TRANSLATE THIS BLOG

Wednesday, July 24, 2013

Sevilla wamsajili Gameiro wa PSG

Timu ya Sevilla imefanikiwa kumsajili striker Kevin Gameiro kutoka mabingwa wa ufaransa msimu uliopita Paris Saint-Germain,klabu hiyo toka hispania imethibitisha hayo leo jumatano.
kwa mujibu wa vyombo vya habari ,Sevilla watalipa kiasi cha yuro euro 10mil ambazo nisawa na  (13.2 million dollars) kwaajili ya saini ya mchezaji huyo mwenye miaka 26.

Sevilla,ambao msimu uliokwisha walimaliza ligi spain LA LIGA wakiwa nafasi ya tisa,wanatizamia sasa kukiimarisha kikosi chao hasa safu ya mbele tangu kufuatiwa kuuzwa kwa strikers wao Alvaro Negredo na Jesus Navas kwa vijana wa ligi kuu uingereza  Manchester City.

Klabu ya Sevilla imetangaza kuwa wamemtoa kwa mkopo beki wao Alberto Botia kwa timu ya  Elche ili       kupata nafasi ya kucheza zaidi.

No comments:

Post a Comment