leo katika historia!!!!!!!!!!!Agosti 20
Leo ni Jumatatu tarehe Pili Mfunguo Mosi Shawaal mwaka 1433 Hijiria
inayosadifiana na tarehe 20 Agosti mwaka 2012 Miladia
Siku kama ya leo miaka 14 iliyopita, yaani Agosti 20 mwaka 1998 Marekani
ilizishambulia kwa makombora Sudan na Afghanistan. Serikali ya
Washington ilidai kwamba, watu walioshiriki katika kulipua kwa mabomu
balozi za Marekani mjini Dar es Salaam Tanzania na Nairobi Kenya wiki
mbili kabla, walikuwa na uhusiano na nchi hizo. Aidha Washington ilisema
ilikishambulia kwa mabomu kiwanda cha kuzalisha madawa cha ash-Shifaa
nchini Sudan kwa madai kwamba kilikuwa kikitengeneza mada za kemikali.
Hata hivyo weledi wa masuala ya kisiasa walisema kwamba, sababu ya
Marekani kufanya mashambulio ya mabomu dhidi ya Sudan na Afghanistan
ilikuwa ni kujaribu kufunika fedheha ya kimaadili iliyokuwa ikimkabili
rais wa nchi hiyo Bill Clinton. Kwa ajili hiyo mashambulizi hayo
yaliamsha hasira za fikra za walio wengi na serikali nyingi duniani
dhidi ya siasa za kutumia mabavu na kujichukulia maamuzi ya upande mmoja
za Marekani.
Siku kama ya leo miaka 849 iliyopita muwafaka na tarehe Pili Shawwal
mwaka 584 Hijiria, alifariki dunia Ibun Ta'awidhi mshairi na mwanafasihi
wa Baghdad. Alizaliwa mwaka 519 Hijiria na ujanani mwake aliwahi
kufanya kazi mahakamani. Mshairi huyo wa Kiislamu alipitisha wakati wake
mwingi kusoma mashairi. Ibun Ta'awidhi ametunga mashairi mazuri sana na
marefu ya kuwasifia Watu wa Nyumba ya Mtume Mtukufu SAW. Mashairi huyo
kabla ya kupoteza macho yake alifanya jitihada kubwa za kukusanya
athari zake na hata baada ya kupofuka macho yake aliendelea kutunga
mashairi.
Na miaka 498 iliyopita katika siku kama ya leo, kulitokea mapigano ya
kihistoria ya Chaldoran kati ya Iran na dola la Othmania katika eneo la
bonde lililoko kati ya Tabriz na Khoui, kaskazini magharibi mwa Iran.
Mapigano hayo yalikuwa kati ya wapiganaji wa Shah Ismail Swafawi na
vikosi vya Sultan Salim Othmani.
No comments:
Post a Comment