NAIBU MRATIBU WA SKAUTI TANGA;
JAMII YA KISLAM IZINGATIE MAFUNDISHO WALIYOPATA KATIKA KIPINDI HIKI
Huku zikiwa zimebakia siku chache kukamilika kwa mwezi wa ramadhani, Jamii ya kiislam imeaswa kuzingatia mafunzo yatokanayo na mwezi huo katika maisha yao ya kila siku.
Hayo yamesemwa na mratibu msaidizi wa skauti wa kiislamu mkoa wa Tanga Ustadh Selemani Amiri Mssey alipokuwa akitoa ujumbe wake katika ghafla ya kufuturisha iliyoandaliwa na skauti wa kiislamu jiji la Tanga leo katika shule ya msingi Mwakidila.
Aidha aliwataka wazazi na walezi kuhakikisha vijana wao wanasherehekea siku kuu ya Idd ul Fitr kwa kufuata mafunzo ya Mtume Mohammad (Swallalahu alaihi Wassallam) kwa kujiepusha na vitendo viovu.
Wengine waliohudhuria ni pamoja na kiongozi wa mafunzo ya gwaride la skauti jiji la Tanga kamanda Hassan Shakha pamoja na viongozi mbalimbali wa dini ya kiislamu jiji laTanga
No comments:
Post a Comment