TRANSLATE THIS BLOG

Monday, October 8, 2012


Suarez AFUNGIWE kwa kujidondosha makusudi!

Chapisha
Toleo la kuchapisha

MENEJA STOKE CITY, Pulis, aitaka FA imuadhibu Suarez!!

MENEJA mwingine ataka RVP aadhibiwe!!

Bosi wa Stoke City Tony Pulis amekitaka Chama cha Soka England, FA, kimuadhibu Straika wa Liverpool Luis Suarez kwa tabia yake ya kutaka kuwahadaa Marefa kwa kujidondosha makusudi ndani ya boksi ili apate Penati.

Jana, Stoke City ilikuwa Anfield kucheza na Liverpool kwenye Mechi ya Ligi Kuu England ambayo ilimalizika 0-0 na katika Kpindi cha Pili Luis Suarez ‘alijidondosha’ kutaka Penati ambayo Tony Pulis anaamini ulikuwa ni udanganyifu.


Pulis amesema: “Siku nyingi nimepigia kelele hili na Kipindi cha Pili tukio moja lilikuwa aibu kubwa! FA walitazame hili. Wampe Kifungo Mechi 3 na ataacha kujirusha!”

Alipohojiwa, Meneja wa Liverpool, Brendan Rodgers, alijibu: “Sikuona tukio hilo hivyo siwezi kusema chochote lakini chochote anachofanya Luis litakuwa tatizo tu!”

Hata hivyo, kuhusu tukio la Suarez kujidondosha kwa makusudi, FA haiwezi kuchukua hatua yeyote ile kwani Sheria zinawaruhusu kutoa adhabu pale tu matukio yalistahili Kadi Nyekundu na Refa hakuona na si matukio ambayo yangestahili Kadi ya Njano.

-----------------------------------------------------

Robin van Persie

Wakati huo huo, Meneja wa Newcastle United  Alan Pardew ameitaka FA imwadhibu Straika wa Manchester United Robin van Persie kwa kile alichodai kumpiga ‘kipepsi’ Kiungo wa Newcastle, Yohan Cabaye, katika Mechi ya jana ya Ligi Kuu England huko Sports Direct Arena ambayo Manchester United iliitandika Newcastle bao 3-0.


Ingawa mwenyewe amekiri hakuliona tukio ambalo lilitokea wakati si Van Persie wala Cabaye kuwa na mpira huku wote wakikimbilia golini, Pardew amedai: “Van Persie alimtazama Cabaye na kumpiga kiwiko, nikiwa mkweli, FA walitazame tukio hilo.”

FA inaweza kulipitia tukio hilo na kutoa adhabu ikiwa tu Refa wa Mechi hiyo, Howard Webb, atakiri hakuliona tukio hilo na kama angeliliona angetoa Kadi Nyekundu.



No comments:

Post a Comment