TRANSLATE THIS BLOG

Friday, November 16, 2012


KATIKA kuhakikisha  ari ya wachezaji inarudi kama ilivyokuwa mwanzo, uongozi wa klabu ya Simba una mpango wa kuipeleka timu nje ya nchi ili kuwapa muda wachezaji wa kusahau yaliyopita na kujipanga vema kwa mzunguko wa pili. 

Aidha, uongozi wa mabingwa hao watetezi wa ligi kuu ya Vodacom, umemuomba radhi kipa na nahodha wake, Juma Kaseja kutokana na kudhalilishwa na baadhi ya watu baada ya timu hiyo kuwa na mwenendo usioridhisha katika michezo yake ya mwishoni mwa mzunguko wa kwanza. 

Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage amesema leo kwamba  kudhalilishwa kwa Kaseja si sahihi kwani anaweza kukofanya makosa ya kiufundi kama binadamu mwingine, hivyo anahitaji ushauri wa kimawazo. 

“Tuache kudhalilisha wachezaji kwani kufanya hivyo si uungwana wa michezo hata kidogo…kila mtu anafahamu kuna kushinda, kufungwa na kutoka sare, kama hatutaki kufungwa tujiondoe wenye ligi,”alisema Rage


Kuelekea mchezo wa jumapili baina ya timu ya soka ya vijana ya Tanzania bara Serengeti Boys dhidi ya timu ya vijana ya Congo Brazzaville utakaopigwa uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam,  kocha msaidizi wa Serengeti Boys Jamhuri Kihwelu 'Julio' amesema wataingia katika mchezo huo wakiwa na rufaa mkononi kutokana na kile alichokieleza kuwa wachezaji wengi wa Congo wanaonekana kama wana umri mkubwa.

Julio amesema amepata nafasi ya kuwaona wachezaji hao asubuhi ya leo wakati wakifanya mazoezi na ushahidi wa machoni unaonyesha wazi kuwa wachezaji hao wengiwao si chini ya umri wa miaka 17.

Julio amesema anaimani kuwa wachezaji waliopimwa vipimo vya umri na shirikisho la soka barani Afrika CAF kwa siyo hao walikokuja nchini. 

Jana Rockersports ilikuwa ikiongea na kocha Jacob Michelsen kuhusiana na wasiwasi wa kucheza na wachezaji vijeba ambao wengine walishiriki kombe la dunia mwaka jana na kutolewa katika hatua ya 16 bora na Uruguay, kimsingi amesema hilo analiacha kwa shirikisho la soka TFF.

Sasa Rockersports imejaribu kuperuzi mtandao wa shirikisho la soka duniani fifa ambapo imebaini wachezaji ambao ni zaidi ya umri wa miaka 17. 

Katika kikosi kilichoshiriki kombe la dunia kwa vijana nchini Mexico kuna wachezaji 8ambao wana umri zaidi ya miaka 17 ambao wamezaliwa si zaidi mwezi oktoba mwaka 1994 ambao kimsingi wamezidi umri wa miaka 17



Uongozi wa klabu bingwa Tanzania Bara Simba ya mtaa wa Msimbazi umeamua kufutilia mbali kamati zake zote kwa lengo la kujipanga upya kwa ajili ya ligi kuu ya soka Tanzania Bara pamoja na michuano klabu bingwa barani Afrika.

Kauli ya kuvunja kamati hizo imetolewa na mwenyekiti wa klabu hiyo  alhaji Ismail Aden Rage(mbunge) katika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika katika makao makuu ya klabu hiyo Kariakoo mtaa wa Msimbazi  jijini Dar es Salaam.

Rage ambaye hata hivyo hakutaja ni lini kamati mpya zitaundwa, pia amekiri kuwa matokeo ya michezo ya mwisho ya timu yao hayakuwa mazuri kiasi cha kuwasikitisha wanachama na wapenzi  wa  klabu yao.

 Amesema mfululizo wa kuendelea kuharibu kulitokana na wachezaji wa timu hiyo kuharibikiwa kisaikolojia na kwamba ili kuhakikisha hali hiyo inaondoka katika vichwa vya wameamua kuitoa timu yao nje ya nchi katika kujaribu kuwarejesha mashindanoni ambapo ameahidi kutanga nchi hiyo baadaye.

Amewataka wanachama na wapenzi wa Simba kufahamu kuwa katika kipindi hiki ligi ya Tanzania bara imekuwa katika ushindani mkubwa hivyo ni vema wakawa wavumilivu na hali hiyo tofauti na ilivyoljitokeza katika siku za hivi karibuni ambapo kikundi cha wanachama kimoja kiliibuka na kutaka kuhatarisha hali ya amani ya klabu yao.

Pia Rage ametangaza kulifuta tawi la Simba la Mpira pesa ambalo uongozi wa Simba umesema lilichochea vurugu za hivi karibuni ambapo pia Rage ametangaza kumfuta uanachama mwenyekiti wake Masoud Awadhi kwa kuitisha kikao batili cha wanachama pia kutokana na kutokulipa ada ya uanachama kwa miaka mitatu.

Novemba 5 kuliibuka tafrani katika makao makuu ya klabu hiyo ambapo wanachama wa tawi la mpira pesa na baadhi ya wapenzi wa timu waliutaka uongozi wa juu wa klabu hiyo kuondoka na kuwaachia simba yao.

Mbango yalisomekam "Kaburu na Kaseja ondokeni tuachieni Simba yetu" jambo lilionekana kama vurugu zimeanza msimbazi lakini jitihada za msemaji wa klabu hiyo Ezekiel Kamwaga kuwatuliza wanachama zilizaa matunda kwa kujibu hoja mbalimbali za wanachama zilizoibuka kupitia vyombo vya habari.


KLABU BINGWA AFRIKA kujulikana Jumamosi huko Tunis, Esperance v Al Ahly!!
BINGWA kuzoa DOLA 1.5 MILIONI!!
BINGWA kucheza FIFA KLABU BINGWA DUNIANI Japan Desemba!!!

Mechi ya marudiano ya Fainali ya kutafuta Klabu Bingwa Afrika, CAF CHAMPIONZ LIGI, kati ya Mabingwa watetezi Esperance ya Tunisia na Al Ahly ya Misri itachezwa ndani ya Rades Stadium huko Tunis, Tunisia Jumamosi Oktoba 17 na Timu hizi zinaingia Uwanjani baada ya kutoka 1-1 huko Cairo, Misri huku Esperance wakitaka sare ya 0-0 au ushindi ili kujiunga ile Klabu Spesho ya Timu 3 tu katika historia kuweza kutetea vyema Taji lao la Ubingwa wa Afrika.

Al Ahly, TP Mazembe ya Congo DR na Enyimba ya Nigeria pekee ndio ziliwahi kufanikiwa kutetea vyema Taji la Ubingwa wa Afrika.

Esperance, ambao wametwaa Ubingwa wa Afrika Mwaka 1994 na 2011, wana kibarua kigumu kwani licha ya Al Ahly kuwa Mabingwa wa Afrika mara 6, Klabu hiyo ya Tunisia itaingia kwenye Mechi hii bila ya Nyota wake kadhaa ambao ni majeruhi na wengine wapo kifungoni.

Wachezaji ambao wana Kadi na hawatacheza ni Staa wao kutoka Ghana, Harrison Afful, na Sameh Derbali na majeruhi wao ni pamoja na Majdi Traoui.

Al Ahly itamkosa Beki Sayed Moawad ambae ameumia mguu lakini mmoja wa Makocha wao, Mohamed Youssef, amesema wataziba pengo hilo na wataingia Uwanjani kwa lengo moja tu la kushambulia mwanzo hadi mwisho.

Na ili kudhibiti usalama Uwanjani, Uwanja wa Rades, ambao kawaida huingiza jumla ya Mashabiki 60,000, kwenye Fainali hii ni Watu 35,000 tu ndio wataruhusiwa kuingia.

Mshindi wa Fainali hii atatawazwa kuwa Klabu Bingwa Afrika na kuzoa kitita cha Dola Milioni 1 na Nusu na pia ataiwakilisha Afrika katika Mashindano ya FIFA ya kusaka Klabu Bingwa Duniani yatakayochezwa huko Japan Mwezi Desemba.

---------------------------------------------------------------------


ROONEY;NITAIVUNJA RIKODI YA SIR CHARLTON 

Wayne Rooney amedhamiria kuivunja rekodi ya ufungaji iliyowekwa na Sir Bobby Charlton katika klabu ya Manchester United na timu ya taifa ya England.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27 kwasasa yuko katika nafasi ya nne ya wafungaji bora waliowahi kupita United akiwa ameshafumania nyavu mara 185 ambayo ni pungufu ya mabao 64 ya Charlton ambaye anaendelea kushikilia rekodi ya ufungaji ya klabu hiyo ya mabao 249.

Katika timu ya taifa ya England ‘Three Lions Rooney’ Rooney amefunga jumla ya magoli 32 ambayo ni pungufu mabao 17 kufikia rekodi ya Charlton ya mabao 49.

Amekaririwa Rooney akisema
"Sir Bobby anashikilia rekodi zote mbili,  hii ni changamoto kubwa sana, jamaa ni mwasisi katika klabu kwahiyo ni kama mtu ambaye anaendelea kuwepo katika klabu, kama nitafanikiwa kuvunja rekodi yake ya ufungaji bora katika klabu na hata katika timu ya taifa hilo litakuwa ji jambo la kupendeza."

Rooney pia anataka kucheza soka katika kipindi kirefu zaidi kama ilivyo kwa Ryan Giggs na Paul Scholes wachezaji ambao wanamvutia kwa kuendelea kuwepo kwa zaidi ya muongo mmoja.

Terry nje kwa wiki tatu 

Meneja wa Chelsea Roberto Di Matteo amethibitisha kuwa John Terry atakuwa nje ya uwanja kwa takribani wiki tatu kufuatia kuwa majeruhi wa mguu.

Kuna wasiwasi kuwa huenda mlinzi huyo wa kati akaendelea kuwa nje kwa kipindi kirefu zaidi kutokana na kuwepo taarifa kuwa mguu wake ambao aligongana na mshambuliaji wa Liverpool Luis Suarez katika mchezo wa jumapili uliomalizika kwa sare ya bao 1-1, kupinda kidogo.

Mlinzi huyo wa kimataifa wa England alionekana akigumia kwa nguvu kutokana na maumivu na kisha kutolewa nje kwa kutumia machela katika dimba la Stamford Bridge ambapo kipimo cha 'MRI scans' hapo kabla kikonyesha alipatwa na madhara kidogo katika mshipa wa mguu.

Hata hivyo bosi wa ‘The Blues' Di Mateo ametanabaisha kuwa mlinzi huyo mwenye umri wa miaka 31 atakosekana kwa wiki tatu jambo ambapo amesema ni pigo kwa kikosi chake.


Papiss Cisse hatihati kuikosa Newcastle v Swansea...

Bosi wa Newcastle Alan Pardew ametoboa kuwa Papiss Cisse huenda asicheze Mechi ya Ligi Kuu Jumamosi dhidi ya Swansea kwa sababu ya mgogoro na Senegal kufuatia Straika huyo kutojiunga na Timu ya Taifa ya Senegal ambayo Jumatano, Siku ya Kalenda ya FIFA, ilicheza Mechi ya Kirafiki na Niger.

Inadaiwa sasa Senegal wametishia kuitumia Sheria ya FIFA ya kumfungia Papiss Cisse kwa Siku 5 kwa sababu hawakujulishwa kuhusu Mchezaji huyo kutojiunga na Timu ya Taifa.


Pardew amedai Cisse alikuwa na maumivu ya mgongo aliyoyapata kwenye Mechi ya Jumapili iliyopita waliyofungwa 1-0 na West Ham ambayo yalimlazimu Mchezaji huyo kutolewa nje kwenye Mechi hiyo.

Newcastle imedai ilituma Ripoti ya Madaktari kuhusu Cisse kwa Barua Pepe kwa Chama cha Soka cha Senegal lakini Pardew amesema inaelekea haikupokelewa.

Ikiwa Cisse, Miaka 27, ataikosa Mechi na Swansea hilo litakuwa pigo kwa Newcastle ambao wanahitaji ushindi kwa vile wameshinda Mechi moja tu kati ya sita zilizopita za kwenye Ligi.

Pardew amesema kuwa wanawasiliana na FA ya England na Viongozi wa Senegal ili kupata uhakika kama wanaweza kumtumia Mchezaji huyo Jumamosi.

Luis Suarez ni furaha kubakia Liverpool Miaka mingi!!

Straika wa Liverpool Luis Suarez amesema anafurahia kubakia Liverpool na anataka awe hapo kwa Miaka mingi ingawa sasa kuna tetesi kubwa Manchester City wanataka kumsaini Mwezi Januari Dirisha la Uhamisho likifunguliwa.


Mwanzoni mwa Msimu huu, Suarez alisaini Mkataba mpya na Liverpool na Msimu huu amekuwa kwenye fomu nzuri kwa kufunga Mabao 11 katika Mechi 16 alizochezea Liverpool.

++++++++++++++++++++++++++
Luis Suarez akiwa Liverpool
-ALISAINIWA: Januari 2011 (£22.7m)
-MECHI: 68
-MAGOLI: 32
++++++++++++++++++++++++++

Hata hivyo, Meneja wa Liverpool, Brendan Rodgers, amesema Mchezaji huyo hauzwi.

Rodgers ametamka: “Tukimpoteza Suarez hatuna Straika, hivyo hatuwezi kumuuza.”

Tangu atue England Suarez, licha ya kufanya vizuri akiwa na Liverpool, amekuwa akikumbwa na migogoro ya mara kwa mara.

Alifungiwa Mechi 8 baada ya kumkashifu Kibaguzi Beki wa Manchester United Patrice Evra na baada ya hapo akazua mzozo mpya baada ya kukataa kumpa mkono Evra Timu za Liverpool na Man United zilipokutana Old Trafford.

Hata hivyo, Msimu huu, Wachezaji hao walipeana mikono Timu zao zilipokutana.

Hivi karibuni aliandamwa kwa madai kuwa hujiangusha makusudi kwenye Eneo la Penati ili kuwahadaa Marefa apewe Penati tabia ambayo wakati mwingine imemdhuru mwenyewe kwa kunyimwa Penati za wazi huku Marefa wakidhani anawadaa.

------------------------------------------------------------


Dante: Nimekuja Bayern kusaka mataji na si kuuza sura


Mlinzi wa kati wa Bayern Munich Dante amesema waziwazi kuwa kilichomshawishi kujiunga na klabu hiyo si kingine isipokuwa anahitaji kushinda mataji.

Mlinzi huyo wa zamani wa Borussia Monchengladbach alijiunga na Bavaria kwa ada ya euro million 4.7 katika kipindi cha uhamisho wa kiangazi baada ya kuipa mafanikio Gladbach katika msimu wa 2011-12 ambapo ilimaliza katika nafasi ya nne katika msimamo wa ligi ngumu kabisa ya nchini Ujerumani ‘Bundesliga’.

Akiwa hajawahi kushinda taji lolote kubwa katika soka , mlinzi huyo mwenye umri wa miaka 29 anafikiria ndoto yake itatimia kwa kujiunga na kikosi cha kocha Jupp Heynckes.
-------------------------------------------------------------------

Wakati huo huo.......

Msemaji wa Kiungo na nahodha wa zamani wa England David Beckham amekanusha taarifa kuwa mchezaji huyo ana mpango wa kuihama klabu yake ya LA Galaxy na kuelekea nchini Australia baada ya shirikisho la soka nchini Australia (FFA) kudai kuwa kiungo huyo ambaye kwasasa ana umri wa miaka 37 alikuwa anaitamani ligi kuu ya soka ya nchi hiyo ya A-League.

Msemaji wa FFA amedokeza kuwa mchezaji huyo wa zamani wa Manchester United alikuwa katika mpango wa kufuata nyayo za akina Alessandro Del Piero na Emile Heskey na kujiunga na soka la Australia.

Taarifa kupitia msemaji wa FFA ambazo zilionyesha ni kama kuifagilia ligi ya Australia imesomeka
"kuja kwa David Beckham ni ishara kuwa hadhi ya ligi yetu ya Hyundai A-League imekuwa duniani.

"Beckham ni nyota mkubwa sana duniani na atakuwa mtu mwingine mkubwa katika soka kujiunga na Hyundai A-League baada ya kuja kwa Alessandro Del Piero, Emile Heskey na Shinji Ono. Lakini kwasasa ujio wake bado uko katika hatua za awali"

Hata hivyo msemaji wa Beckham amekanusha taarifa hizo akisema mchezaji huyo kwasasa ana furahia maisha katika jiji la Los Angeles na hana mpango wa kuondoka.


Ronaldo arejea mazoezini Real

Cristiano Ronaldo returned to training with his international Real Madrid team-mates on Thursday afternoon, with Jose Mourinho having no new injury problems to deal with ahead of Saturday's La Liga clash with Athletic Bilbao at the Estadio Santiago Bernabeu.

The eye injury suffered by the Portuguese attacker during last weekend's win at Levante ruled him out of Portugal's friendly in Gabon this week, with Ronaldo suffering "dizzy spells, problems with his vision and a headache" after the game, according to Portuguese FA doctor Henrique Jones.
However, the 27-year-old was back training as normal at Madrid's……

Wednesday, November 14, 2012


Japan wakaribia kufuzu kombe la Dunia 

November 14, 2012
By mwambao fm  staff

Japan wameshinda  2-1 dhidi ya  Oman na kuwafanya wawe katika nafasi nzuri ya kufuzu kucheza world cup 2014 huko brazil 


Keisuke Honda in action for Japan against Oman


Shinji Okazaki alikuwa shujaa wa Japan katika dakika za majeruhi baada  Ahmed Mubarak's deflected free-kick cancelled out Hiroshi Kiyotake's first-half opener.

Japan, hawakushiriki kombe la dunia tangu mwaka 1998, sasa wana 13 points katika michezo 5 na wakiwa pointi 8 zaidi ya yule anaekamata nafasi ya pili Australia having played one more game.

Jordan wamepokea kichapo  1-0  toka kwa  Iraq  huko  Doha. Hammadi Ahmed alifunga goli katika dk ya  86t grab and move Iraq level with theSocceroos.




          Serbia hatarini kushukiwa na rungu la FIFA

Shirikisho la soka nchini Serbia SFA huenda likakumbwa na rungu la FIFA kufuatia machafuko yaliyozuka katika mchezo kati ya timu ya Taifa ya Serbia dhidi ya Wales na kupelekea kuvurugika kwa mechi hiyo ya kufuzu kwa kombe la dunia.


FIFA imethibitisha kuwa bado ipi katika mchakato wa kupeleleza tukio hilo lililotokea Septemba 11 pale Wales walipopachikwa mabao 6-1.

Rungu la FIFA litawashukia pia watakaobainika kuhusika na tukio jingine kama hilo ambalo lilijirudia mwezi Oktoba kwenye mechi kati ya Croatia na Macedonia ambao nao wapo katika kundi hilo.

Kesi zote hizo zitasikilizwa na kamati ya nidhamu ya FIFA Novemba 20, mwaka huu wakati Shirikisho la kandanda barani Ulaya kwa upande wake limetenga Novemba 22 kama siku ya kushughulikia sakata hilo.

Kesi hiyo itaweka bayana malalamiko juu ya tabia zilizoonyeshwa na wachezaji wao, wakati Serbia pia watahojiwa juu ya kauli za ubaguzi wa rangi zilizotolewa na mashabiki.


Santos imethibitisha kumtaka Robinho.

Kocha wa Santos Muricy Ramalho ameweka wazi kuwa klabu yake ina matumaini makubwa ya kumrejesha mshambuliaji wa AC Milan Robinho katika uhamisho wa mwezi Januari.

Taarifa kutoka nchini Brazil zimedai Robinho, Nene, Pablo Aimar na Diego ni miongoni mwa wachezaji walio katika orodha ya kocha Ramalho kwa ajili ya msimu ujao wakati ambapo kuna tetesi kuwa huenda klabu hiyo ikampoteza mshambuliaji wake hodari Felipe Anderson.

Mapema wiki hii alikaririwa mwanasheria wa Robinho Marisa Alija akisema Robinho ana matumaini ya kurudi Santos, lakini alikataa kusema itakuwa lini.

"tunasikia mengi juu ya Robinho lakini tukumbuke ana mkataba na Milan mpaka 2014,"
 "hajaniambia chochote juu ya kurejea Santos msimu ujao. Lakini anashindwa kuficha juu ya nia yake ya kurejea lakini katika hatua hii sidhani kama itawezekana."
-------------------------------------------------------------------

NA.....

Mshambuliaji wa kimataifa wa Sweden Zlatan Ibrahimovic anaamini wakati umefika sasa kwa kiungo mzoefu wa Liverpool Steven Gerrard kuondoka katika soka na England na kujiunga na vilabu vingine vikubwa nje ya nchi yake.

Ibrahimovic ametoka maoni yake hayo wakati huu ambapo Sweden inaelekea kucheza na timu ya taifa ya England maarufu kama Simba watatu mjini Stockholm ukiwa ni mchezo wa kimataifa wa kirafiki.

Muda mfupi baada ya mchezo wao akiwa na klabu yake ya Paris Saint-Germain dhidi ya Liverpool Zlatan alionyesha wazi kumkubali Gerrard, lakini akasema ni muda muafaka kwa Skipper huyo kuondoka Premier League.

"nadhani Steven Gerrard anaheshimika kote barani ulaya,  nafahamu hilo kwasababu mara nyingi kocha huwa anasema kuwa muangalifu na Gerrard kwasababu ndiyo mchezaji anaye leta utofauti uwanjani.

"lakini licha ya Liverpool kuwa klabu kubwa Ulaya, ningependa kumuona Steven katika klabu nyingine kubwa Ulaya.
"kwangu mimi mchezaji mzuri ni yule anaye onyesha utofauti kila sehemu. Nina uhakika Steven Gerrard anaweza."
--------------------------------------------------------------------------

leo ni mechi za kimataifa za kirafiki!!!!!...



Wilfried Bony kujiunga na Chelsea Januari.

Mshambuliaji wa Vitesse Wilfried Bony amekaribisha tetesi juu ya klabu ya Chelsea kutaka huduma yake katika kipindi cha uhamisho cha mwezi January.

Bony mwenye umri wa miaka 23, amekuwa katika kiwango huko Eredivisie tangu kuihama klabu yake ya zamani ya Sparta Prague mwezi January 2011, akiwa amesha pachika wavuni jumla ya mabao 12 baada ya kushuka dimbani mara 11 katika msimu huu.

Mapema mwezi huu wakala wa mchezaji huyo Francis Kacou alinukuliwa akisema,
"kuna vilabu kadhaa vya ligi kuu nchini England vimeonyesha nia ikiwemo Chelsea na Aston Villa"
Katika mahojiano yake na jarida moja la nchini Czech la  Pravo, nyota huyo wa kimataifa wa Ivory Coast alithibitisha kuwa angependelea kuelekea Stamford Bridge.

"sitaki kuongea mengi kuhusu hilo lakini kama imeandikwa kuwa nakwenda huko basi ni kitu kizuri"
 "kama wananitaka nitakuwa ni heshima kubwa. Napenda kujiunga na klabu kama hiyo, napenda soka na England na siogopi kwenda huko. Chelsea ni klabu kubwa"

Mkurugenzi wa michezo wa Chelsea Michael Emenalo hivi karibini alielekea Arnhem kuangalia mchezo baina ya  Vitesse dhidi ya FC Twente ambao ulimalizika kwa sare ya 0-0.


Pele apata nafuu baada ya kufanyiwa upasuaji wa nyonga.


Nyota wa zamani wa klabu ya Santos na timu ya taifa ya Brazil ambaye pia ni alama muhimu katika ulimwengu wa soka Edison Arantes do Nascimento ‘Pele’ amefanyiwa upasuaji wa nyonga na inaarifiwa ya kwamba anaendelea vizuri baada ya kuwa katika uangalizi mzuri mjini Sao Paulo.

Pele ambaye kwasasa ana umri wa miaka 72, alifanyiwa upasuaji huo katika hospitali ya Albert Einstein licha ya kwamba hakuna habari zaidi zilizo tolewa ikiwa ni agizo kutoka kwa familia ya gwiji huyo wa soka wa zamani.

Msemaji wake Jose Fornos ameidokeza Agence France-Presse akisema;
"kila kitu kimekwenda vizuri na ulikuwa ni upasuaji mdogo" 

Pele anaangaliwa kama ni mchezaji mkubwa kuwahi kutokea duniani akifunga magoli 1,300 na kushinda mataji matatu ya kombe la dunia katika miaka ya 1958, 1962 na 1970 katika cha uchezaji wake ulio tukuka.

Baada ya kuendelea kushikilia rekodi nyingi za dunia katika soka, hatimaye Pele wiki iliyopita alishuhudia moja ya rekodi yake ikivunjwa na mshambuliaji wa kimataifa wa Argentina na klabu ya Barcelona Lionel Messi ya kufunga magoli 75 katika kipindi cha mwaka mmoja



 Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars imefanikiwa kuifunga timu ya Taifa ya Kenya Harambee Stars bao 1-0 katika mchezo uliofanyika katika uwanja wa CCM  Kirumba mkoani Mwanza.

Bao pekee la Taifa Stars limefungwa na mlinzi wake wa kati Aggrey Morris kwa kichwa katika dakika ya 5 ya mchezo huo.

Stars iliingia dimbani hii leo ikiwa ina muda wa siku mbili kambini  jambo ambalo limeonekana timu hiyo inahitaji kupongezwa kwa mchezo mzuri ambao umeonekana kuwavutia watazamaji wengi.

Kwa Harambee stars huu ni mchezo wao wa pili kupoteza katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita ambapo mwezi Oktoba ilifungwa mabao 2-1 na Afrika Kusini mchezo uliofanyika jijini Nairobi.

Hii leo Harambee Stars ilikuwa ikiongozwa na mshambuliaji wake Denis Oliech akisaidiana na wakali kama Ayubu Timbe Masika Jerry Santo na James Wakhungu Situma,  ambapo ilikuwa ikicheza mchezo wa kasi na kujiamini zaidi karibu sehemu kubwa ya mchezo lakini hata hivyo utulivu wa wachezaji wa Stars uliwasaidia katika kuharibu mipango ya Harambee Stars.

 Baada ya mchezo huo kocha wa Taifa Stars Kim Poulsen amekipongeza kikosi chake kwa kusema wamecheza mchezo mzuri licha ya mazoezi ya muda mfupi.

Amekiri Harambee Stars ni timu nzuri lakini nidhamu ya kimchezo ya vijana wake imesaidia kuweza kuwadhibiti wapinzani wao.

   kuelekea katika michuano ya Challenge atakuwa na muda wa kutosha wa kufanya maandalizi mazuri zaidi kabla ya kuanza kwa michuano hiyo ambayo safari hii yatafanyika nchini Uganda.

Kwa upande wake kocha wa Harambee Henri Michel amesema kikosi chake kimecheza mchezo mbovu katika mchezo wa leo na kwamba kabla ya michuano ya Challenge atalazimika kufanya mabadiliko makubwa katika kuimarisha kikosi hicho. 

Taifa Stars baada ya mchezo wa leo itakuwa imebadili jina na sasa kuitwa Kilimanjaro Stars na itaendelea kuwepo mkoani Mwanza ikiendelea na maandalizi yao kabla ya kuelekea nchini Uganda tayari kwa michuano ya Kombe la Challenge ambapo Tanzani Bara itakuwa katika kundi moja pamoja na Burundi, Sudani Kaskazini pamoja na Somalia.

Wachezaji Nasoro Chollo na Aggrey Moris wanatarajiwa kuondoka katika kambi ya timu hiyo hapo Kesho na kuelekea Zanzibar kujiunga wa wenzao katika kambi ya timu ya Taifa ya Zanzibar inayojiandaa kwa ajili ya michuano ya Challange.

  Kikosi cha Stars Kilichoanza dhidi ya Harambee Stars: Juma Kaseja, Kelvin Yondani, Aggrey Morris, Erasto Nyoni, Amir Maftah, Shomali Kapombe, Salum Abubakar, Amri Kiemba, Mwinyi Kazimoto na Thomas Ulimwengu.

 Wachezaji waliotokea benchi ni pamoja na Shabani Nditi, Simon Msuva, John Bocco, Amri Kiemba na Issa Rashidi. 


Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limefanya mabadiliko kwa kiingilio cha juu cha mechi ya raundi ya mwisho ya mchujo kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 kati ya Tanzania (Serengeti Boys) na Congo Brazzaville itakayochezwa Jumapili (Novemba 18 mwaka huu).

Awali kiingilio cha juu katika mechi hiyo itakayofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni kilikuwa sh. 5,000. Lakini kwa lengo la kuwafanya wadau wa kiingilio hicho kuchangia gharama za mechi hiyo sasa kutakuwa na viingilio vitatu tofauti katika viti vya VIP.

Kwa VIP A ambayo ina viti 748 kiingilio kitakuwa sh. 10,000, VIP B inayochukua watazamaji 4,160 kiingilio ni sh. 5,000 wakati VIP C yenye viti 4,060 kiingilio ni sh. 2,000. Kwa sehemu nyingine (viti vya rangi ya chungwa, kijani na bluu) ambavyo jumla yake ni 48,590 kiingilio kitabaki kuwa sh. 1,000.

Timu ya Congo Brazzaville kwa taarifa tulizopata awali kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu la Congo (FCF) ilikuwa iwasili jana (Novemba 13 mwaka huu) usiku. Lakini timu hiyo haikutokea na sasa tunatarajia itawasili leo (Novemba 14 mwaka huu) saa 8 mchana kwa ndege ya Ethiopian Airlines. Congo itafikia Sapphire Court Hotel.

KAMPUNI YA Darworld Links imeandaa mpambano mwingine wa ubingwa wa masumbwi utakaowakutanisha bondia Nassibu Ramadhani na Fransic Miyayusho, mpambano huo utakaofanyika katika Ukumbi wa PTA Sabasaba,

Aakizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Mohamed Bawazir,amesema  kuwa amewakutanisha mabondia hao kutaka kujua nani zaidi ya mwenzake kwa kuwa viwango vyao vina fanana na vinatambulika kimataifa hivyo amewataka watanzania kujitokeza kuwapa sapoti hususani kudhamini wa mchezo huo wa masumbwi.

Udhamini tunapoomba sehemu ya makampuni mbalimbali ukienda wanasema atuhusiki na mchezo huo,Wengine wanasema kabisa wadhamini wa michezo wakati wanabagua michezo mingine kama ngumi awapewi kipaumbele kabisaa

amewaomba wapenzi na mashabiki kujitokeza siku ta 9 Desemba kuja kuangalia ngumi ili zisonge mbele watakaosindikiza mpambano huo wa masumbwi ni Fadhili Majia VS Juma Fundi Moh'd Rashid Matumla VS Doi Miyayusho Ibrahimu Class 'King Class Mawe' VS Said Mundi wa Tanga
Fred Sayuni VS Deo Samweli Hassani Kidebe VS Baina Mazola

Mapambano yote ya utangulizi ni mazuri na vijana wanaotakiwa kuendelezwa katika elimu ya masumbwi Duniani ili wawe mabondia wazuri.