TRANSLATE THIS BLOG

Tuesday, April 7, 2015


LEO Mabingwa na Vinara wa Serie A huko Italy, Juventus, wana kibarua kigumu cha kugeuza kipigo walichopewa Nyumbani kwao na Fiorentina kwenye Nusu Fainali ya Coppa Italia.

Katika Mechi ya kwanza iliyochezwa huko Juventus Stadium, Fiorentina waliichapa Juve Bao 2-1 na Leo Fiorentina wako kwao Stadio Artemio Franchi kulinda ushindi huo ili watinge Fainali.

Mechi nyingine ya Marudiano ya Nusu Fainali itachezwa kesho Jumatapo huko Stadio San Paolo kati ya Napoli na Lazio ambazo zilitoka 1-1 katika Mechi ya kwanza.

Tayari Marefa wa Mechi hizi wameshatangazwa na Davide Massa atachezesha Fiorentina v Juventus na Daniele Orsato ile ya Napoli v Lazio.


Italy - Coppa Italia
April 7
21:45 Fiorentina ? - ? Juventus

kwa mechi za leo za ligi mbalimbali tembelea http://www.livescore.com/

No comments:

Post a Comment