TRANSLATE THIS BLOG

Friday, September 7, 2012


BPL: Yatafakari kubana Mishahara Mikubwa Wachezaji, Matumizi kwa Klabu!

BARCLAYS_PREMIER_LEAGUE_LOGO_2012.png

Msimu ujao, wa Mwaka 2013/14, UEFA inaanza rasmi kutumia zile Sheria zake mpya za kila Klabu kuishi kwa Mapato na Matumizi yake ya Mwaka wa Fedha husika, na Wasimamizi wa Ligi Kuu England wamekutana na kupendekeza Mishahara ya Wachezaji pamoja na Bajeti za Klabu zifuate mfumo mpya wa UEFA.

Klabu za England zinategemea mapato yao kuongezeka maradufu baada ya Makataba mpya wa TV kwa Kipindi cha 2013/16 kusainiwa hivi karibuni.

Wakati Manchester United na Arsenal zinataka Klabu za England zikubaliane tangu sasa na Sheria mpya za UEFA za kuzuia Mishahara mikubwa kwa Wachezaji na Klabu kujiendesha yenyewe kwa Mapato yake, zipo Klabu nyingi haziafiki hayo.

Kwa mujibu wa taratibu za FA, lazima Klabu 14 ziafike kati ya 20 ili Sheria ibadilishwe.

Ukiziondoa Klabu Tajiri Chelsea na Manchester City, Klabu nyingine ambazo hazijiafiki msimamo huu mpya ni Fulham, Everton, West Bromwich Albion, Newcastle na Tottenham Hotspur.

Klabu ambazo zimesimama kidete Sheria hii mpya ifuatwe ni West Ham, ambayo Mwenyekiti wake David Gold anataka kuwepo na kima maalum ya kiwango cha juu cha Mishahara ya Wachezaji.

David Gold yuko msimamo mmoja na David Whelan wa Wigan.

Peter Coates, Mmiliki wa Stoke City, amesema: “Nategemea tumekubaliana. Haiwezekani Fedha zote hizi ziwe za Wachezaji tu.”

Klabu zote 20 zimefikia maafikiano ya kuweka Makundi mawili ya Timu 10 kila moja ambayo yatatoa Ripoti zao mwishoni mwa Desemba ili uamuzi utoke.


No comments:

Post a Comment