TRANSLATE THIS BLOG

Wednesday, October 10, 2012


MPYA za LEO: Kaka Brazil kama kawa , Abidal ajifua, Busquets ‘nje’ UEFA!!

Wakati Mchezaji wa Barcelona, Abidal, aliebadilishwa Ini hivi karibuni, ameripotiwa kuanza tena mazoezi ili arejee dimbani Mwezi Desemba, Supastaa Kaka anategemewa kuichezea Brazil Alhamisi baada ya kimya cha Miaka miwili na Mchezaji mwingine wa Barcelona, Busquets, ametwangwa Kifungo cha Mechi mbili za UEFA CHAMPIONZ LIGI na UEFA.

                             Kaka kurudi Brazil

Kaka anatarajiwa kuivaa Jezi ya Brazil hapo Alhamisi itakapocheza Mechi ya Kirafiki na Iraq huko Malmo, Sweden ikiwa ni mara ya kwanza tangu Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2010 huko Afrika Kusini.

Mazoezini, hapo jana, Kaka amekuwa akiwekwa upande mmoja wa Wachezaji wa kawaida wa Brazil wanaoanza Mechi kina Oscar, Hulk na Neymar na Kocha wa Brazil, Mano Menezes, amedokeza kuwa Kaka atakuwa mmoja wa Viungo wake.

Mara baada ya Mechi hii na Iraq, Brazil watasafiri hadi Nchini Poland kucheza Mechi nyingine ya Kirafiki na Japan hapo Jumanne Oktoba 16.

           UEFA yamfungia Busquets Mechi 2!

Kiungo wa Barcelona Sergio Busquets, ambae alitolewa kwa Kadi Nyekundu katika Dakika ya 88 ya pambano lao na Benfica la UEFA CHAMPIONZ LIGI Wiki mbili zilizopita huko Lisbon, Ureno, amefungiwa Mechi 2 na UEFA.


Kufungiwa Sergio Busquets kutamfanya azikose Mechi mbili za Kundi G la UEFA CHAMPIONZ LIGI, zote dhidi ya Celtic, hapo Oktoba 23 na marudiano yake hapo Novemba 7.

Abidal back in Barca training
After seven months on the sidelines, Eric Abidal has returned to training at Barcelona

Beki wa Barcelona, Eric Abidal, yupo kwenye Milima ya Pyrenees, mpakani mwa Spain na France, akifanya mazoezi maalum baada ya kufanyiwa operesheni ya kubadilishwa Ini.

Abidal, mwenye Miaka, 33 na ambae ni Mchezaji wa Kimataifa wa France, anafanya mazoezi hayo chini ya Msimamizi wa mazoezi ya Viungo wa Barca, Emili Ricart.


Mwezi Machi, 2001, Abidal alifanyiwa operesheni kuondolewa uvimbe kwenye Ini na Miezi miwili baadae akarudi Uwanjani kwenye ushindi wao huko Wembley walipotwaa Kombe la UEFA CHAMPIONZ LIGI kwa kuitoa Manchester United.

Baadae Madaktari wakaamua inabidi Abidal atolewe Ini lake lote na kuwekewa jingine.

Mwenyewe Abidal ameshasema kuwa anategemea kurudi Uwanjani Mwezi Desemba.

No comments:

Post a Comment