TRANSLATE THIS BLOG

Friday, November 16, 2012




Uongozi wa klabu bingwa Tanzania Bara Simba ya mtaa wa Msimbazi umeamua kufutilia mbali kamati zake zote kwa lengo la kujipanga upya kwa ajili ya ligi kuu ya soka Tanzania Bara pamoja na michuano klabu bingwa barani Afrika.

Kauli ya kuvunja kamati hizo imetolewa na mwenyekiti wa klabu hiyo  alhaji Ismail Aden Rage(mbunge) katika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika katika makao makuu ya klabu hiyo Kariakoo mtaa wa Msimbazi  jijini Dar es Salaam.

Rage ambaye hata hivyo hakutaja ni lini kamati mpya zitaundwa, pia amekiri kuwa matokeo ya michezo ya mwisho ya timu yao hayakuwa mazuri kiasi cha kuwasikitisha wanachama na wapenzi  wa  klabu yao.

 Amesema mfululizo wa kuendelea kuharibu kulitokana na wachezaji wa timu hiyo kuharibikiwa kisaikolojia na kwamba ili kuhakikisha hali hiyo inaondoka katika vichwa vya wameamua kuitoa timu yao nje ya nchi katika kujaribu kuwarejesha mashindanoni ambapo ameahidi kutanga nchi hiyo baadaye.

Amewataka wanachama na wapenzi wa Simba kufahamu kuwa katika kipindi hiki ligi ya Tanzania bara imekuwa katika ushindani mkubwa hivyo ni vema wakawa wavumilivu na hali hiyo tofauti na ilivyoljitokeza katika siku za hivi karibuni ambapo kikundi cha wanachama kimoja kiliibuka na kutaka kuhatarisha hali ya amani ya klabu yao.

Pia Rage ametangaza kulifuta tawi la Simba la Mpira pesa ambalo uongozi wa Simba umesema lilichochea vurugu za hivi karibuni ambapo pia Rage ametangaza kumfuta uanachama mwenyekiti wake Masoud Awadhi kwa kuitisha kikao batili cha wanachama pia kutokana na kutokulipa ada ya uanachama kwa miaka mitatu.

Novemba 5 kuliibuka tafrani katika makao makuu ya klabu hiyo ambapo wanachama wa tawi la mpira pesa na baadhi ya wapenzi wa timu waliutaka uongozi wa juu wa klabu hiyo kuondoka na kuwaachia simba yao.

Mbango yalisomekam "Kaburu na Kaseja ondokeni tuachieni Simba yetu" jambo lilionekana kama vurugu zimeanza msimbazi lakini jitihada za msemaji wa klabu hiyo Ezekiel Kamwaga kuwatuliza wanachama zilizaa matunda kwa kujibu hoja mbalimbali za wanachama zilizoibuka kupitia vyombo vya habari.

No comments:

Post a Comment