TRANSLATE THIS BLOG

Monday, October 15, 2012


                                  BRAZIL v JAPAN: Marcelo avunjika!

MFUPA wa Kidole cha Mguu, kuwa nje hadi Miezi 3!!

Fulbeki wa Brazil na Real Madrid Marcelo amevunjika mfupa wa kidole cha mguu wakati akiwa mazoezini na Timu ya Taifa ya Brazil inayojitayarisha kucheza Mechi ya Kirafiki na Japan huko Wroclaw, Poland Jumanne Oktoba 16 na hili ni pigo kubwa kwa Real Madrid kwani Ijumaa walimpoteza Fulbeki mwingine, Fabio Coentrao, alieumia akiwa na Nchi yake Portugal iliyokuwa ikicheza na Russia.

Wachezaji wote hao wawili watarudi kwenye Klabu yao Real Madrid kwa uchunguzi zaidi.


Baadae Shirikisho la Soka la Brazil lilitoa taarifa kuwa Marcelo anategemewa kuwa nje ya Uwanja kwa kipindi kinachoweza kufikia Miezi mitatu.

Mechi ya Brazil na Japan itakuwa Mechi ya pili ya Kirafiki kwa kila Timu kucheza Barani Ulaya ndani ya Wiki moja kufuatia Brazil kuichapa Iraq 6-0 Alhamisi iliyopita huko Malmo, Sweden na Japan kuitungua France 1-0 huko Paris, France.

Brazil ndio watakuwa Wenyeji wa Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2014 na Japan wapo kwenye kinyang’anyiro cha kuingia Fainali hizo kutoka Kundi lao la Bara la Asia.

No comments:

Post a Comment