TRANSLATE THIS BLOG

Friday, November 16, 2012


Dante: Nimekuja Bayern kusaka mataji na si kuuza sura


Mlinzi wa kati wa Bayern Munich Dante amesema waziwazi kuwa kilichomshawishi kujiunga na klabu hiyo si kingine isipokuwa anahitaji kushinda mataji.

Mlinzi huyo wa zamani wa Borussia Monchengladbach alijiunga na Bavaria kwa ada ya euro million 4.7 katika kipindi cha uhamisho wa kiangazi baada ya kuipa mafanikio Gladbach katika msimu wa 2011-12 ambapo ilimaliza katika nafasi ya nne katika msimamo wa ligi ngumu kabisa ya nchini Ujerumani ‘Bundesliga’.

Akiwa hajawahi kushinda taji lolote kubwa katika soka , mlinzi huyo mwenye umri wa miaka 29 anafikiria ndoto yake itatimia kwa kujiunga na kikosi cha kocha Jupp Heynckes.
-------------------------------------------------------------------

Wakati huo huo.......

Msemaji wa Kiungo na nahodha wa zamani wa England David Beckham amekanusha taarifa kuwa mchezaji huyo ana mpango wa kuihama klabu yake ya LA Galaxy na kuelekea nchini Australia baada ya shirikisho la soka nchini Australia (FFA) kudai kuwa kiungo huyo ambaye kwasasa ana umri wa miaka 37 alikuwa anaitamani ligi kuu ya soka ya nchi hiyo ya A-League.

Msemaji wa FFA amedokeza kuwa mchezaji huyo wa zamani wa Manchester United alikuwa katika mpango wa kufuata nyayo za akina Alessandro Del Piero na Emile Heskey na kujiunga na soka la Australia.

Taarifa kupitia msemaji wa FFA ambazo zilionyesha ni kama kuifagilia ligi ya Australia imesomeka
"kuja kwa David Beckham ni ishara kuwa hadhi ya ligi yetu ya Hyundai A-League imekuwa duniani.

"Beckham ni nyota mkubwa sana duniani na atakuwa mtu mwingine mkubwa katika soka kujiunga na Hyundai A-League baada ya kuja kwa Alessandro Del Piero, Emile Heskey na Shinji Ono. Lakini kwasasa ujio wake bado uko katika hatua za awali"

Hata hivyo msemaji wa Beckham amekanusha taarifa hizo akisema mchezaji huyo kwasasa ana furahia maisha katika jiji la Los Angeles na hana mpango wa kuondoka.

No comments:

Post a Comment