TRANSLATE THIS BLOG

Monday, September 24, 2012

vituko na matukio duniani

ladha kitandani.

Wanasayansa kweli wana visa.

Wiki hii wamekuja na utafiti wa ajabu. lakini utafiti wenye manufaa kwa wengi.

Watu wengi, sio wanawake wala wanaume huwa na matatizo ya unyumba lakini hawasemi. Hujitangazia ushujaa wa urongo. Utamsikia mtu akisema mimi? Wee...kube wapi Bure kabisa.

Lakini wanasayansi wa uingereza wamegundua kwamba kuna njia rahisi na eti ya kuaminika bola mtu kutumia madawa ya kusisimua ashiki.

Wanasayansi hao wa shirika la Retailer Littlewoods wanasema siri ya ubingwa kitandani unategemea bed shiti au mashuka ya vitandani.

Katika utafiti waliofanyia familia 2,000 za uingereza, watafiti hao wamegundua kumbe bed-shiti au mashuka ya rangi ya zambarau au purple ni kiboko yao.

Wanasema ukiongezea kwa kupaka kitanda chako au fanicha za bedroom rangi hiyo ya zambarau basi matokeo hua ya kuridhisha. Na

Utafiti huo unaonyesha kuwa waliotumia rangi hiyo walifaulu kuonana kimwili wastani ya mara 4 katika wiki moja na wale waliotumia ma bed shiti ya rangi nyegine matokeo ilikuwa ni kujitahidi na kufaulu mara moja peke yake.

shirika hilo la Retailer Littlewoods la uingereza linasema shuka hizo au bed-shiti hizo za rangi ya zambarau zikiwa aina ya silk au hariri basi...we..we we....

Mapenzi na magari

Sijui ni wazimu au nikupagawa ?.

Lakini Edward Smith Washington Marekani anasema yeye ni Mzima na akili zake.

Edward Smith hana haja na mpenzi anayetembea kwa miguu miwili.

Mmarekani huyo anasema sio hata hana hisia , anazo tena nyingi. Lakini sio kwa binadamu.

Edward Smith ambaye ni mtunzi wa mashairi ana fanya mapenzi na gari, kufanya mapenzi kwa maana halisi ya kufanya mapenzi . Smith anasema akiwa na hamu hufanya na gari kama vile nissan, pudjo, mercidez benz na vitu kama hivyo, lakini sio mtu.

Shirika la habari la Reuters limeripoti kwamba kwa wakati huu Edward Smith anafanya mapenzi na gari lake jeupe la Volkswagen Beetle .

Usiniulize anafanya mapenzi vipi na magari. Mimi sijui.

Lakini Edward Smith amefichua kuwa mara ya kwanza kufanya mapenzi na gari alikuwa na umri wa miaka 15, tena gari la babake aina ya Range Rover.

Na kwa yale mahaba aliyonayo kwa mpenzi wake wa sasa Volkswagen Beetle ambaye ameeishi naye kwa miaka mitano,amelibandika kipenzi chake jina la Vanilla.

My sweet vannila wala sio my sweet Elizabeth.

My sweet Elizabeth kanda bongoman...

Papasa ya Makalio

Nyie wapenzi wa soka hasa ligi ya primia mshaona hili.

Mchezaji tuseme wa Man U akicheza vizuri uwanjani utaona mchezaji mwenzake au hata kocha wake kama Sir Alex Furgeerson , akimpiga piga makalio...mimi nadhani ni ishara ya pongezi..well done..well done.

Lakini Afghanistani! Weeeee. Mwiko.

Wanajeshi wa marekani au uingereza wanaohudumu huko wamewahi kipigwa risasi kwa kuwapapasa au kumpiga piga tako mwanajeshi wa Afghanistan.

Sasa wizara ya ulinzi ya Afghan imeamua kutoa mafunzo maalum kwa wanajeshi wake kwamba kubalini kupapaswa makalio na wamarekani hizo kwao ni ishara za pongezi au salamu.

Mafunzo haya maalum yanenza baada ya visa vya wanajeshi wa Afghan kuwauwa wanajeshi wa marekani katika siku za hivi karibuni.

Msemaji wa Wizari ya Ulinzi wa Afghanistan Zahir Azimi amesema wanajeshi wote karibu laki mbili watapewa mafunzo ya kuwaelewa Wamarekani na kukubali salamu zao.

Mwaka huu peke yake wanajeshi wa Afghan wamewapiga risasi na kuwauwa walimu wao wa kimarekani 45. Kwa kumbe sababu ni hizo za kupigwa pigwa makalio eti ni pongezi.

Kwa Mafghanistan hakuna pongezi za hivyo.

Dada Mpiga Kabari

Wiki hii mjini New Jersy Marekani madereva wawili waliishia kucheka baada ya kushuhudia ujambazi.

Ilikuwa ni eneo la Plainfield ambapo walisikia mtu akipiga kelele akiomba msaada.

Kufika wakamkuta jibaba fulani wanang'ang'ana na mwana dada fulani.

Madereva hao wawili mara moja wakaamua kumsaidia yule dada asiimbie na jambazi mwanamume.

Kumbe wapi?

Jambazi alikuwa ni mwana dada alikuwa amemshika kabari yule baba aseweze kupumua.

Kufumba na kufumbua , jamaa chini amewacha hoi, dola 400 zimekwenda na mkufu wake wa dhahabu pia umekwenda.

Jamaa alibaki akigaagaa kwa maumivu na mwingi wa manung'uniko.

Kazi ni Kazi

Nani anataka kazi?

Sri lanka imetangaza kazi mbili na mshahara wake ni mnono ajabu.

Sri Lanka kwa haraka upesi inatafuta wanyongaji.

Watu wa kuwanyonga wafungwa 480 ambao wamehukumiwa kunyongwa kwa makosa mbali mbali katika nchi hiyo iliyo kusini mwa India.

Ikiwa inataka kazi ya kunyonga watu Sri Lanka tuma maombi yako sasa hivi. Shirika la Habari la Reuters linasema kwamba ijapo watu 176 tayari wameshahojiwa lakini zoezi la kutafuta mnyongaji mzuri bado linaendelea.

Kazi ni kazi ndio ujumbe wetu

Mungu akituwezesha tukutane tena wiki ijayo.

Mimi ni Odhiambo Joseph

No comments:

Post a Comment