TRANSLATE THIS BLOG

Monday, February 25, 2013

HABARI FUPI FUPI NA HARAKATI ZA USAJILI

Klabu ya Newcastle inamtaka winga mfaransa Hatem Ben Arfa kusaini mkataba mpya na kuendelea kusalia St James' Park,na hii ni baada ya Liverpool kuanza kumtolea macho kijana huyo mwenye miaka 25.

---------------------------------
Meneja wa majogoo wa jiji Liverpool Brendan Rodgers alifunga safari mpaka Holland kumshuhudia nahodha wa Feyenoord anaecheza beki ya kati Stefan De Vrij(21 yrs),katika mchezo wa ligi ya uholanzi iliyopigwa jumapili ambapo Feyenoord iliibuka na ushindi wa 2-1 mbele ya PSV Eindhoven. Rodgers amekuwa akisaka beki kwaajili kuziba nafasi ya Jamie Carragher ambae amestaafu soka.
----------------------------------
Kiungo wa Southampton Gaston Ramirez, 22yrs,anawindwa na vilabu vinavyoshiriki ligi kuu ya Italia seria A,vinara Juventus,Inter Milan na Fiorentina.
----------------------------------
Boss wa West Ham Sam Allardyce huwenda akamuongeza katika kikosi chake beki wa zamani wa Bolton Ricardo Gardner.mchezaji huyo wa kimataifa toka Jamaica ,34yrs,kwa sasa ni mchezaji huru baada ya kuondoka Reebok Stadium akiwa mchezaji huru msimu uliopita.
-----------------------------------
Mshambuliaji wa mashetani wekundu Manchester United Robin van Persie atakuwa fit kuikabili Real Madrid wiki ijayo katika klabu bingwa barani ulaya baada ya kuumia katika mchezo dhidi ya Queens Park Rangers.

 

lakini taarifa iliyopo nikwamba Van Persie ataukosa mchezo wa jumamosi katika dimba la nyumbani Old Trafford watakapo wakaribisha nyumbani Norwich City.
-----------------------------------
Meneja wa Celtic Neil Lennon ameitaka klabu yake kumpatia kandarasi mpya kiungo wa timu hiyo mwenye umri wa miaka 26 Joe Ledley.
------------------------------------
AND FINALLY

Klabu toka Italia Palermo imemfukuza kazi manager wao Alberto Malesani baada ya wiki tatu tu katika kazi yake,nafasi yake amepewa Gian Piero Gasperini - the man Malesani replaced.

 Full story: La Gazzetta dello Sport 

No comments:

Post a Comment