TRANSLATE THIS BLOG

Wednesday, November 14, 2012


Wilfried Bony kujiunga na Chelsea Januari.

Mshambuliaji wa Vitesse Wilfried Bony amekaribisha tetesi juu ya klabu ya Chelsea kutaka huduma yake katika kipindi cha uhamisho cha mwezi January.

Bony mwenye umri wa miaka 23, amekuwa katika kiwango huko Eredivisie tangu kuihama klabu yake ya zamani ya Sparta Prague mwezi January 2011, akiwa amesha pachika wavuni jumla ya mabao 12 baada ya kushuka dimbani mara 11 katika msimu huu.

Mapema mwezi huu wakala wa mchezaji huyo Francis Kacou alinukuliwa akisema,
"kuna vilabu kadhaa vya ligi kuu nchini England vimeonyesha nia ikiwemo Chelsea na Aston Villa"
Katika mahojiano yake na jarida moja la nchini Czech la  Pravo, nyota huyo wa kimataifa wa Ivory Coast alithibitisha kuwa angependelea kuelekea Stamford Bridge.

"sitaki kuongea mengi kuhusu hilo lakini kama imeandikwa kuwa nakwenda huko basi ni kitu kizuri"
 "kama wananitaka nitakuwa ni heshima kubwa. Napenda kujiunga na klabu kama hiyo, napenda soka na England na siogopi kwenda huko. Chelsea ni klabu kubwa"

Mkurugenzi wa michezo wa Chelsea Michael Emenalo hivi karibini alielekea Arnhem kuangalia mchezo baina ya  Vitesse dhidi ya FC Twente ambao ulimalizika kwa sare ya 0-0.

No comments:

Post a Comment