TRANSLATE THIS BLOG

Friday, August 17, 2012

TANGA EID HAPATOSHI KTK UKUMBI ULIOJIZOLEA UMAARUFU MKUBWA...(PWEZA CLUB)

siku ya idi pili katika ukumbi wa pweza kutakuwa na pambano kubwa la ubingwa wa Afrika mashariki na kati, kati ya Alen Kamote wa Tanga na bondia toka Uganda ni pambano la raundi kumi.

zuberi kitandula wa Tanga atazipiga na Sadiki Abdul azizi wa Dar es salaam raundi kumi,jay jay ngotiko wa tanga atapigana na bondia juma afande toka morogoro .

Pia kutakuwepo na mapambano mengi ya utangulizi ya mabondia wakongwe wa tanga na wale chipukizi takribani mabondia wote wa kulipwa wa jiji la Tanga watashindana hakuna atakaekosa kazi labda awe na matatizo binafsi. 

mwazoa alimalizia kwa kusema hizi ni mbio za kuyakusanya mataji yote ya Tanzania na Afrika mashariki yaje mkoani Tanga na tayari mpaka sasa ina mabingwa sita wa Tanzania na mmoja wa Afrika mashariki.

No comments:

Post a Comment