MSHINDANO ya baiskeli
yajulikanayo kama Tour de France yamefikia tamati jana kwa Chris Froome
wa Uingereza kutawadhwa bingwa mpya wa mashindano ambayo ni ya 100 toka
kuanzishwa kwake.
Akishinda
taji hilo kwa zaidi ya dakika nne, Froome alishikana mikono na na
wenzake wa timu ya Sky wakati akikatisha katika msitari wa ushindi
jijini Paris, Ufaransa.
Huo
unakuwa ushindi wa pili kwa Uingereza kwenye michuano hiyo baada ya
mwendesha baiskeli Sir Bradley Wiggins ambaye naye anatoka katika timu
ya Sky kushinda michuano hiyo mwaka jana. Mashindano
yalishirikisha waendesha baiskeli kutoka nchi mbalimbali ambapo
waliendesha baiskeli kwa kilometa 3,200 katika miji mbalimbali ya ya
Ufaransa katika kipindi cha wiki mbili cha mashindano hayo.
No comments:
Post a Comment