TRANSLATE THIS BLOG

Saturday, September 1, 2012

Kura za uchaguzi wa Angola zahisabiwa 

Kura zinahisabiwa baada ya uchaguzi mkuu nchini Angola.
Wafuasi wa chama tawala cha MPLA
Mwandishi wa BBC mjini Luanda anasema ingawa kulikuwa na mvutano hapo kabla, lakini upigaji kura wenyewe wa Ijumaa unaonesha ulikwenda vema.
Huu ni uchaguzi wa pili tangu kumalizika kwa vita virefu vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.
Hata hivo kulikuwa na malalamiko kwamba kumetokea ulalamishi, huku baadhi ya wapigaji kura walikataliwa kura kwa sababu majina yao hayakuwemo kwenye daftari.
Rais Jose Eduardo dos Santos - ambaye amekuwa madarakani kwa zaidi ya miaka 30 - anataraji chama chake kitashinda na hivo kumpa yeye muhula mwengine wa uongozi

No comments:

Post a Comment