TRANSLATE THIS BLOG

Monday, July 22, 2013

Taifa Stars kwenda Kampala Jumatano


Timu ya Taifa ya Tanzania itaondoka Mwanza Jumatano kwenda Kampala, Uganda kwa ajili ya mechi ya marudiano ya Kombe la CHAN itakayochezwa Jumamosi katika Uwanja wa Mandela kuanzia saa kumi kamili jioni. 

Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager iko kambini jijini Mwanza chini ya Kocha Kim Poulsen tangu Julai 14 mwaka huu kujiandaa kwa mechi hiyo itakayoamua ni timu ipi kati ya hizo mbili itacheza Fainali za CHAN zitakazofanyika mwakani nchini Afrika Kusini.
Timu hiyo itaondoka Uwanja wa Ndege wa Mwanza saa 7.25 mchana kwa ndege ya PrecisionAir, na inatarajiwa kutua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Entebbe saa 10.15 jioni.
Wakati huo huo, Kocha Kim Poulsen atakuwa na mkutano na waandishi wa habari kuzungumzia maandalizi ya kikosi chake Jumanne.

No comments:

Post a Comment