TRANSLATE THIS BLOG

Friday, October 5, 2012


AC Milan yabembeleza Mashabiki kuona Dabi na Inter ndani ya San Siro


Ingawa Dabi ya Jiji la Milano ni moja ya Dabi kubwa Barani Ulaya lakini Mechi hiyo ya Wikiendi hii imechukua hatua mpya pale Klabu ya AC Milan kuwabembeleza Mashabiki wake kuhudhuria pambano hilo na Mahasimu wao Inter Milan litakalochezwa ndani ya Uwanja wa San Siro.

AC Milan wanaingia kwenye Dabi hii wakiwa nafasi ya 11 wakiwa na Pointi 7 zikiwa ni Pointi 5 nyuma ya Inter Milan, ambao wako nafasi ya 3, na Pointi 9 nyuma ya vinara Juventus.

VS

Huku wakiwa wameondokewa na Wachezaji wao nyota, Zlatan Ibrahimovic na Thiago Silva, waliouzwa kwa Paris Saint-Germain, Mashabiki wa AC Milan wamekuwa wakisusa Mechi za Klabu yao.

Mpaka jana Jumatano ni Tiketi 55,000 tu zimeuzwa kwa ajili ya Dabi hiyo itakayochezwa Jumapili na miongoni mwa hizo ni Tiketi 23700 za wale Washabiki wanaokata Tiketi za Msimu mzima wakati Uwanja wa San Siro hupakia Watu 80,018.

Wiki iliyopita, kwenye Mechi ya kwanza waliyoshinda nyumbani, Watu 28,000 tu walihudhuria kushuhudia AC Milan ikiifunga Cagiari 2-0.

Msimu uliopita Mashabiki 79,612 walishuhudia Inter Milan ikiifunga AC Milan 1-0 kwa bao la Diego Milito na Mwaka juzi, Watu 80,000 walikuwepo AC Milan ilipoitwanga Inter Milan bao 3-0.

Uhafifu wa mahudhurio umeifanya AC Milan iweke Video kwenye Tovuti yake ambayo Nahodha Massimo Ambrosini na Straika Stephan El Shaarawy wanawabembeleza Mashabiki wao na kuwaambia: “Dabi bila nyie haina maana yeyote!”

Juzi, AC Milan walipata ushindi mtamu wa ugenini kwenye UEFA CHAMPIONZ LIGI walipoichapa Zenit St Petersburg bao 3-2.

Nae Meneja wa AC Milan, Massimiliano Allegri, ambae amekuwa akisakamwa kwa mwendo mbovu, amedai: “Ni Magazeti ndio yanyodai tupo hali mbaya. Tunaingia kwenye Dabi tukitoka kwenye ushindi mzuri…ingawa tunajua Dabi siku zote zina maajabu!”

RATIBA=Serie A

[SAA za Bongo]

Jumamosi Oktoba 6

19:00 Chievo Verona v Sampdoria

21:45 Genoa v Palermo

Jumapili Oktoba 7

13:30 AS Roma v Atalanta

16:00 Torino FC v Cagliari

16:00 Siena v Juventus

16:00 Pescara v SS Lazio

16:00 Catania v Parma

16:00 Fiorentina v Bologna

21:45 AC Milan v Inter Milan

21:45 Napoli v Udinese

No comments:

Post a Comment