TRANSLATE THIS BLOG

Friday, November 16, 2012


ROONEY;NITAIVUNJA RIKODI YA SIR CHARLTON 

Wayne Rooney amedhamiria kuivunja rekodi ya ufungaji iliyowekwa na Sir Bobby Charlton katika klabu ya Manchester United na timu ya taifa ya England.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27 kwasasa yuko katika nafasi ya nne ya wafungaji bora waliowahi kupita United akiwa ameshafumania nyavu mara 185 ambayo ni pungufu ya mabao 64 ya Charlton ambaye anaendelea kushikilia rekodi ya ufungaji ya klabu hiyo ya mabao 249.

Katika timu ya taifa ya England ‘Three Lions Rooney’ Rooney amefunga jumla ya magoli 32 ambayo ni pungufu mabao 17 kufikia rekodi ya Charlton ya mabao 49.

Amekaririwa Rooney akisema
"Sir Bobby anashikilia rekodi zote mbili,  hii ni changamoto kubwa sana, jamaa ni mwasisi katika klabu kwahiyo ni kama mtu ambaye anaendelea kuwepo katika klabu, kama nitafanikiwa kuvunja rekodi yake ya ufungaji bora katika klabu na hata katika timu ya taifa hilo litakuwa ji jambo la kupendeza."

Rooney pia anataka kucheza soka katika kipindi kirefu zaidi kama ilivyo kwa Ryan Giggs na Paul Scholes wachezaji ambao wanamvutia kwa kuendelea kuwepo kwa zaidi ya muongo mmoja.

No comments:

Post a Comment