TRANSLATE THIS BLOG

Sunday, October 7, 2012


Neymar: Oscar anataka mimi nijiungeChelsea

Nyota wa klabu ya Santos ya Brazil Neymar amesema kwamba,mchezaji mwenzake katika kikosi cha timu yaifa ya Brazil Oscar anamtaka yeye kujiunga na Chelsea,wakati huo huo  Dani Alves nae amejaribu kumshawishi aelekee Barcelona - akiwaelezea watu hawa wawili amesema ..... "very good salesmen".



Neymar amekuwa moja ya wachezaji ambao wanawindwa kwa udi na uvumba na vilabu bingwa barani ulaya na vigogo wa Spain Barca and Real Madrid na kuna hofu huwenda moja kati ya timu hizi kubwa ikafanikiwa ikiwa Neymar ataamua kuondoka Brazil.
Kwa sasa  Chelsea  huwenda nao wakaanza kiminyano baada ya kuibuka taarifa kwamba  Oscar anaekipiga klabuni hapo ambae pia anacheza timu moja ya Taifa na Neymar amekuwa akimshawishi kijana huyo mwenye miaka 20 kujiunga na the blues na kumuelezea faida za kuishi Stamford Bridge.

Hata hivyo si Oscar pekee ambae amejaribu kumshawish kinda huyo wa kibrazil kujiunga nae...Beki wakimataifa toka Brazil na klabu ya Barcelona  Dani Alves amekuwa pia akimwambia ahamie Catalans kama anataka kuja ulaya.

"Neymar amesema ujumbe wa maandishi alioupata toka kwa Oscar ulikuwa ukimuelezea jinsi gani klabu kubwa  chelsea ilivyo na jinsi jiji la London lilivyo..akamzungumzia Oscer na Dan Alves akisema nivery good salesmen for their club.," Neymar amesema hayo wakati wa mazungumzo na The Sun

No comments:

Post a Comment