TRANSLATE THIS BLOG

Saturday, September 1, 2012

kichapooo

Anusurika kifo baada ya kumchoma mwenzake kisu tumboni mjini Moshi



Jamaa huyu ambaye jina lake halikuweza fahamika mara moja akiwa hoi katika stendi kuu ya mabasi mjini Moshi baada ya kutembezewa kipigo na wananchi wenye hasira kali.hali hii ilikuja baada ya jamaa huku kumsadikiwa kumchoma mwenzake kisu cha tumboni.Jamaa akihemea juu juu baada ya msaada wa askari polisi kutokea na kumuokoa katika kipigo hicho.akisaidiwa kuinuka.akiingizwa kwenye Deffender ya polisi waliofika eneo hilo kumuokoa.
Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii Moshi.
MTU mmoja ambaye jina lake halikufahamika mara moja amenusurika kifo baada ya wananchi wenye hasira kumkimbiza ,kumkamata na kuanza kumshushia kipigo baada ya kumchoma mwenzake kwa kisu tumboni.
Tukio hilo lilitokea jana majira ya saa 10 jioni katika eneo la kituo kikuu cha mabasi ambapo kwa mujibu wa mashuhuda kijana aliyepigwa na wananchi alionekana kumkimbiza mwenzake ambaye alijitahidi kukimbia bila mafanikio.
Mashuhuda hao wameeleza kuwa baada ya kumfikia karibu kijana huyo alitoa kisu na kumchoma mwenzake tumboni ndipo alianguka pale pale huku wananchi waliokuwa karibu na tukio wakamnyanganya kisu .
Hata hivyo wakati wasamalia wema hao wakijaribu kumsaidia kijana aliyechomwa kisu ndipo mtuhumiwa huyo alifanikiwa kuwakimbia wananchi waliokuwa wamemshikilia.
Wamesema baada ya kukimbia ndipo wananchi wakapiga yowe hatimaye akakamatwa katikati ya kituo cha mabasi na kuanza kumshushia kipigo toka kwa wananchi ..........
 

Kijana aliyechomwa kisu alikimbizwahospitali ya mkoa wa Kilimanjaro,Kitete huku askari polisi wakifanikiwa kumuokoa mtuhuhimiwa ambaye naye pia alichukuliwa na kupelekwa hosptali yaKitete.

Kamanda wa polsi Robert Boaz amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.
                                               kwamsaada wa Michuzi BLOG!!!!!!!!!!!!

No comments:

Post a Comment