TRANSLATE THIS BLOG

Monday, September 24, 2012


TERRY ABWAGA MANYANGA KUCHEZEA ENGLAND!!


LEO KUMKABILI PILATO wa FA kwa TUHUMA za UBAGUZI!!...........

John Terry, Nahodha wa Chelsea ambae ameichezea England mara 78, ametangaza kustaafu kuichezea Timu ya Taifa ya England huku leo akitakiwa kufika mbele ya Jopo la FA, Chama cha Soka England, akikabiliwa na tuhuma za kumkashifu kibaguzi Beki wa QPR Anton Ferdinand wakati wa Mechi ya Ligi Kuu England iliyochezwa Loftus Road Mwezi Oktoba Mwaka jana kati ya QPR na Chelsea.

 Akitangaza kustaafu kwake kuichezea England, Terry alisema kuendelea kuichezea England huku FA imeamua kumshitaki wakati Mahakama imemsafisha kunamwia vigumu.

Mara baada ya tukio hilo la kutuhumiwa kukashifu kibaguzi, FA ilifungua uchunguzi lakini suala hilo likadakwa na Polisi na hatimae kutua Mahakamani baada ya Shabiki mmoja kulalamika lakini Terry alishinda Kesi hiyo Mwezi Julai.

Mara tu baada ya Kesi Mahakamani kumalizika, FA ilifungua tena uchunguzi wake na kuamua kumshitaki Terry na endapo atapatikana na hatia huenda akafungiwa kwa muda mrefu kama alivyofanyiwa Luis Suarez wa Liverpool baada ya kumkashifu kibaguzi Patrice Evra wa Manchester United.

John Terry, ambae alianza kuichezea Chelsea tangu ana Miaka 14, alianza kuichezea England Mwaka 2003 na kuteuliwa kuwa Kepteni wake Mwaka 2006 baada ya David Beckham kujiuzulu wadhifa huo.

Mwaka 2010, Terry alinyang’anywa Ukepteni na Meneja wa wakati huo Fabio Capello baada ya kuibuka skandali la kutembea na Bibi wa Mchezaji mwenzake wa Chelsea na England Wayne Bridge.

Lakini, baada ya kuumia aliekuwa Nahodha wa England Rio Ferdinand, Terry alipewa tena Ukepteni ambao alinyang’anywa na FA Februari Mwaka huu kufuatia kuamuliwa kupelekwa Mahakamani kwa tuhuma za kumkashifu kibaguzi Beki wa QPR Anton Ferdinand, kitendo ambacho pia kilimfanya

No comments:

Post a Comment