TRANSLATE THIS BLOG

Monday, February 25, 2013

   KUELEKEA DABY YA  LONDON KASKAZIN

Beki wa washika bunduki wa london Arsenal Per Mertesacker amesema kiungo wa timu hiyo says Santi Cazorla ni mtandaza soka hasa na hii ni baada ya muhispania huyo kutupia nyavuni mara mbili katika ushindi walioupata jumamosi iliyopita wa magoli 2-1 dhidi ya Aston Villa.

 

Cazorla alikuwa katika kiwango chake kwa mara nyingine tena na jumamosi hii Gunners watakuwa ugenini katika dimba la White Hart Lane kuwakabili wenyeji wao spurs katika ile derby ya london ya kaskazin na Mertesacker anamatumaini na kiungo wake huyo kuendelea kufanya vizuri..
------------------------

WILSHARE;BADO TUNAWEZA

Tukiendelea kusalia London kunako vijana wa ARSHBATON,Kiungo  Jack Wilshere amewataka wechezaji wenzake kuendelea kufanya vyema na kuhakikisha hawashuki kiwango kwani msimu bado haujafika mwisho wanayo nafasi ya kufanya vyema na kuwapiku wapinzani wao katika ligi na hata kukamata nafasi mbili za juu....

Katika upande wa klabu bingwa barani ulaya,Arsenal inaonekana kuwa na nafasi finyu ya kusonga mbele  baada ya kukubali kichapo cha goli 3-1 toka kwa Bayern Munich katika uwanja wa nyumbani na mwezi ujao Arsenal itasafiri mpaka Munich katika dimba la Arena kuikabili Bayern.
-------------------------------------------------
BALE;SPURS ZAIDI

Wakati huo huo kutoka london ya kaskazini,Gareth Bale anaamini kwa sasa Tottenham iko vizuri (ni bora) zaidi ya  Arsenal katika kuwania nafasi nne za juu ambazo zinakuwezesha kucheza Champions League.

No comments:

Post a Comment