TRANSLATE THIS BLOG

Wednesday, July 24, 2013

HIGUAIN KWENDA NAPOLI...arsenal hoi!!!


MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Argentina na klabu ya Real Madrid, Gonzalo Higuain inasemekana amekamilisha usajili wake kwenda Napoli ya Italia kwa mujibu ya magazeti ya nchini Hispania.

 Gazeti la AS na Marca ya nchi hiyo lilidai kuwa Napoli wamelipa kiasi cha euro 37(Ambazo ni sawa na dollar za kimarekani 48.8mil) kwa ajili saini ya nyota huyo mwenye umri wa miaka 25.

 Kama mpango huo ukikamilika Higuain atakuwa mchezaji wa tatu wa Madrid kuuzwa Napoli katika kipindi hiki cha uasajili majira ya kiangazi baada ya Raul Albiol na Jose Callejon kuwa tayari wameuzwa.

Kumbuka Napoli kwa sasa inaongozwa na Mhispania Rafa Benitez.

 Kwa mujibu wa taarifa za gazeti hilo pesa zitakazopatikana kwa mauzo ya Higuain zitatumika katika kutafuta saini za Gareth Bale wa tottenham na Luis Suarez wa Liverpool...

Kwa msisitizo!!!!!!!!...
According to media reports, Real will use the money for Higuain to bid for Gareth Bale of Tottenham and Luis Suarez of Liverpool.

No comments:

Post a Comment