TRANSLATE THIS BLOG

Friday, November 16, 2012


Kuelekea mchezo wa jumapili baina ya timu ya soka ya vijana ya Tanzania bara Serengeti Boys dhidi ya timu ya vijana ya Congo Brazzaville utakaopigwa uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam,  kocha msaidizi wa Serengeti Boys Jamhuri Kihwelu 'Julio' amesema wataingia katika mchezo huo wakiwa na rufaa mkononi kutokana na kile alichokieleza kuwa wachezaji wengi wa Congo wanaonekana kama wana umri mkubwa.

Julio amesema amepata nafasi ya kuwaona wachezaji hao asubuhi ya leo wakati wakifanya mazoezi na ushahidi wa machoni unaonyesha wazi kuwa wachezaji hao wengiwao si chini ya umri wa miaka 17.

Julio amesema anaimani kuwa wachezaji waliopimwa vipimo vya umri na shirikisho la soka barani Afrika CAF kwa siyo hao walikokuja nchini. 

Jana Rockersports ilikuwa ikiongea na kocha Jacob Michelsen kuhusiana na wasiwasi wa kucheza na wachezaji vijeba ambao wengine walishiriki kombe la dunia mwaka jana na kutolewa katika hatua ya 16 bora na Uruguay, kimsingi amesema hilo analiacha kwa shirikisho la soka TFF.

Sasa Rockersports imejaribu kuperuzi mtandao wa shirikisho la soka duniani fifa ambapo imebaini wachezaji ambao ni zaidi ya umri wa miaka 17. 

Katika kikosi kilichoshiriki kombe la dunia kwa vijana nchini Mexico kuna wachezaji 8ambao wana umri zaidi ya miaka 17 ambao wamezaliwa si zaidi mwezi oktoba mwaka 1994 ambao kimsingi wamezidi umri wa miaka 17

No comments:

Post a Comment