TRANSLATE THIS BLOG

Monday, October 15, 2012


Nani kuelekea Fainali za mataifa ya Africa 2013 jana zimefikia tamati.

Simba asiyefugika atakosekana kwa mara ya pili mfululizo katika fainali ya mataifa ya Afrika wakati mataifa kadhaa yakielekea Afrika kusini.


Cameroon ilitakiwa kushinda si chini ya mabao 2-0 kwa kuzingatia matokeo ya mchezo wa mkondo wa kwanza ambapo walifungwa na Cape Verde lakini licha ya Samuel Eto'o kurejea katika kikosi cha timu hiyo bado ushindi ulishindikana zaidi ya kuishia kupata matokeo ya ushindi wa mabao 2-1 na hivyo kushindwa kufikia dhamira.  

Licha ya kuondoshwa mashindanoni bado mashabiki wa soka wa Cameroon walishangilia bao zuri la mchezaji kinda mwenye umri wa miaka 16 ambaye ndio kwanza alikuwa akianza kuitumikia timu ya taifa ya Cameroon Fabrice Olinga, akiwa ni mchezaji zao la taasisi ya Samuel Eto'o Foundation, shambulizi lake  lilitokana na akili yake.

Mataifa yaliyofuzu ni pamoja na South Africa, Zambia, DR Congo, Ethiopia, Nigeria, Niger, Ghana, Mali, Togo, Burkina Faso, Angola, Cape Verde, Algeria, Morocco na Tunisia.

Ethiopia imefuzu kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1982, baada ya kuwachapa Sudan 2-0 na hivyo kufuzu kutokana na faida ya bao la ugenini wakati ambapo Niger ikifuzu baada ya kuwafunga Guinea kwa mabao 2-0 katika mchezo uliochezwa mjini Niamey.

Burkina Faso walihitaji goli la dakika za mwisho kupitia kwa Alain Traore na hivyo kujihakikishia ushindi wa mabao 3-1dhidi ya Jamhuri ya kati ili kukwepa kichapo cha faida ya goli la ugenini.

Emmanuel Adebayor alifunga goli muhimu lililo amua hatma ya Togo baada ya kuichapa Gabon 3-2, wakati ambapo mshambuliaji wa zamani wa Manchester United  Manucho alipoibuka shujaa wa Angola akifunga magoli mawili na kuwadhoofisha Zimbabwe kwa mabao 2-0.

DR Congo imefungwa mabao 2-1 na Equatorial Guinea lakini imefanikiwa kufuzu kwa ushindi wa jumla wa mabao 5-2, wakati ambapo Algeria ikiwachapa  Libya 2-0 na kujihakikishia ushindi wa jumla wa mabao 3-0.

Ghana, Mali, Morocco, Nigeria, Tunisia na bingwa mtetezi Zambia, wao wamefanikiwa kufuzu katika michezo yao iliyochezwa jumamosi.

Cote d'Ivoire ni kama itaungana na mataifa mengine yaliyofuzu kufuatia mchezo wao dhidi ya Senegal kuvunjika baada ya kutokea kuvurugu za mashabiki licha ya kwamba shirikisho la soka barani Afrika kuwa kimya kufuatia tukio hilo lililotokea katika mji wa Dakar nchini Senegal.
--------------------------------------------------------

kwa ufupi


Villa: Bent haendi popote!!!
Meneja wa klabu ya Aston Villa Paul Lambert amesema hana mango wa kumuuza mshambuliaji wake amber kwa sass ameonekana kukalia kuti kavu Darren Bent ifikapo mwezi January katika dirisha dogo la usajili. 








No comments:

Post a Comment