TRANSLATE THIS BLOG

Tuesday, April 7, 2015


TENGA AULA TENA CAF


MWENYEKITI wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Leodegar Tenga amerejea katika nafasi yake ya Ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shiriksiho la Soka Afrika (CAF) baada ya uchaguzi uliokwenda sambamba na Mkutano Mkuu mjini Cairo, Misri Aprili 6 na 7 mwaka huu.

Tenga, Rais wa zamani wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), sasa ataitumikia nafasi hiyo kwa miaka mingine minne kama Mkuu wa ukanda wa CECAFA
(Rais wa FIFA Sepp Blatter akiwa na Leodegar Chilla Tenga walipokutana hivi karibuni makao makuu ya FIFA jijini Zurich)
Taarifa ya Katibu Mkuu wa CECAFA , Nicholas Musonye leo, imesema kwamba Mkutano Mkuu wa CAF ambao hufanyika kila mwaka, ulianza Jumatatu mjini Cairo na nchi zote 54 wanachama zikiwemo 12 za CECAFA zilihudhuria.

Wanachama wa CECAFA ni Burundi, Kenya, Uganda, Tanzania, Somalia, Djibouti, Eritrea, Ethiopia, Zanzibar, Rwanda, Sudan na Sudan Kusini.

Tenga alichaguliwa bila kipingamizi, baada ya aliyekuwa mpinzani wake, Hassan Suleiman wa Djibouti kujitoa na kumsapoti Nahodha huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars.


No comments:

Post a Comment