika Novemba 3 mwaka huu wakati wa pili utamalizika Aprili 27 mwakani.