TRANSLATE THIS BLOG

Wednesday, October 10, 2012



Thomas Vermaelen anaamini kuwa Jack Wilshere ana uwezo wa kuwa mmoja kati ya viungo hodari dunaini.

Kiungo huyo alikuwa nje ya uwanja kwa takribani miezi 14 akisumbuliwa na maumivu ya enka na mguu lakini amerejea akiwa vizuri katika kikosi cha timu ya taifa ya wachezaji wenye umri chini ya miaka 21.



Amenukuliwa na mtandao wa klabu hiyo akisema Vermaelen akisema,

"unajua alichokifanya katika msimu wake mzima wa kwanza akiwa na Arsenal, alifanya vitu vikubwa sana”. 

"kwa upande wangu anaweza kuwa mmoja kati ya viungo bora kabisa duniani. Ana uwezo mkubwa wa kufikia hapo.

"ninafuraha sana amerejea sasa. Anafanya kazi ya kurejesha uwezo wake kama zamani na hilo ni jambo muhimu. Nadhani baadaye ataibeba timu hii."

Wakati huo huo


Bacary Sagna

Bacary Sagna, ambae amepona baada ya kuvunjika mguu Mwezi Mei katika Mechi na Norwich, hataharakishwa kurudi Uwanjani bali ataimarishwa pole pole ili arudi na nguvu zaidi.

Sagna, ambae ameumia vibaya mara mbili ndani ya Mwaka mmoja, amesema yuko tayari kucheza ila bado anajiimarisha zaidi.

Wakati alipokosekana Sagna nafasi yake ilichukuliwa na Chipukizi Carl Jenkinson ambae amecheza vyema mno na Sagna amekiri hilo kwa kusema: “Amecheza vizuri sana na amejifunza mengi. Ametulia na ni Beki mzuri.”

Fellaini aumia!

Kiungo wa Everton, Marouane Fellaini, amejitoa kwenye Kikosi cha Belgium ambacho kinajitayarisha kwa Mechi za Ijumaa na Jummane ijayo za Kombe la Dunia dhidi ya Serbia na Scotland baada ya kuumia goti.

Fellaini alipata maumivu hayo Jumamosi iliyopita Everton ilipocheza na Wigan kwenye Mechi ya Ligi Kuu England na Everton imesema haijulikani atakuwa nje kwa muda gani.

Hata hivyo Kambi ya Belgium imesema Mchezaji huyo atakuwa nje kwa Wiki 3 na hivyo kuzikosa Mechi za Everton dhidi ya QPR hapo Oktoba 21 na ile Dabi ya Liverpool dhidi ya Mahasimu wao Liverpool hapo Oktoba 28.

Kumkosa Fellaini ni pigo kubwa kwa Everton ambao wameanza vyema Msimu huu na wapo nafasi ya 4 kwenye Ligi Kuu baada ya kushinda Mechi 4, sare 2 na kufungwa moja tu.


No comments:

Post a Comment