TRANSLATE THIS BLOG

Friday, October 5, 2012


John Terry apewa hadi Oktoba 18 kukata Rufaa!


ChapishaToleo la kuchapisha

FA yachapisha Ripoti ya Kesi iliyomfungia Mechi 4, Faini £220,000

Kufuatia kuchapishwa kwa Ripoti yenye Kurasa 63 zilizoelezea kwanini John Terry amefungiwa Mechi 4 na kupigwa Faini £220,000, Nahodha huyo wa Chelsea sasa ana Siku 14, hadi Oktoba 18, kukata Rufaa.

Kiini cha Ripoti hiyo ambayo ilielezea mwenendo wa Kesi yake mbele ya Jopo Huru la FA, Chama cha Soka England, aliyoshitakiwa kwa kumkashifu kibaguzi Beki wa QPR, Anton Ferdinand, kimetaja kuwa Utetezi wa Terry kwenye Kesi hiyo ulikuwa ‘hauwezekani, haueleweki na wa kupanga.’

Ripoti hiyo pia imefafanua kuwa Kifungo cha Terry kimekuwa nusu ya kile cha Luis Suarez wa Liverpool kwa kumkashifu kibaguzi Patrice Evra wa Manchester United kwa vile Terry alitumia neno la kibaguzi ‘mweusi’ mara moja na Suarez alirudia mara nyingi.

Hata hivyo, Ripoti hiyo imebainisha kuwa Jopo lao limekubali kuwa Terry sio mbaguzi.


Pia Ripoti hiyo imetoboa kuwa ushahidi wa Mchezaji wa Chelsea, Ashley Cole, ulitofautiana kutoka maelezo ya kwanza ya Cole kwa FA ambayo Cole hakutaja kumsikia Ferdinand akitaja neno ‘mweusi’ wakati maelezo ya baadae yalionyesha Cole alimsikia Ferdinand akitaja neno hilo na mabadiliko hayo ni kufuatia Afisa wa Chelsea, David Banard, kutaka maelezo ya Cole yabadilishwe.


Ripoti hiyo imesema tofauti hiyo ya ushahidi wa Cole haukuwasilishwa Mahakamani wakati Kesi iliposikilizwa na Jopo lina imani kama Hakimu wa Kesi iliyomwona Terry hana hatia wangejua tofauti hiyo wangetizama mara mbili ushahidi wa Cole.

Ripoti hiyo imekiri kuwa Anton Ferdinand amekashifiwa kibaguzi na hilo limemwathiri lakini Siku zote amekuwa mtulivu na mwenye heshima.

Ikiwa Terry ataamua kukata Rufaa Kifungo chake kitasitishwa hadi uamuzi wa Rufaa utoke lakini akikubali Adhabu aliyopewa Kifungo chake kitaanza mara moja lakini ikiwa hatatoa jibu lolote adhabu yake itaanza mara tu baada ya Oktoba 18.

No comments:

Post a Comment