TRANSLATE THIS BLOG

Friday, August 17, 2012


Tanga.
JESHI la Polisi Mkoani Tanga kwa kushirikiana na Dawati la Jinsia na watoto limetoa msaada, Mchele,Mbuzi, Sabuni,Mafuta ya kula na Pipi katika vituo viwili vya kulelea watoto yatima vilivyopo mkoani hapa.

Vituo ambavyo vimepatiwa msaada huo ni kituo cha Abu Abdaramani na kikundi cha wavitima kilichopo Duga jijini hapa ambapo msaada huo ulikabidhiwa leo katika ofisi ya Kamanada wa Polisi.

Akizungumza wakati akikabidhi vifaa hivyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Constatine Massawe amesema jeshi la polisi mkoa wa Tanga wameona washiriki na watoto wanaolelewa na dawati hilo katika kipindi hiki cha sikukukuu ya Iddi.

Massawe ametoa wito kwa jamii kuangalia vituo vya kulelea watoto vilivyopo mkonoa hapa kwa jicho la huruma kwa kutoa misaada ya hali na mali ambayo itawawezesha watoto hao kujisikia nao wapo na wanapendwa na jamii zinazowazunguka.

Akizungumza baada ya kupokea msaada huo, Mwakilishi wa Kituo cha Makorora kiitwacho Abu Abduraman amshukuru Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga kwa jitihada walizoanzisha za kuwasaidia watoto wanaoishi katika vituo vya kulelea yatima jijini hapa.

Wakati huo huo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Costantine Massawe amesema jeshi hilo limejipanga vilivyo ili kuweza kuhakikisha wanahimarisha ulinzi katika maeneo mbalimbali ili kuweza kuwapa fursa watu kuadhimisha sikukuu ya idi kwa amani.

Massawe ametoa wito kwa wale wote wanaendesha vyombo vya moto kuacha kuendesha huku wakiwa wamelewa kwani kufanya hivyo ni kukiuka taratibu na hupeleka kusababisha ajali ambapo ameongeza kuwa jeshi hilo halitawavumilia wale wote wenye tabia za kuendesha huku wakiwa wamelewa.

Mwisho.....
-----------------------------------------------------

No comments:

Post a Comment