UEFA CHAMPIONZ LIGI: Tathmini Mechi za leo Jumanne!
BIGI MECHI ni Santiago Bernabeu Real Madrid v Man City!!.....
Jumanne ya leo Septemba 18 ndio mwanzo rasmi wa Michuano
ya hatua ya Makundi ya UEFA ya kusaka Klabu Bingwa Ulaya,
UEFA CHAMPIONZ LIGI, na zitakuwepo Mechi 8 za Makundi A
hadi D lakini, bila shaka, kati ya hizo, BIGI MECHI, ile
Mechi ya Mvuto, ni ile itakayochezwa Uwanja wa Santiago
Bernabeu kati ya Mabingwa wa Spain Real Madrid na Mabingwa
wa England, Manchester City.
=====================
RATIBA:
[Mechi zote kuanza Saa 3 Dak 45 Usiku, TANZANIA]
Jumanne Septemba 18
GNK Dinamo - FC Porto
Paris Saint-Germain FC - FC Dynamo Kyiv
Montpellier Hérault SC - Arsenal FC
Olympiacos FC - FC Schalke 04
Málaga CF - FC Zenit St. Petersburg
AC Milan - RSC Anderlecht
Borussia Dortmund - AFC Ajax
Real Madrid CF - Manchester City FC
=====================
TATHMINI MECHI ZA JUMANNE
KUNDI A
-GNK Dinamo Zagreb v FC Porto
-Paris Saint-Germain FC v FC Dynamo Kyiv
=====================
Klabu ‘Tajiri’ Paris Saint-Germain wanarejea tena kwenye
UEFA CHAMPIONZ LIGI kwa mara ya kwanza tangu Msimu
wa 2004/5 na watakuwa wenyeji wa Dynamo Kiev
Uwanjani Parc des Princes.
PSG, chini ya Meneja Carlo Ancelotti, wameanza vyema
kwenye Ligi ya Ufaransa, Ligi 1, kwa kutoka sare Mechi 3 na
kushinda mbili huku Straika wao mkubwa Zlatan
Ibrahimovich akipiga bao 5.
Mbali ya Ibrahimovich, PSG wanao hatari nyingine kina
Javier Pastore na Ezequiel Lavezzi na pia kuanza tena
kucheza kwa Beki toka Brazil, Thiago Silva, ambae hajaichezea
Timu yake mpya baada ya kuumia akiwa na Brazil
kwenye Michezo ya Olimpiki, kutawaongezea nguvu.
Lakini Dynano Kiev sio nyanya na wameanza vyema
kwenye Ligi yao ya Ukraine kwa kupoteza Mechi mbili
tu kati ya 9 walizocheza huku tishio lao kubwa likitoka
kwa Mnigeria Ideye Brown ambae amewafungia
bao 8 Msimu huu.
Kwenye Kiungo, Dynamo Kiev wanae Mchezaji wa zamani
wa Tottenham Niko Kranjcar ambae kwenye Ligi ya
Ukraine amepachika bao 4.
Mechi nyingine ya Kundi A ni ile itayochezwa Stadion Maksimir
kati ya wenyeji Dinamo Zagreb na FC Porto.
Wakiwa bila ya Straika wao mahiri kutoka Brazil, Hulk, ambae
wamemuuza kwa Zenit St Petersburg, FC Porto
watawategemea Lucho Gonzalez na James Rodriguez
kuwapatia magoli.
Lakini Dinamo Zagreb, wakiwa na mashine yao ya Kibrazil
ya magoli, Sammir, hawajafungwa hata Mechi moja
kwenye Ligi yao Msimu huu, wapo kileleni, na
watataka kufuta uchungu wa Msimu uliopita ambao
kwenye UEFA CHAMPIONZ LIGI walifungwa Mechi zao
zote 6 za Kundi lao na kupachikwa jumla ya bao 22.
Moja ya vipigo hivyo 6 ni kile cha 7-1 mikononi
mwa Lyon na kuleta uzushi kuwa wamepanga matokeo.
KUNDI B
-Montpellier Hérault SC v Arsenal FC
-Olympiacos FC v FC Schalke 04
=====================
Straika wa Arsenal, Olivier Giroud, anarudi tena Klabu
yake ya zamani Montpellier ambayo ilimuuza kwa
Arsenal kabla Msimu huu kuanza huku akiwa bado
akisaka bao lake la kwanza kwa Klabu yake
mpya katika Mashindano rasmi.
Arsenal wanatinga kwenye Mechi hii ya Ulaya wakitoka
kuitandika Southampton bao 6-1 hapo juzi mechi
ambayo walicheza bila ya Giroud ingawa
Mchezaji wao mpya mwingine, Lukas Podolski, aling’ara.
Tofauti na Arsenal, Mabingwa wa Ufaransa
Montpellier wanatinga kwenye Mechi hii wakiwa
wanasuasua huko kwao kwenye Ligi 1 wakiwa
wameshinda Mechi moja tu kati ya 5 walizocheza
ikiwa ni pamoja na kichapo cha 3-1 mikononi
mwa Reims Ijumaa iliyopita.
Katika Mechi nyingine ya Kundi B, Schalke watakuwa
safarini kucheza Uwanja wa Karaiskakis nyumbani
kwa Mabingwa wa Ugiriki Olympiacos ambao
wameanza vyema kutetea Taji lao kwa
kushinda Mechi zao zote 3.
Tishio kubwa kwa Olympiacos ni toka kwa Schalke
ni lile la Straika wa Holland Klaas-Jan Huntelaar
ambae ni mfungaji hatari.
KUNDI C
-Málaga CF v FC Zenit St Petersburg
-AC Milan v RSC Anderlecht
=====================
AC Milan, walioanza vibaya kwenye Ligi yao ya Italy
Serie A na pia kuchapwa 1-0 hivi juzi na Atalanta,
wanawakaribisha Timu ngumu ya Anderlecht ya
Ubelgiji ambayo huko kwao haijafungwa katika Mechi 7.
Chini ya Kocha Massimiliano Allegri, AC Milan bado
inayumbishwa na kuondokewa kwa Nyota wao
kadhaa Msimu huu ambao ni Zlatan Ibrahimovic
na Thiago Motta waliokwenda Paris Saint-Germain
na wengine ni Wakongwe Alessandro Nesta,
Filippo Inzaghi, Gianluca Zambrotta, Gennaro Gattuso,
Mark van Bommel na Clarence Seedorf.
Pia AC Milan imempoteza Straika Antonio Cassano
ambae walibadilishana na yule wa Inter Milan
Giampaolo Pazzini lakini pia wameweza kununua
Wachezaji wawili, Kiungo Nigel de Jong
na Beki Francesco Acerbi.
Mechi nyingine ya Kundi C ni kati ya Timu mbili ambazo
zimeanza vizuri Ligi za nyumbani kwao ambazo ni
Malaga ya Spain na Zenit St Petersburg ya Urusi.
Ingawa Malaga wamempoteza Santi Cazorla
alieenda Arsenal lakini kwenye La Liga
wanafanya vyema na wako nafasi ya pili.
Zenit St Petersburg, chini ya Kocha Luciano Spalletti,
wanafanya vyema hasa ukuta wao imara na
Straika Alexander Kerzhakov amekuwa akifunga
bao zao nyingi kabla na kuimarishwa kwa
kuwanunua Hulk na Kiungo Axel Witsel.
KUNDI D
-Borussia Dortmund v AFC Ajax
-Real Madrid CF v Manchester City FC
=====================
Mechi ya Real Madrid na Manchester City Uwanjani
Santiago Bernabeu ndio gumzo la kila pembe Duniani.
Man City, chini ya Kocha Roberto Mancini, Msimu
uliokwisha walishindwa kuvuka hatua ya Makundi
ya UEFA CHAMPIONZ LIGI na safari hii tena wako
kwenye ‘Kundi la Kifo’ ambalo pia wako Mabingwa
wa Ujerumani Borussia Dortmund na Mabingwa
wa Holland, Ajax Amsterdam.
Hii ndio Mechi ambayo, pengine, itathibitisha
kukomaa kwa Man City lakini pengine imekuja
kwao kwenye wakati mbaya kwani Real Madrid,
chini ya Kocha makeke Jose Mourinho, wako
kwenye wakati mgumu kwenye La Liga baada ya
kuanza utetezi mbovu wa Taji lao huko Spain.
Wakati Man City hawajafungwa kwenye Ligi Kuu
England wakiwa nafasi ya 4, Real Madrid wameshinda
Mechi moja tu na wapo nafasi ya 14 kwenye La Liga
huku wakigubikwa na utata kuhusu hatima ya Staa
wao mkubwa Cristiano Ronaldo ambae amebainisha
hana furaha Klabuni hapo.
Hii ni Mechi ambayo Mourinho lazima ashinde ili kurekebisha
Jahazi lake linaloenda mrama na hilo, pengine, linaweza
kuashiria maafa kwa Man City.
Mechi nyingine ya Kundi D ni ile itakayochezwa
Westfalenstadion, Uwanja ambao unasifika kwa
kelele, pale Ajax Amsterdam watakapotua kuwavaa
wenyeji Borussia Dortmund.
Baada ya kumpoteza Shinji Kagawa aliehamia Manchester
United, Dortmund walimnunua Marco Reus toka
Borussia Moenchengladbach na amekuwa moto.
Lakini Ajax, chini ya Staa wa zamani wa Holland Frank de Boer
, si mzaha na Msimu huu hawajapoteza Mechi.
Ajax, licha ya kuwapoteza Wachezaji wao Jan Vertonghen
(aliekwenda Tottenham), Gregory van der Wiel (Paris Saint-Germain)
na Vurnon Anita (Newcastle United), bado wanao
wengine tishio kina Thulani Serero, Tobias Sana na Siem de Jong.
RATIBA:
[Mechi zote kuanza Saa 3 Dak 45 Usiku, Bongo Taimu]
Jumatano Septemba 19
FC Shakhtar Donetsk - FC Nordsjælland
Chelsea FC - Juventus
LOSC Lille - FC BATE Borisov
FC Bayern München - Valencia CF
FC Barcelona - FC Spartak Moskva
Celtic FC - SL Benfica
Manchester United FC - Galatasaray A.S.
SC Braga - CFR 1907 Clu
No comments:
Post a Comment