TRANSLATE THIS BLOG

Wednesday, November 14, 2012


Santos imethibitisha kumtaka Robinho.

Kocha wa Santos Muricy Ramalho ameweka wazi kuwa klabu yake ina matumaini makubwa ya kumrejesha mshambuliaji wa AC Milan Robinho katika uhamisho wa mwezi Januari.

Taarifa kutoka nchini Brazil zimedai Robinho, Nene, Pablo Aimar na Diego ni miongoni mwa wachezaji walio katika orodha ya kocha Ramalho kwa ajili ya msimu ujao wakati ambapo kuna tetesi kuwa huenda klabu hiyo ikampoteza mshambuliaji wake hodari Felipe Anderson.

Mapema wiki hii alikaririwa mwanasheria wa Robinho Marisa Alija akisema Robinho ana matumaini ya kurudi Santos, lakini alikataa kusema itakuwa lini.

"tunasikia mengi juu ya Robinho lakini tukumbuke ana mkataba na Milan mpaka 2014,"
 "hajaniambia chochote juu ya kurejea Santos msimu ujao. Lakini anashindwa kuficha juu ya nia yake ya kurejea lakini katika hatua hii sidhani kama itawezekana."
-------------------------------------------------------------------

NA.....

Mshambuliaji wa kimataifa wa Sweden Zlatan Ibrahimovic anaamini wakati umefika sasa kwa kiungo mzoefu wa Liverpool Steven Gerrard kuondoka katika soka na England na kujiunga na vilabu vingine vikubwa nje ya nchi yake.

Ibrahimovic ametoka maoni yake hayo wakati huu ambapo Sweden inaelekea kucheza na timu ya taifa ya England maarufu kama Simba watatu mjini Stockholm ukiwa ni mchezo wa kimataifa wa kirafiki.

Muda mfupi baada ya mchezo wao akiwa na klabu yake ya Paris Saint-Germain dhidi ya Liverpool Zlatan alionyesha wazi kumkubali Gerrard, lakini akasema ni muda muafaka kwa Skipper huyo kuondoka Premier League.

"nadhani Steven Gerrard anaheshimika kote barani ulaya,  nafahamu hilo kwasababu mara nyingi kocha huwa anasema kuwa muangalifu na Gerrard kwasababu ndiyo mchezaji anaye leta utofauti uwanjani.

"lakini licha ya Liverpool kuwa klabu kubwa Ulaya, ningependa kumuona Steven katika klabu nyingine kubwa Ulaya.
"kwangu mimi mchezaji mzuri ni yule anaye onyesha utofauti kila sehemu. Nina uhakika Steven Gerrard anaweza."
--------------------------------------------------------------------------

leo ni mechi za kimataifa za kirafiki!!!!!...


No comments:

Post a Comment