TRANSLATE THIS BLOG

Monday, August 20, 2012

Jumatatu, 20 Agosti 2012 13:52

Malawi na Tanzania kukutana leo kujadili mzozo wa mpaka

Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania na Malawi wanakutana leo katika mji wa Mzuzu, ulioko kaskazini mwa Malawi  kwa shabaha ya kujadiliana juu ya mzozo wa nusu karne wa mpaka baina ya nchi mbili hizo.
 
 Hivi karibuni Tanzania na Malawi zilitumbukia katika malumbano makubwa ya mpaka ambayo yalikaribia kuzitumbukiza nchi hizo katika vita.
 
Hata hivyo mazungumzo ya hivi karibuni baina ya Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania na Bi Joyce Banda wa Malawi huko Maputo Msumbiji yalipunguza kidogo hitilafu hizo baada ya viongozi hao kusisitiza juu ya kutatuliwa hitilafu hizo kwa njia za kidiplomasia.
 Mgogoro huo, unalihusu Ziwa Nyasa, ambalo linatambulika nchini Malawi kwa jina la Ziwa Malawi  na ambalo tayari serikali ya Lilongwe imeshatoa leseni za utafutaji mafuta kwa kampuni moja ya  Uingereza.
 

No comments:

Post a Comment