TRANSLATE THIS BLOG

Tuesday, September 4, 2012

Zenit sign Hulk & Witsel for £64m

Baada ya muda mrefu wa tetesi wapi atatua Klabu Bingwa ya Urusi, 
Zenit St Petersburg, imetangazakuwanasa kwa mpigo Straika wa Brazil
 Hulk kutoka FC Porto na Kiungo wa Ubelgiji Axel Witsel kutoka Benfica.

Hulk

Wachezaji hao wawili tayari wameshaini Mikatabaya Miaka mitano kila mmoja..

Dili hizi za kuwanasa Wachezaji hao zilitangazwa rasmi kwenye Tovuti ya

Klabu hiyo na iliwapa hongera Mashabiki wake kwa habari hizo nzuri.

Hata hivyo, hadi sasa haikutajwa Wachezaji hao wamenunuliwa kwa Dau

 lipi lakini inasemekana Wakala wa Hulk, Teodoro Fonseca, alitamka 

kuwa Hulk amenunuliwa kwa Euro Milioni 60.

TAARIFA NILIOIPATA PUNDE NIKWAMBA HULK AMENUNULIWA KWA  £32m

Hulk, mwenye Miaka 26 ambae alijiunga na FC Porto akitokea Ligi 

ya JapanMwaka 2008, ameshatwaa Ubingwa wa Ureno mara 3 

pamoja na Taji la EuropaLigi Mwaka 2011 na ameifungia Brazil goli 5

 katika Mechi 14 alizocheza.

Nae Witsel, Miaka 23, inadaiwa amesajiliwa na Zenit kwa Dau la 

EURO MIL 40,alijiunga na Benfica Julai 2011 akitokea Standard 

Liege ambayo ilimuuza kwa Ada ya Euro Milioni 8.

katika upande wa michuano ya klabu bingwa ulaya zenet ipo kundi 

moja na vilabu AC Milan and Anderlecht.

Kwa sasa ndio wanaoongoza msimamo wa ligi kuu ya soka Russian 
league wakiwa teyari wameshajizolea 16 points katika michezo 7.

No comments:

Post a Comment