TRANSLATE THIS BLOG

Tuesday, April 7, 2015


DFB-POKAL: LEO DORTMUND KUWANIA KUINGIA NUSU FAINALI!

Klabu 7 za Bundesliga na moja ya Daraja la 3, Arminia Bielefeld, Leo na Jumatano zitawania Nafasi 4 za kuingia Nusu Fainali ya Kombe la Ujerumani, DFB-Pokal.

Miongoni mwa hizo 7 za Bundesliga, 4 zipo kwenye 4 Bora, na pia ipo Borussia Dortmund ambayo Msimu huu inasuasua na ipo Nafasi ya 10.

Kwa Dortmund, ambao Leo watacheza kwao Signal Iduna Park na Hoffenheim, hii ndio nafasi yao pekee iliyobaki Msimu huu kutwaa Taji na Kocha wao, Jurgen Klopp, amesisitiza hilo.

Mabingwa Watetezi wa DFB-Pokal Bayern Munich wana Mechi ngumu ya Ugenini Jumatano dhidi ya Timu iliyo Nafasi ya 4 kwenye Bundesliga, Bayer Leverkusen lakini hilo halikumkatisha tamaa Kiungo wao kutoka Spain, Xabi Alonso, ambae ameshawahi kutwaa Vikombe huko kwao Spain na England na safari hii anataka cha Nchini Germany ambacho kwa Bayern itakuwa DFB-Pokal yao ya 3 mfululizo.

Katika Mechi nyingine za Robo Fainali, Leo Wolfsburg watakuwa Wenyeji wa Freiburg wakati Arminia Bielefeld, Timu ya Daraja la 3 iliyozibwaga katika Raundi zilizopita Klabu za Bundesliga Hertha Berlin na Werder Bremen, itakuwa Nyumbani kucheza na Borussia Monchengladbach hapo Jumatano.

DFB-Pokal

Robo Fainali;Jumanne Aprili 7
20;00 Wolfsburg v SC Freiburg

21;30 Borussia Dortmund v Hoffenheim
Jumatano Aprili 8

20;00 Arminia Bielefeld v Borussia Mönchengladbach
 21;30 Bayer Leverkusen v Bayern Munich

No comments:

Post a Comment