TRANSLATE THIS BLOG

Monday, August 20, 2012


Song Atua Barca rasmi!!!


kingo wa washika bunduki wa london Arsenal Alex Song amefaulu vipimo vya afya na kusaini  mkataba wa miaka mitano na klabu ya Barcelona yenye maskani yake Camp Nou.

Song, 24, ameyakamilisha hayo leo mchana baada ya kuhusishwa kutaka kuhamia moja ya klabu bingwa barani ulaya Barcelona .

katika mtandao wa klabu hiyo daktari wa klabu  Ricard Pruna amesema Song yuko vizuri  kiafya na yuko very good muscular quality. na hadhani kama alishapata muscle injury tangu akiwa na umri wa miaka  17 . Na hiyo ni habari njema,kila vipimo vimekwenda vizuri.

king huyo wa kimataifa wa Cameroon alikuwa Emirates Stadium tangu 2005, inaaminika amejiunga na wakali hao wa hispania kwa ada ya €19 million.

usajili wa Alex song Barca ni moja ya mikakati Tito Vilanova kukiimarisha kikosi chake.

kuondoka kwa Song kumefungua njia kwa Arsenal kuweza kushinda mbio za usajili wa mkopo wa Nuri Sahin kutoka Real Madrid.

No comments:

Post a Comment