TRANSLATE THIS BLOG

Monday, October 15, 2012


Nani kuelekea Fainali za mataifa ya Africa 2013 jana zimefikia tamati.

Simba asiyefugika atakosekana kwa mara ya pili mfululizo katika fainali ya mataifa ya Afrika wakati mataifa kadhaa yakielekea Afrika kusini.


Cameroon ilitakiwa kushinda si chini ya mabao 2-0 kwa kuzingatia matokeo ya mchezo wa mkondo wa kwanza ambapo walifungwa na Cape Verde lakini licha ya Samuel Eto'o kurejea katika kikosi cha timu hiyo bado ushindi ulishindikana zaidi ya kuishia kupata matokeo ya ushindi wa mabao 2-1 na hivyo kushindwa kufikia dhamira.  

Licha ya kuondoshwa mashindanoni bado mashabiki wa soka wa Cameroon walishangilia bao zuri la mchezaji kinda mwenye umri wa miaka 16 ambaye ndio kwanza alikuwa akianza kuitumikia timu ya taifa ya Cameroon Fabrice Olinga, akiwa ni mchezaji zao la taasisi ya Samuel Eto'o Foundation, shambulizi lake  lilitokana na akili yake.

Mataifa yaliyofuzu ni pamoja na South Africa, Zambia, DR Congo, Ethiopia, Nigeria, Niger, Ghana, Mali, Togo, Burkina Faso, Angola, Cape Verde, Algeria, Morocco na Tunisia.

Ethiopia imefuzu kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1982, baada ya kuwachapa Sudan 2-0 na hivyo kufuzu kutokana na faida ya bao la ugenini wakati ambapo Niger ikifuzu baada ya kuwafunga Guinea kwa mabao 2-0 katika mchezo uliochezwa mjini Niamey.

Burkina Faso walihitaji goli la dakika za mwisho kupitia kwa Alain Traore na hivyo kujihakikishia ushindi wa mabao 3-1dhidi ya Jamhuri ya kati ili kukwepa kichapo cha faida ya goli la ugenini.

Emmanuel Adebayor alifunga goli muhimu lililo amua hatma ya Togo baada ya kuichapa Gabon 3-2, wakati ambapo mshambuliaji wa zamani wa Manchester United  Manucho alipoibuka shujaa wa Angola akifunga magoli mawili na kuwadhoofisha Zimbabwe kwa mabao 2-0.

DR Congo imefungwa mabao 2-1 na Equatorial Guinea lakini imefanikiwa kufuzu kwa ushindi wa jumla wa mabao 5-2, wakati ambapo Algeria ikiwachapa  Libya 2-0 na kujihakikishia ushindi wa jumla wa mabao 3-0.

Ghana, Mali, Morocco, Nigeria, Tunisia na bingwa mtetezi Zambia, wao wamefanikiwa kufuzu katika michezo yao iliyochezwa jumamosi.

Cote d'Ivoire ni kama itaungana na mataifa mengine yaliyofuzu kufuatia mchezo wao dhidi ya Senegal kuvunjika baada ya kutokea kuvurugu za mashabiki licha ya kwamba shirikisho la soka barani Afrika kuwa kimya kufuatia tukio hilo lililotokea katika mji wa Dakar nchini Senegal.
--------------------------------------------------------

kwa ufupi


Villa: Bent haendi popote!!!
Meneja wa klabu ya Aston Villa Paul Lambert amesema hana mango wa kumuuza mshambuliaji wake amber kwa sass ameonekana kukalia kuti kavu Darren Bent ifikapo mwezi January katika dirisha dogo la usajili. 









                                  BRAZIL v JAPAN: Marcelo avunjika!

MFUPA wa Kidole cha Mguu, kuwa nje hadi Miezi 3!!

Fulbeki wa Brazil na Real Madrid Marcelo amevunjika mfupa wa kidole cha mguu wakati akiwa mazoezini na Timu ya Taifa ya Brazil inayojitayarisha kucheza Mechi ya Kirafiki na Japan huko Wroclaw, Poland Jumanne Oktoba 16 na hili ni pigo kubwa kwa Real Madrid kwani Ijumaa walimpoteza Fulbeki mwingine, Fabio Coentrao, alieumia akiwa na Nchi yake Portugal iliyokuwa ikicheza na Russia.

Wachezaji wote hao wawili watarudi kwenye Klabu yao Real Madrid kwa uchunguzi zaidi.


Baadae Shirikisho la Soka la Brazil lilitoa taarifa kuwa Marcelo anategemewa kuwa nje ya Uwanja kwa kipindi kinachoweza kufikia Miezi mitatu.

Mechi ya Brazil na Japan itakuwa Mechi ya pili ya Kirafiki kwa kila Timu kucheza Barani Ulaya ndani ya Wiki moja kufuatia Brazil kuichapa Iraq 6-0 Alhamisi iliyopita huko Malmo, Sweden na Japan kuitungua France 1-0 huko Paris, France.

Brazil ndio watakuwa Wenyeji wa Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2014 na Japan wapo kwenye kinyang’anyiro cha kuingia Fainali hizo kutoka Kundi lao la Bara la Asia.


                   COLY;Senegal watakubali adhabu.


Meneja wa timu ya taifa ya Senegal Ferdinand Coly amesema wanatarajia kuwa katika kipindi kigumu mbeleni, baada ya vurugu zilizo sababishwa na mashabiki wa soka wa nchi yao kiasi kupelekea mchezo wa kuwania kufuzu fainali za maraifa ya Afrika dhidi ya Ivory Coast  kuvunjika jumamosi.

Vurugu hizo zilitokea wakati ambapoa Ivory Coast ikiongoza kwa mabao 2-0 ambayo yalikuwa ni matokeo ya jumla ya mabao 6-2.

Amenukuliwa Coly akisema
"tunaelekea katika wakati mgumu lakini Senegal itakubaliana na adhabu".

"kwa wachezaji imewaumiza sana hususani wachezaji wachanga"
Mashabiki wa Senegal walianza kuwasha moto majukwaani na kutupa vitu uwanjani zikiwa zimesalia dakika 15 mchezo huo kumalizika mjini Dakar, muda mfupi baada ya mshambuliaji wa zamani wa Chelsea Didier Drogba kukandamiza bao la pili kwa njia ya penati.

                                          kwa ufupi

Ferdinand Alexandre Coly (born 10 September 1973 in Dakar) is a Senegalese former footballer.
Coly moved to France when he was 7 years old.He played in all of Senegal's matches in the 2002 FIFA World Cup. After impressing at the tournament, he moved from RC Lens to Birmingham City on loan. But this proved to be a poor career move as he only managed a single Premiership appearance, against Arsenal. Coly then moved on to Perugia. In his first season with theItalian club (2003–04), he made 11 appearances but never really impressed. He spent 2004-05 in Serie C (the team descended via playoffs to Serie B then suffered "another relegation", this time in the courts), making 29 appearances and scoring twice. In the summer of 2005 he made a move to Serie A side Parma, where he has been a regular...........

Wednesday, October 10, 2012



Thomas Vermaelen anaamini kuwa Jack Wilshere ana uwezo wa kuwa mmoja kati ya viungo hodari dunaini.

Kiungo huyo alikuwa nje ya uwanja kwa takribani miezi 14 akisumbuliwa na maumivu ya enka na mguu lakini amerejea akiwa vizuri katika kikosi cha timu ya taifa ya wachezaji wenye umri chini ya miaka 21.



Amenukuliwa na mtandao wa klabu hiyo akisema Vermaelen akisema,

"unajua alichokifanya katika msimu wake mzima wa kwanza akiwa na Arsenal, alifanya vitu vikubwa sana”. 

"kwa upande wangu anaweza kuwa mmoja kati ya viungo bora kabisa duniani. Ana uwezo mkubwa wa kufikia hapo.

"ninafuraha sana amerejea sasa. Anafanya kazi ya kurejesha uwezo wake kama zamani na hilo ni jambo muhimu. Nadhani baadaye ataibeba timu hii."

Wakati huo huo


Bacary Sagna

Bacary Sagna, ambae amepona baada ya kuvunjika mguu Mwezi Mei katika Mechi na Norwich, hataharakishwa kurudi Uwanjani bali ataimarishwa pole pole ili arudi na nguvu zaidi.

Sagna, ambae ameumia vibaya mara mbili ndani ya Mwaka mmoja, amesema yuko tayari kucheza ila bado anajiimarisha zaidi.

Wakati alipokosekana Sagna nafasi yake ilichukuliwa na Chipukizi Carl Jenkinson ambae amecheza vyema mno na Sagna amekiri hilo kwa kusema: “Amecheza vizuri sana na amejifunza mengi. Ametulia na ni Beki mzuri.”

Fellaini aumia!

Kiungo wa Everton, Marouane Fellaini, amejitoa kwenye Kikosi cha Belgium ambacho kinajitayarisha kwa Mechi za Ijumaa na Jummane ijayo za Kombe la Dunia dhidi ya Serbia na Scotland baada ya kuumia goti.

Fellaini alipata maumivu hayo Jumamosi iliyopita Everton ilipocheza na Wigan kwenye Mechi ya Ligi Kuu England na Everton imesema haijulikani atakuwa nje kwa muda gani.

Hata hivyo Kambi ya Belgium imesema Mchezaji huyo atakuwa nje kwa Wiki 3 na hivyo kuzikosa Mechi za Everton dhidi ya QPR hapo Oktoba 21 na ile Dabi ya Liverpool dhidi ya Mahasimu wao Liverpool hapo Oktoba 28.

Kumkosa Fellaini ni pigo kubwa kwa Everton ambao wameanza vyema Msimu huu na wapo nafasi ya 4 kwenye Ligi Kuu baada ya kushinda Mechi 4, sare 2 na kufungwa moja tu.



 Shirikisho la Ngumi la Kimataifa (IBF) pamoja na Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Nchini (TPBC) zimeidhinisha kufanyika kwa mapambano manne ya ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati Ghuba ya Uarabu na Uajemi jijini Dar-Es-Salaam mwezi wa Novemba mwaka huu.

Mapambanohayoambayonimaraya kwanza kufanyika katika ukanda huu wa dunia yatakuwa yanashirikisha mabondia kutoka Misri, Kenya, na Tanzania na yatarushwa live na televisheni za Tanzania, Kenya naMisri.

Kufanyika kwa mapambano haya kumewezekana baada ya makapuni manne kutoka Tanzania na Misri kuungana na Shirikisho la Ngumi la Kimataifa (IBF) na kuanzisha programu ya mwaka mmoja itakayoanza Novemba mwaka huu hadi Novemba mwakani.

Katikaprogramuhiimakampunihayapamojana IBF yataandaa mapambano kila baada ya mwezi mmoja Novemba, Januari, Machi, Mei, Julai, Septemba na Novemba mwakani.

Raiswa IBF katikabara la Afrika, Masharikiya Kati, Ghuba ya Uarabu na Uajemi Onesmo Ngowi aliyataja makampuni hayo kuwa ni pamoja na Jambo Concept inayomiliki vyombo vya habari vikiwamo gazeti la Jambo Leo, Tanzanite Sports Promotion Management, Kitwe General Traders yote ya Tanzania na Louaa Boxing Promotion ya Misri.

Katikamapambanohayo, mabondia Alphonce Joseph Mchumiatumbo atapambana na bondia wa Misri anayeishi nchini Marekani, Manzur Ali katika uzito wajuu (Heavyweight) kugombania mkanda wa IBF Mashariki ya Kati, Ghuba ya Uarabu na Uajemi na Afrika.

Bondia wa Misri, Mohammed Metually, ambaye ni bingwa wa Afrika anayetambuliwa na Baraza la Ngumi la Dunia (WBC) atapambana na bondia Nofart Emilio, wa Kenya kugombea mkanda wa IBF Mashariki ya Kati, Ghubaya Uarabu na Uajemi na Afrika katika uzito wa Bantam.

Naye bondia bora wa TASWA mwaka 2011 Nassibu Ramadhani, atachuana vikali na bondia asiyepigika, Nick Otieno, wa Kenya kugombea mkanda wa IBF Mashariki ya Kati, Ghuba ya Uarabu na Uajemi na Afrika katika uzito wa Super Flyweight.

Bondia anayepanda chati kwa kasi Haji Juma, kutoka viunga vya jiji la Tanga atapambana na bondia Twalib Mubiru, wa Kenya kugombea mkanda wa IBF Afrika katika uzito wa bantam.

Hii ni mara ya kwanza kwa Tanzania na bara la Afrika kuwa na mapambano mengi ya ubingwa wa IBF kwa usiku mmoja.

Mabalozi wengi wanaoziwakilisha nchi zao hapa Tanzania, wageni wengi wanaoishi Tanzania na wadau wengi wa ngumi kutoka Misri, Kenya, Uganda na chi za jirani watahudhuria mapambano haya kwa maelfu.

Imetumwana:

Onesmo Alfred McBride Ngowi

Rais,

IBF Africa, Masharikiya Kati, GhubayaUarabunaUajemi


TAWFA KUMENUKA;JOAN MINJA APINGWA

Wagombea sita wa nafasi mbalimbali za uongozi katika Chama cha Mpira wa Miguu wa Wanawake Tanzania (TWFA) wamewekewa pingamizi na wadau wa mchezo huo.

 Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TWFA, Ombeni Zavala, wagombea hao ni Joan Minja anayewania nafasi ya Mwenyekiti ambaye amewekwa pingamizi na wadau sita. Pia Isabellah Kapera ambaye anagombea uenyekiti amewekewa pingamizi moja.


 Wagombea watatu wa nafasi ya Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) nao wamewekewa pingamizi. Wagombea hao ni Julliet Mndeme (pingamizi sita), Zena Chande (pingamizi nne) na Jasmin Soud mwenye pingamizi tatu.

 Naye Rahim Maguza anayewania ujumbe wa Kamati ya Utendaji amewekewa pingamizi moja.

 Licha ya pingamizi hizo, wagombea wote wanatakiwa kuhudhuria usaili wakiwa na vyeti vyao halisi vya kitaaluma utakaofanyika Oktoba 12, 13 na 14 mwaka huu kwenye ofisi za TFF zilizopo Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam kuanzia saa 3 asubuhi

MPYA za LEO: Kaka Brazil kama kawa , Abidal ajifua, Busquets ‘nje’ UEFA!!

Wakati Mchezaji wa Barcelona, Abidal, aliebadilishwa Ini hivi karibuni, ameripotiwa kuanza tena mazoezi ili arejee dimbani Mwezi Desemba, Supastaa Kaka anategemewa kuichezea Brazil Alhamisi baada ya kimya cha Miaka miwili na Mchezaji mwingine wa Barcelona, Busquets, ametwangwa Kifungo cha Mechi mbili za UEFA CHAMPIONZ LIGI na UEFA.

                             Kaka kurudi Brazil

Kaka anatarajiwa kuivaa Jezi ya Brazil hapo Alhamisi itakapocheza Mechi ya Kirafiki na Iraq huko Malmo, Sweden ikiwa ni mara ya kwanza tangu Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2010 huko Afrika Kusini.

Mazoezini, hapo jana, Kaka amekuwa akiwekwa upande mmoja wa Wachezaji wa kawaida wa Brazil wanaoanza Mechi kina Oscar, Hulk na Neymar na Kocha wa Brazil, Mano Menezes, amedokeza kuwa Kaka atakuwa mmoja wa Viungo wake.

Mara baada ya Mechi hii na Iraq, Brazil watasafiri hadi Nchini Poland kucheza Mechi nyingine ya Kirafiki na Japan hapo Jumanne Oktoba 16.

           UEFA yamfungia Busquets Mechi 2!

Kiungo wa Barcelona Sergio Busquets, ambae alitolewa kwa Kadi Nyekundu katika Dakika ya 88 ya pambano lao na Benfica la UEFA CHAMPIONZ LIGI Wiki mbili zilizopita huko Lisbon, Ureno, amefungiwa Mechi 2 na UEFA.


Kufungiwa Sergio Busquets kutamfanya azikose Mechi mbili za Kundi G la UEFA CHAMPIONZ LIGI, zote dhidi ya Celtic, hapo Oktoba 23 na marudiano yake hapo Novemba 7.

Abidal back in Barca training
After seven months on the sidelines, Eric Abidal has returned to training at Barcelona

Beki wa Barcelona, Eric Abidal, yupo kwenye Milima ya Pyrenees, mpakani mwa Spain na France, akifanya mazoezi maalum baada ya kufanyiwa operesheni ya kubadilishwa Ini.

Abidal, mwenye Miaka, 33 na ambae ni Mchezaji wa Kimataifa wa France, anafanya mazoezi hayo chini ya Msimamizi wa mazoezi ya Viungo wa Barca, Emili Ricart.


Mwezi Machi, 2001, Abidal alifanyiwa operesheni kuondolewa uvimbe kwenye Ini na Miezi miwili baadae akarudi Uwanjani kwenye ushindi wao huko Wembley walipotwaa Kombe la UEFA CHAMPIONZ LIGI kwa kuitoa Manchester United.

Baadae Madaktari wakaamua inabidi Abidal atolewe Ini lake lote na kuwekewa jingine.

Mwenyewe Abidal ameshasema kuwa anategemea kurudi Uwanjani Mwezi Desemba.


TENGA AZITAKA KAMATI ZA UCHAGUZI KUSIMAMIA KANUNI
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodegar Tenga
amezitaka Kamati za Uchaguzi kufanya kazi kwa kuzingatia Kanuni za
Uchaguzi za Wanachama wa TFF ili kuwa na uchaguzi huru na wa haki.

 Akizungumza na Waandishi wa Habari, Dar es Salaam leo, Rais Tenga amesema uongozi  wa mpira wa miguu unahitaji uamuzi mgumu, hivyo Kamati za Uchaguzi ambazo zimeundwa kwa mujibu wa Katiba zinatakiwa kufanya kazi kwa kuzingatia kanuni na si kuangalia sura za watu.

 Amepongeza kamati zilizosimamia uchaguzi kwa kufuata kanuni, na ingawa kila mtu ana haki ya kuongoza, jambo lolote lazima liwe na kanuni, kwani hata kwenye mikutano ya hadhara kuna kanuni.

 “Huwezi kufika kwenye mkutano wa hadhara na wewe unaanzisha mkutano wako. Lazima kanuni ziheshimiwe ili kufanya uchaguzi uwe huru na wa haki. Nini kimetokea kwenye maeneo ambayo kuna matatizo? Kila mwanachama wetu mkoa/chama shiriki) ana Kamati ya Uchaguzi ambayo imeundwa kwa mujibu wa kanuni.
 “Zile kamati hazitekelezi majukumu yake, unampitisha mtu unajua hana sifa unasema acha akafie mbele (Kamati ya Uchaguzi ya TFF). Kanuni zinasema jaza fomu mwenyewe, weka nakala za vyeti na si kwamba huyu tunamjua. Kanuni zinatakiwa zifuatwe, ukienda kinyume unaondolewa,” amesema.

 Amesisitiza kamati zifanye kazi kwa kufuata kanuni ili kusaidia mpira wa miguu kwani zimeundwa kihalali, kwa hiyo zisiogope kuengua hata walioziteua kama hawana sifa.

 Pia Rais Tenga amezitaka Kamati za Utendaji na Sekretarieti kutoziingilia Kamati za Uchaguzi katika mchakato wa uchaguzi, badala yake zinatakiwa kuziwezesha tu (facilitation).

Amesema baadhi ya wagombea nao ni tatizo kwani wanaingia kwenye uchaguzi bila kuzielewa Katiba za vyama vyao na Kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF, hivyo ni vizuri wakazielewa kwanza.

 Rais Tenga amesema ni vizuri wanachama wote wakafanya uchaguzi kabla ya uchaguzi wa TFF utakaofanyika Desemba mwaka huu ili wapate fursa ya kupiga kura kwenye uchaguzi huo wa shirikisho.

 Vilevile amewataka wadau kujitokeza kwa wingi kuwania uongozi kwenye chaguzi za vyama wanachama wa TFF, kwani mwitikio umeonekana kuwa mdogo kulinganisha na umaarufu wa mchezo wenyewe.

 Amepongeza vyama vya mikoa ambavyo tayari vimefanya uchaguzi wao. Baadhi ya vyama  hivyo ni Arusha, Dodoma, Iringa, Kagera, Kigoma, Kilimanjaro, Manyara, Mara, Morogoro, Mtwara na Singida.


Tuesday, October 9, 2012


KAMANDA KINYELA MGENI RASMI MARSHALI vs SEBYALA


KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Charles Kenyela, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika pambano la kuwania ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati baina ya Thomas Mashali wa Tanzania na Medi Sebyala wa Uganda litakalopiganwa Oktoba 14, kwenye ukumbi wa Friends Corner Manzese jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam jana, Mratibu wa pambano hilo linalosimamiwa na Oganaizesheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBO), Regina Gwae, alisema mbali Kamanda Kenyela, kutakuwa na wageni wengine maalum akiwemo Mbunge wa Kinondoni, Iddi Azan.


Alisema wanashukuru kwa ushirikiano wa viongozi hao katika maandalizi na hatimaye wamethibitisha ushiriki wao katika pambano hilo ambalo linavuta hisia za watu wengi na wapenzi wa ngumi jijini Dar es Salaam.

Alitaja mapambano manne ya utangulizi ya siku hiyo ambapo Abdul Awilo atazichapa na Shedrack Juma, Selemani Shaaban atavaana na Hamisi Mohamed huku Jonas Segu akinyukana na Ibrahim Class wakati Charles Mashali atatwangana na Teacher Aaron.

“Tumeamua kuchukua mabondia kutoka katika klabu zenye mashabiki wengi, tumechukua kwa Mzazi tumechukua klabu ya manzese anakotoka Mashali na Super D Boxing Club,’ alisema Regina.

Regina alisema, bondia Medi Sebyala na Kocha wake wanatarajiwa kuwasili nchini Oktoba 11 na tayari maandalizi ya safari yao yamekamilika, ikiwemo kuwatumia tiketi na wameshazipokea.

Mratibu huyo, aliishukuru kampuni ya Promasidor wasambazaji wa Sossi Poa, Gazeti la Jambo leo, City Sports Lounge na Times Fm kwa kuwa bega kwa bega kuhakikisha pambano hilo linafanikiwa na kuwa, milango bado iko wazi kwa wadau kujitokeza kufanikisha mchezo huo ambao ni chanzo cha ajira kwa vijana.

Monday, October 8, 2012

MBOYA CUP 2012.......UTATOA YAMBANIA MTU!!!!!

Timu ya soka ya utatoa leo imefanikiwa kutinga hatua ya makundi katika muendelezo wa ligi ya MBOYA CUP inayoendelea kutimua vumbi katika uwanja wa chera baada ya leo kuwasambaratisha Mako bao 5-4
                                                                  (kikosi cha Utatoa Fc)

Magoli ya Utatoa yametiwa kimiani na mshambuliaji wao kuziwa ambae ameifungia timu yake magoli 3,na Amir Kai 2....na kwa upande wa Mako wafungaji ni Issa Amani  magoli 3 na Hussein Tall goli 1

Kwa matokeo hayo Timu ya Utatoa imeungana na wenyeji Road Camp,YeboYebo,Makamuzi...katika hatua ya makundi...
                                                              (kikosi cha mako Fc)

Lgi hiyo itaendelea kutimua tena vumbi lake hapo kesho kwa mchezo mmoja kati ya  KISHOKA vs FULL COMBAT

Taarifa kwa mujibu wa Mratibu wa Ligi
Rajab  Salehe

TADA CHAFANYA UCHAGUZI!!

CHAMA Cha Darts Tanzania(TADA), kimefanya uchaguzi rasmi  na kuwachagua viongozi watakaokiongoza chama hicho kwa miaka mitatu baada ya kukaa na Uongozi wa kuteuliwa kukaimu madaraka kwa muda.

TADA ilifanya uchaguzi kupitia wajumbe wake wa kamati kuu kutoka katika mikoa yote ya Tanzania chini ya usimamizi wa  Wajumbe kutoka Baraza la Michezo Tanzania na kuwasimika, Gesase Waigama kutoka Klabu ya Ibukoni Tabata Segerea ya  Dar es Salaam kuwa Mwenyekiti wa kuchaguliwa kisheria atakaye iongoza DATA kwa miaka mitatu.

Makamu mwenyekiti alichaguliwa David Msabi kutoka Klabu ya Mzinga Morogoro,Katibu Mkuu wa Tada alichaguliwa Kale Mgonja kutoka Klabu ya Kashudu ya Magomeni Dar es Salaam ambapo makamu wake alichaguliwa Tareto Kitali kutoka Klabu ya Magereza Moshi.Katibu Mwenezi wa TADA alichaguliwa Ignas Bwangaya kutoka Klabu ya Katumba Kinondoni Dar es Salaam na Mwekahazina wa chama hicho alichaguliwa Harrod Mono kutoka Klabu ya Kashudu ya Dar es Salaam.

Upande wa Wajumbe wa kiume walichakuliwa, George Kassama kutoka Klabu ya Safari ya MKOANI Kagera Kanda ya Ziwa,Ramadhani Simba kutoka Magereza Moshi,Adelade Chikoma kutoka Polisi Mbeya,Andrew Samo kutoka Pwani,Eakimu Rwisigalo kutoka Pwani na Dokta Mwiru kuoka Kanda ya Kati Dodoma.

Wajumbe wakina mama walichaguliwa, Subira Waziri kutoka Dar es Salaam,Josephine Lamuyani kutoka Arusha,Fabila Namajojo Kutoka Morogoro,Anna Mwakabonga kutoka Mbeya na Safina Msuya kutoka Magereza Moshi.

Mwenyekiti mpya wa miaka mitatu ijayo, Gesase Waigama aliwashukuru wasimamizi kutoka Baraza la michezo Tanzania  kwa usimamizi mzuri ambao haukuwa na malalamiko na kuwataka wajumbe wote waliogombea na kuchaguliwa kuwajibika kufanya kazi kwa nafasi zao kwa kufuata Katiba ya chama  ili kuiendeleza Darts Tanzania na pia aliwashukuru wajumbe wote walioshiriki uchaguzi na kuwachagua na wale ambao hawakuchaguliwa alisema atatoa ushilikiano kwao katika kuendeleza chama na mchezo na kuwaomba wagombee tena awamu nyingine.

Nae Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo ambaye anadhamini Darts aliwapongeza Viongozi waliochaguliwa ambao wengi wao ni wale walikuwa kwenye uongozi wa kuteuliwa na pia aliwapongeza wajumbe waliowachagulia kwani hicho ni kipimo tosha cha kudhihirisha kuwa wanafanya kazi vizuri na ndio maana wamechaguliwa hivyo atatoa ushirikiano wa kutosha kuhakikisha mchezo wa Dars unaenea nchini kote na kurudi kwenye thamani yake.

-------------------------------------------------------------------
wakati huo huo



Kampuni ya Bigright Promotions imeipongeza oganaizesheni ya ngumi za kulipwa nchini(TPBO) kwa kumteua bw Masoud Sinani kuwa makamu wa rais wake.

Bw sinani mwenye stashahada ya biashara aliyoichukulia katika chuo cha salsbury cha nchini ni uingereza ni mdau wa karibu wa michezo,mhamasishaji na mratibu wa michezo mtwara.

Tpbo katika kujipanga vizuri imeonelea ni bora kuimarisha safu ya uongozi mikoani,kwa hiyo ofisi ya makamu wa rais yaweza kuwa mtwara,

Tpbo ambayo imejijenga vema nchini na kuendeleza mchezo wa ngumi kwa kuwapa kipaumbele mabondia wa mikoani kwa kunyanyua vipaji vyao na kuamsha mchezo wa ngumi pale ambapo umelala na watu kudhani hakuna mabondia eneo hilo kumbe wapo.

Juu ya pongezi hizo Bigright promotion kupitia mkurugenzi wake ibrahim kamwe imeahidi kuiunga mkono TPBO katika kuendeleza mchezo wa ngumi na kusaidiana nayo kwa nguvu zote katika utendaji.

Wakati huohuo Tpbo yenyewe imepanga kukutana na viongozi wake,marefa na majaji makao makuu ya ofisi hiyo,tarehe 10/10/2012 katika semina fupi na mkutano utakaozungumzia mpambano wa bingwa wa taifa Thomas Mashali atakae zipiga na mganda med sebyala tarehe 14/10/2012 kugombania ubingwa wa Afrika mashariki na kati





Timu ya utabibu ya Real Madrid imemnyooshea Cristiano Ronaldo alama ya kijani kwenda Ureno kuripoti kwa ajili ya majukumu ya kimataifa.

Mshambuliaji huyo hatari alikuwa katika maumivu ya bega katika mchezo huo wa jana wa ligi kuu ya soka nchini Hispania La Liga ambapo Madrid ilikwenda sare ya mabao 2-2 na Barcelona mchezo uliopigwa katika dimba la Nou Camp.

Kama hiyo haitoshi , Ronaldo tangu jana usiku amekuwa akifanyiwa uangalizi na madaktari wa Madrid akiwa nyumbani, na tayari mabingwa hao wa ligi ya Hispania wametangaza kupitia mtandao wa klabu hiyo kuwa Ronaldo hajapatwa na maumivu makubwa.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27 alitazamiwa kuelekea nyumbani Ureno mchana wa leo kwa ajili ya jukumu la kimataifa ambapo Ureno inatarajia kucheza dhidi ya Russia ijumaa mchezo wa kuwania tiketi ya kucheza fainali ya kombe la dunia 2014 kabla ya mchezo mwingine dhidi ya Ireland ya Kaskazini siku nne baadaye.
-----------------------------------------------------------

Kiungo wa Manchester City Barry: Siko tayari kustaafu soka la kimataifa

Kiungo wa Manchester City Gareth Barry amesisitiza kuwa hayuko tayari kustaafu soka la kimataifa huku  akiwa na matumaini makubwa kuwa atachaguliwa katika kikosi kitakacho tangazwa hivi karibuni, licha ya kutokuwepo katika kikosi kilichopita ambacho kilicheza dhidi ya San Marino and Poland.

Barry, ambaye alifanya kazi kubwa katika timu yake ya City ambayo ilichomoza na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Sunderland jumamosi, hajachaguliwa tangu mchezo wa kwanza wa kirafiki wa kocha Roy Hodgson dhidi ya Norway mwezi May.

MECHI za KIMATAIFA: Kurindima kuanzia Ijumaa!!


Ijumaa Oktoba 16, Mechi za Kimataifa zitaanza kuchezwa na Barani Ulaya, Marekani ya Kusini na kwingineko ni Mechi za Mchujo kuwania kufuzu kucheza Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2014 huko Brazil lakini kwa Afrika, hapo Jumamosi na Jumapili, kutakuwa na Mechi za marudiano za Raundi ya Mwisho ya Mchujo kupata Timu 15 zitakazoungana na Wenyeji Afrika Kusini kucheza Fainali za AFCON 2013, Kombe la Mataifa ya Afrika, Januari 2013.

RATIBA MECHI ZOTE:

ULAYA-Mechi za Makundi Kombe la Dunia 2014

[Saa za Bongo]

Ijumaa Oktoba 12

1800 Russia v Portugal

1830 Finland v Georgia

1900 Armenia v Italy

1900 Faroe Islands v Sweden

1900 Kazakhstan v Austria

2000 Albania v Iceland

2000 Czech Republic v Malta

2030 Liechtenstein v Lithuania

2030 Turkey v Romania

2100 Belarus v Spain

2100 Bulgaria v Denmark

2100 Moldova v Ukraine

2115 Slovakia v Latvia

2130 Estonia v Hungary

2130 Netherlands v Andorra

2130 Serbia v Belgium

2145 Greece v Bosnia-Hercegovina

2145 Rep of Ireland v Germany

2145 Wales v Scotland

2200 England v San Marino

2200 Luxembourg v Israel

2230 Macedonia v Croatia

2230 Switzerland v Norway

2245 Slovenia v Cyprus

Jumanne Oktoba 16

Albania v Slovenia

Andorra v Estonia

Belarus v Georgia

Belgium v Scotland

Bosnia-Hercegovina v Lithuania

Czech Republic v Bulgaria

Hungary v Turkey

Iceland v Switzerland

Israel v Luxembourg

Latvia v Liechtenstein

Macedonia v Serbia

Portugal v Northern Ireland

Romania v Netherlands

Russia v Azerbaijan

San Marino v Moldova

Slovakia v Greece

Spain v France

Ukraine v Montenegro

2000 Cyprus v Norway

2100 Faroe Islands v Rep of Ireland

2130 Austria v Kazakhstan

2130 Croatia v Wales

2145 Germany v Sweden

2145 Italy v Denmark

2200 Poland v England

FAHAMU:
-ULAYA yapo Makundi 9

-Washindi 9 wa kila Kundi wataingia Fainali moja kwa moja na Washindi wa Pili 8 bora wenye rekodi nzuri dhidi ya Timu zilizomaliza nafasi za Kwanza, Tatu, Nne na Tano kwenye Kundi lao watapelekwa kwenye Droo kupanga Mechi 4 za Mchujo, zitakazochezwa nyumbani na ugenini, ili kupata Timu nne zitakazoingia Fainali.

--------------------------------------------------------------

AFCON 2013=Kombe la Mataifa ya Afrika

[Fainali Afrika Kusini-Januari 2013]

[Kwenye Mabano Matokeo Mechi za kwanza]

Jumamosi Oktoba 13

Malawi v Ghana [0-2]

Botswana v Mali [0-3]

Nigeria v Liberia [2-2]

Uganda v Zambia [0-1]

E.Guinea v Congo DR [0-4]

Senegal v Cote d'Ivoire [2-4]

Tunisia v Sierra Leone [2-2]

Morocco v Mozambique [0-2]

Jumapili Oktoba 14

Algeria v Libya [1-0]

Cameroon v Cape Verde [0-2]

Togo v Gabon [1-1]

Angola v Zimbabwe [1-3]

Niger v Guinea [0-1]

Ethiopia v Sudan [3-5]

Burkina Faso v Central African Republic [0-1]

FAHAMU: Washindi 15 wa Mechi hizi watajumuika na Wenyeji Afrika Kusini kwenye Fainali zitakazochezwa Afrika Kusini Januari 2013.

++++++++++++++++++++++++++++++

MAREKANI ya KUSINI-Mechi za Makundi Kombe la Dunia 2014

MSIMAMO:

1 Argentina Mechi 7 Pointi 14

5 Colombia Mechi 7 Pointi 13

3 Ecuador Mechi 7 Pointi 13

4 Uruguay Mechi 7 Pointi 12

2 Chile Mechi 7 Pointi 12

6 Venezuela Mechi 8 Pointi 11

7 Peru Mechi 7 Pointi 7

8 Bolivia Mechi 7 Pointi 4

9 Paraguay Mechi 7 Pointi 4

FAHAMU: Timu 4 za juu zinatinga Fainali Brazil moja kwa moja na ile ya 5 itaenda Mechi ya Mchujo.

Ijumaa Oktoba 12

Colombia v Paraguay

Ecuador v Chile

Bolivia v Peru

Argentina v Uruguay

Jumanne Oktoba 16

Bolivia v Uruguay

Venezuela v Ecuador

Paraguay v Peru

Chile v Argentina


CONCACAF [Nchi za Marekani ya Kati, Kaskazini na Carribean]- Mechi za Makundi Kombe la Dunia 2014==RAUNDI ya 3


KUNDI A
-USA
-Guatemala
-Jamaica
-Antigua and Barbuda

KUNDI B
-Mexico
-El Salvador
-Costa Rica
-Guyana

KUNDI C
-Panama
-Honduras
-Canada
-Cuba

FAHAMU:

-Mshindi wa kila Kundi na Mshindi wa Pili wataingia Raundi ya 4 ambayo ni ya mwisho itayochezwa kwa mtindo wa Ligi ili kutoa Timu 3 zitakazoenda Fainali za Kombe la Dunia moja kwa moja na ya 4 itapelekwa Mechi ya Mchujo.

-Kundi B: Mexico wamefuzu kuingia Raundi ya 4 kwa vile tayari wana Pointi 12 wakifuatiwa na El Salvador wenye 5, Costa Rica 4 na Guyana 1 huku kila Timu imebakiza Mechi 2.


RATIBA:

Ijumaa Oktoba 12

Antigua and Barbuda v USA

El Salvador v Costa Rica

Canada v Cuba

Guatemala v Jamaica

Guyana v Mexico

Panama v Honduras

Jumanne Oktoba 16

Honduras v Canada

Cuba v Panama

USA v Guatemala

Jamaica v Antigua and Barbuda

Costa Rica v Guyana

Mexico v El Salvador


PAMBANO LA SIMBA, OLJORO JKT LAINGIZA MIL 46/-
Pambano la Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Simba na Oljoro JKT ya Arusha lililochezwa jana (Oktoba 7 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa wenyeji kuibuka na ushindi wa mabao 4-1 limeingiza sh. 46,680,000.

Watazamaji 8,081 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 8,172,396.61 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 7,120,677.97.

Mgawo mwingine wa mapato hayo ni posho ya msimamizi wa kituo sh. 120,000, kamishna wa mechi sh. 193,000, waamuzi sh. 210,000, mwamuzi wa akiba (reserve referee) sh. 70,000, usafi na ulinzi wa uwanja sh. 2,350,000 na Wachina (stadium technical support) sh. 2,000,000.

Umeme sh. 300,000, maandalizi ya uwanja (pitch preparation) sh. 400,000, ulinzi wa mechi sh. 3,500,000 wakati tiketi ni sh. 3,175,000. Gharama za mchezo sh. 2,724,132.20, uwanja sh. 2,724,132.20, Kamati ya Ligi sh. 2,724,132.20, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 1,634,479.32 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,089,652.88.

PONGEZI KWA UONGOZI MPYA ARFA
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linatoa pongezi kwa uongozi mpya wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Arusha (KRFA) uliochaguliwa katika uchaguzi uliofanyika jana (Oktoba 7 mwaka huu).

Ushindi waliopata viongozi waliochaguliwa kuongoza chama hicho unaonesha jinsi wajumbe wa Mkutano Mkuu wa ARFA walivyo na imani kubwa kwao katika kusimamia mchezo huo mkoani Kigoma.

TFF inaahidi kuendeleza ushirikiano wake kwa Kamati ya Utendaji ya ARFA chini ya uenyekiti wa Khalifa Mgonja ambaye amechaguliwa tena kuongoza chama hicho.

Uongozi huo mpya una changamoto nyingi, kubwa ikiwa ni kuhakikisha unaendesha shughuli za mpira wa miguu mkoani Arusha kwa kuzingatia katiba ya ARFA pamoja na vyombo vya mpira wa miguu vilivyo juu yake.

Pia tunatoa pongezi kwa Kamati ya Uchaguzi ya ARFA na Kamati ya Uchaguzi ya TFF kwa kuhakikisha uchaguzi huo unaendeshwa kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi za wanachama wa TFF.

Viongozi waliochaguliwa katika uchaguzi huo ni Khalifa Mgonja (Mwenyekiti), Seif Banka (Makamu Mwenyekiti), Adam Brown (Katibu), Peter Temu (Mjumbe wa Mkutano Mkuu TFF), Omari Walii (Mwakilishi wa Klabu TFF) na Mwalizo Nassoro (Mhazini).

Waliochaguliwa kuwa Wajumbe wa Kamati ya Utendaji katika uchaguzi huo uliofanyika Leganga, Usa River ni Hamisi Issa, Athuman Mhando na Eliwanga Mjema. Nafasi ya Katibu Msaidizi iko wazi na itajazwa katika uchaguzi mdogo utakayofanyika baadaye.

Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

Stojkovic nje katika mechi ya kufuzu kombe la Dunia!!!!...

Mlinda mango wa Partizan Belgrade Vladimir Stojkovic atakosa mchezo wa kuwania kufuzu kucheza kombe la Dunia mwezi huu wakati timu yake ya Serbia itakapokuwa mawindoni baada ya  kuvunjika kikanyagio cha mguu  katika muendelezo wa ligi siku ya jumamosi….taarifa toka Serbian Football Association (FSS) .


katika taarifa iliyotolewa leo jumatatu katika tovut ya shirikisho la mpira wa miguu Serbia imesema "Golie wa Bruges,Bojan Jorgacevic ameitwa katika kikosi cha timu hiyo ya Taifa kuchukua nafasi ya Stojkovic 

Stojkovic alitolewa katika kipindi cha kwanza  katika mechi ambayo Partizan' waliibuka na ushindi wa 2-1  wakiwa nyumbani dhidi ya Javor Ivanjica  na kukimbizwa hospital huku kwa matokeo hayo Partizan  Wamekwea kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya soka ya Serbia.

Serbia, who top Group A on goal difference with four points from two games, entertain Belgium at Red Star's Marakana stadium on Friday before visiting neighbours Macedonia on October 16.

Udinese keeper Zeljko Brkic is favoured to stand in for Stojkovic, given that Jorgacevic's last competitive international was a 1-0 defeat to Slovenia in a Euro 2012 qualifier when he conceded a goal from the halfway line.


Suarez AFUNGIWE kwa kujidondosha makusudi!

Chapisha
Toleo la kuchapisha

MENEJA STOKE CITY, Pulis, aitaka FA imuadhibu Suarez!!

MENEJA mwingine ataka RVP aadhibiwe!!

Bosi wa Stoke City Tony Pulis amekitaka Chama cha Soka England, FA, kimuadhibu Straika wa Liverpool Luis Suarez kwa tabia yake ya kutaka kuwahadaa Marefa kwa kujidondosha makusudi ndani ya boksi ili apate Penati.

Jana, Stoke City ilikuwa Anfield kucheza na Liverpool kwenye Mechi ya Ligi Kuu England ambayo ilimalizika 0-0 na katika Kpindi cha Pili Luis Suarez ‘alijidondosha’ kutaka Penati ambayo Tony Pulis anaamini ulikuwa ni udanganyifu.


Pulis amesema: “Siku nyingi nimepigia kelele hili na Kipindi cha Pili tukio moja lilikuwa aibu kubwa! FA walitazame hili. Wampe Kifungo Mechi 3 na ataacha kujirusha!”

Alipohojiwa, Meneja wa Liverpool, Brendan Rodgers, alijibu: “Sikuona tukio hilo hivyo siwezi kusema chochote lakini chochote anachofanya Luis litakuwa tatizo tu!”

Hata hivyo, kuhusu tukio la Suarez kujidondosha kwa makusudi, FA haiwezi kuchukua hatua yeyote ile kwani Sheria zinawaruhusu kutoa adhabu pale tu matukio yalistahili Kadi Nyekundu na Refa hakuona na si matukio ambayo yangestahili Kadi ya Njano.

-----------------------------------------------------

Robin van Persie

Wakati huo huo, Meneja wa Newcastle United  Alan Pardew ameitaka FA imwadhibu Straika wa Manchester United Robin van Persie kwa kile alichodai kumpiga ‘kipepsi’ Kiungo wa Newcastle, Yohan Cabaye, katika Mechi ya jana ya Ligi Kuu England huko Sports Direct Arena ambayo Manchester United iliitandika Newcastle bao 3-0.


Ingawa mwenyewe amekiri hakuliona tukio ambalo lilitokea wakati si Van Persie wala Cabaye kuwa na mpira huku wote wakikimbilia golini, Pardew amedai: “Van Persie alimtazama Cabaye na kumpiga kiwiko, nikiwa mkweli, FA walitazame tukio hilo.”

FA inaweza kulipitia tukio hilo na kutoa adhabu ikiwa tu Refa wa Mechi hiyo, Howard Webb, atakiri hakuliona tukio hilo na kama angeliliona angetoa Kadi Nyekundu.



Uingereza!!!!!


Barclays Premier League | LOGS

PosTeamPWDLGFGAGDPts
1Chelsea76101541119
2Man Utd7502179815
3Man City7430158715
4Everton7421148614
5Tottenham7421138514
6West Brom7421117414
7Arsenal7331135812
8West Ham732288011
9Fulham73131511410
10Newcastle7232811-39
11Swansea7223121118
12Stoke71516518
13Sunderland614157-27
14Liverpool7133912-36
15Wigan7124713-65
16Aston Villa7124612-65
17Southampton71151220-84
18Reading6033813-53
19Norwich7034517-123
20QPR7025616-102
Print