Kamati ya Uchaguzi ya Chama cha Mpira wa Miguu cha Wanawake (TWFA) imetangaza kipindi cha pingamizi kwa waombaji uongozi katika uchaguzi wa chama hicho utakaofanyika mwezi ujao.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati hiyo Ombeni Zavala, kipindi cha pingamizi ni kuanzia Oktoba 5 hadi 9 mwaka huu, na pingamizi ziwasilishwe ofisi za TWFA. Mwisho wa kupokea pingamizi ni saa 10 kamili jioni, na hakuna ada kwa ajili ya pingamizi.
Pia amesema usaili kwa wagombea utafanyika kati ya Oktoba 12 na 14 mwaka huu kuanzia saa 3 asubuhi kwenye ofisi za TWFA zilizopo Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam. Kila mgombea anatakiwa kufika kwenye usaili akiwa na vyeti vyake halisi (original) vya kitaaluma.

No comments:
Post a Comment