TRANSLATE THIS BLOG

Monday, September 10, 2012



thumb.php.jpg

Timu za Simba na Azam zimeandika barua Shirikisho la Soka nchini (TFF) kuomba mchezo wao wa kesho wa Ngao ya Jamii uchezwe usiku. Mchezo huo umepangwa kuanza saa kumi alasiri, lakini zenyewe zinataka uanze saa 12 jioni ama saa moja usiku.

Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Geofrey Nyange ‘Kaburu’, alisema jana kuwa walikaa pamoja na Azam kuomba TFF wabadili muda wa kuanza pambano hilo hadi saa 12 jioni. 

“Tulikaa na Azam tukaandika barua ya kuwaomba TFF wasogeze mbele muda wa kuanza mchezo huo, maana saa 10 watu wengi wanakuwa bado wako makazini,”alisema Kaburu. Mchezo wa Ngao ya Jamii ni ishara ya ufunguzi wa Ligi Kuu Tanzania Bara inayotarajiwa kuanza Jumamosi ijayo.

No comments:

Post a Comment