TRANSLATE THIS BLOG

Friday, November 16, 2012


Terry nje kwa wiki tatu 

Meneja wa Chelsea Roberto Di Matteo amethibitisha kuwa John Terry atakuwa nje ya uwanja kwa takribani wiki tatu kufuatia kuwa majeruhi wa mguu.

Kuna wasiwasi kuwa huenda mlinzi huyo wa kati akaendelea kuwa nje kwa kipindi kirefu zaidi kutokana na kuwepo taarifa kuwa mguu wake ambao aligongana na mshambuliaji wa Liverpool Luis Suarez katika mchezo wa jumapili uliomalizika kwa sare ya bao 1-1, kupinda kidogo.

Mlinzi huyo wa kimataifa wa England alionekana akigumia kwa nguvu kutokana na maumivu na kisha kutolewa nje kwa kutumia machela katika dimba la Stamford Bridge ambapo kipimo cha 'MRI scans' hapo kabla kikonyesha alipatwa na madhara kidogo katika mshipa wa mguu.

Hata hivyo bosi wa ‘The Blues' Di Mateo ametanabaisha kuwa mlinzi huyo mwenye umri wa miaka 31 atakosekana kwa wiki tatu jambo ambapo amesema ni pigo kwa kikosi chake.

No comments:

Post a Comment