TRANSLATE THIS BLOG

Monday, September 10, 2012


WAKUFUNZI WA WAAMUZI WA FIFA WAMEANZA KUNOLEWA


KOZI ya wakufunzi wa waamuzi (Futuro III Refereeing Course) ya Shirikisho la Kimataifa la Soka  (FIFA) Imeanza leo kwenye hoteli ya Holiday Inn jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF) Boniface Wambura, kozi hiyo imeanza saa tatu asubuhi imeshirikisha  jumla ya washiriki 69 kutoka nchi 21 za Afrika.

Amesema kozi hiyo inayotarajiwa kumalizika Septemba 22 mwaka huu inafanyika katika maeneo mawili ya ufundi (technical) na utimamu wa mwili (fitness).

 Nchi washiriki ni Afrika Kusini, Botswana, Eritrea, Ethiopia, Gambia, Ghana, Kenya, Lesotho, Liberia, Malawi, Mauritius, Namibia, Nigeria, Seychelles, Sierra Leone, Somalia, Swaziland, Tanzania, Uganda, Zambia na Zimbabwe.

“Washiriki kutoka Tanzania kwenye kozi hiyo ni Joan Minja, Leslie Liunda na Soud Abdi (technical) na Riziki Majalla (fitness),”.

Wambura amesema   baadhi ya wakufunzi wa kozi hiyo wanaotoka FIFA na Shirikisho la soka Afrika (CAF) ni Carlos Henriques anatoka Afrika Kusini, Fernando Gracia (Hispania), Steve Bennett (Uingereza), Tarek Bouchamaoui (Tunisia), James Sekajugo (Uganda), Bester Kalombo (Malawi), Felix Tangawarima (Zimbabwe) na An-Yan Lim Kee Chong (Mauritius).

Aidha, Wambura amesema kozi hiyo imefunguliwa na Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Leodegar Tenga ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya CAF na mjumbe wa Kamati ya Vyama (Associations Committee) ya FIFA.

No comments:

Post a Comment