TRANSLATE THIS BLOG

Monday, January 7, 2013


Wakala: Lampard lazima aondoke Chelsea.
 
Imethibitika kuwa Frank Lampard ataihama Chelsea mwishoni mwa msimu huu, kwa mujibu wa wakala wake Steve Kutner.
 
Akikaririwa na magazeti ya nchini Uingereza akisema,
"watendaji wa Chelsea walimwambia Frank kule Japan wakati wa michuano ya kombe la dunia la vilabu na hata mara baada ya ushindi dhidi ya Everton mwezi uliopita kuwa hakuna chochote kitakacho pelekea klabu kumpa ofa nyingine Lampard baada ya msimu huu"
 
"hakuna kitakacho badilika kwa vyovyote vile. Frank anapashwa kukubaliana na hayo inabidi ajikusanye kumalizia msimu kwa mafanikio katika klabu ambayo aliipenda sana."
 
Lampard alipata nguvu mpya kutokana na kushangiliwa na mashabiki wa Chelsea katika mchezo wa mzunguko wa tatu wa michuano ya FA dhidi ya Southampton jumamosi pale alipofunga goli ambalo kimsingi lilimfanya kuwa sawa na mchezaji wa zamani klabu hiyo Kerry Dixon mwenye rekodi ya juu ya ufungaji magoli, lakini inaonekana sherehe ya ushangiliaji baada ya kufunga goli akiwa katika jezi yake maarufu namba 8 mgongoni inaelekea ukingoni.
 
Mashabiki wa Chelsea wamekuwa wakitaka Lampard apewe mkataba mwingine lakini hali inavyo onekana ni kuwa hakuna nafasi nyingine ya kuendelea kusalia Stamford Bridge.
Mwenyewe Lampard amekaririwa akisema
"pengine sikuwa na mvuto wa kutosha lakini mashabiki wamekuwa na mimi katika kipindi chote ambacho tumekuwa pamoja hapa"

No comments:

Post a Comment