TRANSLATE THIS BLOG

Wednesday, October 3, 2012


                Zambia, Cameroon zaomba kucheza CHALENJI CUP

Mabingwa wa Afrika, Zambia, wameomba kushiriki Mashindano ya Mwaka huu ya CHALENJI CUP, Tusker CECAFA Cup, ambayo ndio hutoa Nchi Bingwa wa Afrika Mashariki na Kati ambayo yatafanyika huko Kampala, Uganda kati ya Novemba 27 na Desemba 12.

Nchi nyingine 4 ambazo pia zimeomba kushiriki ni Cameroon, Malawi, Zimbabwe na Cote D'Ivoire.

Habari za maombi ya Nchi hizo zimethibitishwa na Katibu Mkuu wa CECAFA, Nicolas Musonye, ambae amesema ushiriki wa Nchi hizo utategemea uamuzi wa CECAFA ambao utatolewa baada ya Mkutano wao.

Mkutano huo wa CECAFA unategemewa kufanyika Wikiendi ijayo baada ya Mechi za Raundi ya Mwisho ya Mtoano ya AFCON 2013.

Mwaka jana, Malawi na Zimbabwe, zilishiriki kama Wageni waalikwa.

Hata hivyo, Musonye pia amesema ushiriki wa Nchi hizo ambao si Wanachama wa CECAFA utategemea pia ikiwa kama kutakuwa na Nchi Mwanachama ambayo itajitoa ingawa hadi sasa Nchi zote 12 Wanachama wa CECAFA zimethibitisha ushiriki wao.

Droo ya kupanga Ratiba ya Michuano hiyo itafanyika huko Kampala hapo November 8.

Bingwa Mtetezi wa CHALENJI CUP ni Uganda ambao pia ndio Nchi iliyotwaa Ubingwa huo mara 12 ambazo ni nyingi kupita Nchi nyingine.


No comments:

Post a Comment